BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Showing posts with label UWANJA WA MASTAA. Show all posts
Showing posts with label UWANJA WA MASTAA. Show all posts

Wednesday, 21 March 2018

21 March

TAARIFA JUU YA KESI YA NONDO NA HATIMA YAKE

Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi, Abdul Nondo

Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi, Abdul Nondo amerudishwa mkoani Iringa na kufikishwa Mahakama ya Wilaya. Awali Nondo alitolewa Iringa baada ya mahojihano na Polisi na kupelekwa Dar kwa Mkurugenzi wa Upelelezi makosa ya Jinai kwa mahojiano.

Kwa mujibu wa Wakili wake, Jebra Kambole, amesema dhamana ya Nondo itatazamwa Jumatatu ijayo baada ya hakimu kuomba kusoma sheria inasemaje juu ya kuzuiwa dhamana kwake.

Imeelezwa kuwa, Nondo amesomewa mashtaka kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo Mitandaoni na kosa la pili ni kudanganya kuwa katekwa. Shauri limeahirishwa na mtuhumiwa amepelekwa rumande. 


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Tuesday, 20 March 2018

20 March

ALIYOFUNGUKA MANWATER KUHUSU UJIO MPYA WA ALIKIBA

Msanii mkongwe wa muziki wa BongoFleva-Alikiba

Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa BongoFleva, Man Water amefunguka na kuwahakikishia mashabiki wa Alikiba kuwa kuna ngoma mpya imeshafanyika mpaka 'video' na muda wowote kutoka sasa inaweza kuachiwa ili kuvunja ukimya uliokuwepo kwa kipindi kirefu.

Man Water amebainisha hayo wakati alipokuwa anapiga stori na 'BIG CHAWA' kutoka katika kipindi cha Planet Bongo 'PB' ya East Africa Radio baada ya kuwepo na malalamiko mengi yanatoka kwa mashabiki wake waliokuwa wanadai wanataka kumsikia mfalme wao aking'uruma katika muziki.

"Kuna ngoma ambayo tumefanya na imeshafanyiwa video tayari kwa jinsi nilivyosikia, kwasababu Alikiba yupo South Afrika 'SA'. Pengine wimbo huo unaweza ukawa ndio unaofuata kwa sasa baada ya 'Seduce me", amesema Man Water.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
20 March

IJUE REKODI YA MADAKTARI WANAOMTIBU TUNDU LISSU

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.


HUU ndio ukweli! Madaktari wawili waliobobea wanaomtibu Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu, Profesa Stefaan Nijs na Profesa Willem-Jan Mertsemakers wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg, Ubelgiji ni wataalamu waliobobea kwa upasuaji barani Ulaya, UWAZI limegundua.

Kwa mujibu wa mtandao wa hospitali hiyo ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg Ubelgiji,madaktari hao wametajwa kuwa ni wataalamu wa ubasuaji wa hali ya juu wanaotegemewa katika Bara la Ulaya.Maprofesa hao wamebainishwa kuwa ndio waliofanya kazi kubwa kuokoa maisha ya majeruhi wa bomu lililolipuliwa na magaidi Machi mwaka jana nchini Ubelgiji.

“Profesa Stefaan Nijs ambaye ni mkuu wa idara ya mafunzo ya udaktari chuoni hapo ndiye aliyeongoza kikosi cha madaktari wengine akiwemo Profesa Willem- Jan Mertsemakers kutibu na kuwafanyia upasuaji waliojeruhiwa na bomu, yeye na timu yake ndio waliowafanyia upasuaji wa hali ya juu waathirika wa mlipuko wa bomu na kuokoa maisha ya majeruhi wengi, ”lilisema gazeti Telegraph nchini humo.

Imeelezwa kuwa madaktari hao ni maarufu siyo tu Ubelgiji, bali pia nchi mbalimbali za Ulaya na wameshapewa tuzo mbalimbali kutokana na kuokoa maisha ya watu sehemu mbalimbali duniani.

Habari kutoka Hospitali ya Leuven na kuthibitishwa na Lissu ambaye pia Mwenyekiti wa Chama Cha Wanasheria Tanzania (TLC),zinasema madaktari hao ndio waliogundua kuwa goti la mwanasiasa huyo lina shida kubwa na linahitaji upasuaji la sivyo hata kama angepona kungewezekana kuvunjika tena siku za usoni.


Profesa Stefaan Nijs.

Lissu tayari amefanyiwa upasuaji kama alivyoshauriwa na madaktari hao na alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema operesheni hiyo iliyochukua saa mbili, ilifanywa na timu ya madaktari bingwa chini ya uongozi wa Profesa Willem-Jan Mertsemakers.“Operesheni ilienda vizuri na kwa sasa naendelea na dawa na mapumziko hospitalini kwa muda wa angalau wiki tatu zinazokuja, ” alisemaLissu katika taarifa yake.

Akaongeza: “Wameniwekea chuma cha kuimarisha mfupa wote wa paja la kulia. Pia wamechukua vipimo ili kuangalia kama hakuna tatizo la bacteria kabla hawajafunga kabisa sehemu ya kwenye goti ambayo haijaunga hadi sasa.

”Mke wake, Alicia Lissu alisema anamshukuru Mungu kwamba upasuaji huo umekwenda vyema.Wakati Lissu akisema hayo huko Ubelgiji, kaka yake,Wakili Alute Mughwai ambaye ndiye msemaji wa familia yao,alisema wameelezwa kuwa baada ya siku 10, madaktari watatoa taarifa juu ya maendeleo ya afya yake na mazoezi ya viungo ambayo alikuwa anaendelea nayo.

Alipoulizwa na gazeti hili atarudi lini ndugu yake alikuwa na haya ya kusema:“Kutokana na maelekezo ya madaktari kwa sasa, hatuwezi kusema Lissu atarudi lini nchini, kwani upasuaji (aliofanyiwa wiki iliyopita) umesababisha alazwe tena hospitali,” alisema.

Mughwai aliwashukuru Watanzania wanaoishi Ubelgiji kwa mchango mkubwa wanaotoa katika matibabu ya Lissu, kama ilivyokuwa kwa Watanzania wanaoishi Nairobi, Kenya. Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma alipokuwa anahudhuria vikao vya bunge, baada ya shambulizi alipelekwa Nairobi Kenya kwa matibabu na baada ya miezi mitatu alisafirishwa kupelekwa nchini Ubelgiji kwa hatua nyingine ya matibabu ambako ndipo alipo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Sunday, 18 March 2018

18 March

RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA ATAKA HUITISWAJI WA MJADALA WA KITAIFA KUHUSU HALI YA ELIMU NCHINI


Rais Mstaafu, Benjamin Mkap
DODOMA: Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesema ni muhimu kuitishwa mjadala wa kitaifa ili kujadili hali ya elimu nchini

Amefafanua kuwa ni lazima taifa litafakari kwanini shule za serikali zinaendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kila mwaka

Aidha, Mkapa ameshauri mjadala huo uhusishe makundi yote ya jamii wakiwemo wadau kutoka sekta binafsi, wasomi pamoja na wananchi wa kawaida ili kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo hilo

Mkapa ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ameyasema hayo wakati wa tukio la kumkaribisha Makamu Mkuu mpya wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Egid Mubofu na kumuaga aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo aliyemaliza muda wake, Profesa Idrisa Kikula.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Saturday, 17 March 2018

17 March

NCHEMBA AWAFUNDA WANAFUNZI WANAOJIHUSISHA NA SIASA VYUONI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba March 16, 2018 amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza taswira mbaya juu ya serikali badala yake kuwa na mitazamo chanya.

Ameyasema hayo katika kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum, Ester Mmasi.

Amesema wanafunzi hawatakiwi kufanya harakati ili wawe adui wa serikali kwani serikali yenyewe haina muda wa kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.

“Nilishawahi kufanya harakati nikiwa chuoni na nilipewa jina la Chifu, majina yangu yamekuja kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya ajenda za Taifa ambazo niliona hazina manufaa,” – Dk Mwigulu Mchemba.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Tuesday, 13 March 2018

13 March

MAOFISA HABARI WAZEMBE KUKIONA CHA MOTOWAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema atawasilisha kwa Waziri Mkuu majina ya maofisa habari wazembe, ili watumbuliwe.

Alisema hayo kufuatia uzembe unaofanywa na baadhi yao huku wakibweteka kukaa maofisini bila kufanya kazi.

Alisema maofisa habari wasiojituma ni sawa na kuwa na maofisa habari hewa, ambao wanakula mishahara wasioifanyia kazi, jambo ambalo hakubaliani nalo.

Dk. Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa kazi wa siku tano wa maofisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini, unaofanyika jijini hapa, aliwataka kubadilika na kutekeleza malengo waliojiwekea.

"Kweli naangalia tovuti za halmashauri zipo tisa tu zinazofanya vizuri, zingine wahusika wamelala; na mikoa 18 tu inafanya vizuri kuhabarisha, sasa hawa wengine wajitathmini vinginevyo nitapeleka majina yao kwa Waziri Mkuu, ili watumbuliwe, tutoe ajira kwa wengine," alisema.

Aliwataka wafanye kazi ya kuhabarisha wananchi kazi zinazofanywa na serikali, ili wasitumbuliwe, Alisema hata wizara husika pia wapo wazembe nao atapeleka taarifa ngazi ya juu ili wachukuliwe hatua, lengo kazi nzuri zinazofanywa na serikali zitambulike kwa wananchi na kuziba mianya kwa wapotoshaji wa taarifa za serikali.

Dk. Mwakyembe aliwataka maofisa habari hao kujituma na kutoa taarifa za kazi zinazofanyika kila siku kwenye mitandao ya kijamii na endapo watazuiwa na mtu yeyote, wawafichue hata kwa siri ili wizara ishughulike na muhusika.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez, aliwataka maofisa habari hao kubadilika na kuleta tija kwa taifa baada ya mkutano huo kuisha.

Alisema dunia sasa imeunganishwa kwa teknolojia, hivyo ni vema jamii ikapata taarifa zilizo sahihi kwa wakati.

Aidha, alisema serikali pia inahitaji kusikiliza jamii na sauti za wananchi, ili kupiga hatua katika kufikia Tanzania ya Viwanda.

“Sisi kama wadau tunahitaji kusikia zaidi habari za wananchi wa vijijini, ili tuone jinsi wanavyobadilika katika hali walizonazo,” alisema.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Monday, 12 March 2018

12 March

MTENDAJI KATA YA BUKANDWE AJILIPUA KWA AJILI YA WANANCHI

Rais JPM kushoto na kulia kwake ni Mtendaji wa kata ya Bukandwe, mkoani Gaita Mh, Muberwa Bakalemwa
Mtendaji wa Kata ya Bukandwe Wilaya ya Mbogwe mkoa wa Geita, Muberwa Bakalemwa ni miongoni mwa Viongozi vijana ambao wamekua mstari Wa mbele kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa rika na watu wote katika jamii. Mtendaji huyo amekua mbele kuitendea kazi kauli mbiu ya rais magufuri ya HAPA KAZI TU kutoka na jukumu zimaalilojipa katika kuhakikisha anaboresha na kuinua elimu katika kata ya Bukandwe pia ikiwa ni sehemu ya kuunga jitihada za Mh JPM katika harakati ya kuijenga Tanzania ya viwanda.

Mtendaji Wa kata ya Bukandwe Mh Muberwa Bakalemwa akishirikiana na wananchi katika ujenzi Wa darasa

Mh, Muberwa akiwa ni moja ya viongozi shujaa na makini, ameamua kujitoa kwa dhati katika kuhakikisha wananchi wa kata ya Bukandwe na viunga vyake  wanafaidika na rasilimali walizonazo na kuhakikisha anaweka mikakati itakayo andaa rasilimali watu watakao ijenga Tanzania ya viwanda.

Kupitia jitihada zake, mh Muberwa, ameweza kutambua umuhimu elimu na kuweka jitihada na mipango thabiti  kuhakikisha kila mwanafunzi anasoma katika mazingira salama na rafiki hususani katika uboreshaji na ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye maeneo yenye kero zaidi.

Mnaomo mwezi January mwaka huu, wananchi wa bukandwe wakiongozwa na viongoji wao wakata na vijiji na vitongoji waliweza kujitolea kwa dhati na kufanikisha uchimbaji wa misingi miwili ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Bukandwe.

Hawakuishia hapo, tarehe 8 na 9 mwezi huu (march), wananchi Wa Bukandwe wakiongozwa na shujaa wao Mh Muberwa, walianza ujenzi wa misingi ya majengo hayo ili kuhakikisha wanapunguza huaba wa madarasa waliyokua nayo.
Mtendaji wa kata Mh Muberwa (kushoto) akishirikiana na wananchi kuchanganya mchanga kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa shule Bukandwe

Mtendaji akiwa mstari wa mbele katika ujenzi wa msingi wa shule ya msingi Bukandwe
 Akiongea na Edusportstz Leo, Muberwa amesema haya!

"Kwanza ningependa kushukuru wananchi pamoja na viongozi wenzangu Wa taifa, mkoa, wilaya, kata, vijiji na vitongoji kwa ushirikiana wanaonipa katika safari yangu ya kuhakikisha tunaijenga Bukandwe na kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wote"

"Katika kata ya bukanydwe, tunaupungufu wa vyumba vya madarasa 6, Lakini tumeridhia ifikapo mwezi wa 12 tuwetumefikia malengo tuliyojiwekea"

"Mpaka sasa, tumeanza na ujenzi wa vymba 4 ikiwa majengo mawili, yaani kila jengo litakua na ofisi moja na darasa moja"

"Pia tunamikakati ya kujenga mabweni mawili katika shule ya sekondari ya Kanengee na zahanati mbili za Bukandwe na Nhungwiza"

Mh, Muberwa amehitimisha kwa kusema kuwa anaomba viongozi, watu binafsi na wananchi kwa ujumla kumuunga mkono kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa majengo hayo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

12 March

VIDEO YA WAZIRI NCHEMBA "HATAMKIANDAMANA CHUMBANI TUTAWAKAMATA TU"

mwigulu nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dkt Mwigulu Nchemba, ametoa onyo kali kwa kikundi ama mtu yoyote atakayejaribu kufanya maandamano ya aina yoyote yatakayo plekea kuvuruga amani ya nchi. Waziri Nchemba ameyasema hayo alipohudhuria katika uzinduzi wa kiwanda cha Alizeti mkoani Singida.

BOFYA HAPA KUSIKIA VIDEO HII

 EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au
kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Sunday, 11 March 2018

11 March

MCHUNGAJI DR SHAYO AYAANIKA WAZI MAMBO 6 YANAYOITAFUNA NCHI


Mkuu wa pili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kilimanjaro Kati, Mchungaji, Fred Njama


Mkuu wa pili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kilimanjaro Kati, Mchungaji, Fred Njama amesema kuna mambo sita nchini ambayo hayako sawa.

Alitaja mambo hayo kuwa ni pamoja na hali ya uchumi, ajira kwa vijana, ughali wa matibabu na tangazo la elimu bure.

Mchungaji Njama ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa Usharika wa Karanga mjini Moshi, alitaja mambo mengine kuwa ni hali ya kisiasa nchini na kundi kubwa la wastaafu kutolipwa mafao yao. Alitoa kauli hiyo jana wakati akiwasilisha taarifa yake katika mkutano mkuu wa 21 wa usharika huo wa Karanga, uliohudhuriwa pia na Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk Martin Shao.

Mkutano huo mbali na kuhudhuriwa na mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Kati, Mchungaji Kennedy Kisanga na wachungaji wa sharika jirani, ulihudhuriwa pia na wawakilishi kutoka jumuiya 32.

Kauli ya Mchungaji Njama imekuja siku chache baada ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, (TEC) kuitaka Serikali ifufue mchakato wa uundwaji wa Katiba Mpya uliokwama.

Naibu Katibu Mkuu wa TEC, Padri Daniel Dulle alisema majadiliano yanahitajika ili kudumisha amani, heshima na kujenga taifa linaloheshimiana.


Hali ya uchumi

Akizungumzia hali ya uchumi nchini, Mchungaji Njama alisema awamu ya tano ilipoanza, watu walikuwa na mategemeo makubwa kwamba uchumi utaimarika lakini mambo yamekuwa tofauti.

“Umaskini unaendelea kuongezeka kwa nguvu. Tumeshuhudia biashara nyingi zikifungwa, wakulima wamekata tamaa, gharama za uzalishaji zimekuwa kubwa sana,” alisema Mchungaji Njama na kuongeza:

“Serikali haitoi ruzuku ila wakati wa kuuza mazao yao, wakulima hawajui wauze wapi na kwa bei gani. Wafugaji wanazalisha kwa gharama kubwa. Vyakula vya mifugo na dawa ni ghali.”

Hali ya kisiasa

Katika hotuba yake hiyo, Mchungaji Njama alisema kuna dalili za kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari na siasa.

“Inavyoelekea uhuru umeanza kuminywa. Ulianza kwenye siasa, ukaja kwenye vyombo vya habari... Kwa mfano takwimu za uchumi au chochote hata kama kina ukweli lakini utawala hautaki kusikia ukizungumzia hadharani au kwenye daladala ni kosa la jinai. Matukio ya miili kuokotwa yamezidi,matumizi ya risasi yameanza kuzoeleka kama kitu cha kawaida. Watu kupigwa risasi kwa walio wanasiasa na wasio wanasiasa yanafanya watu waishi kwa hofu.”

Baadhi ya matukio ya watu kupigwa risasi, ni pamoja na lile la Septemba mwaka jana, la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyeshambuliwa akiwa nje ya nyumba yake mjini Dodoma.

Kadhalika, tukio la hivi karibuni la mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini wakati wa maandamano.

“Hali hii ikiachwa, nchi itaingia kwenye umwagaji damu mkubwa,” alitahadharisha na kuungwa mkono na baadhi ya waumini.

Ukosefu ajira kwa vijana
Akizungumzia hali ya ajira nchini, Mchungaji Njama alisema miaka ya nyuma vijana walijua kwamba wakisoma watapata ajira, lakini leo imekuwa ni kinyume chake na karibu kila nyumba ina kilio.

“Karibu kila nyumba ina kijana aliyemaliza chuo kikuu au vyuo vya kati. Kundi la wasio na kazi limeongezeka maradufu na hii si dalili njema,” alisema.

Gharama za matibabu
Kwa upande wa matibabu, Mchungaji Njama alidai matibabu yamekuwa ghali akitolea mfano wa upasuaji wa kawaida kufikia Sh500,000 mbali na vipimo vya CT-Scan na MRI ambavyo ghamara yake pia kubwa.

“Watu wanashindwa kumudu gharama za matibabu. Bima za wasio na ajira za Serikali zinabagua matibabu na dawa. Wazee ambao wanapaswa kutibiwa bure imekuwa ni nadharia,” alidai.

Elimu bure
Mchungaji Njama alidai kuwa tangazo la elimu bure limeleta kushuka kwa elimu kuliko wakati wowote na kutolea mfano kuwa kati ya shule 100 zinazofanya vizuri, za Serikali ni chache.

“Ninashauri wajumbe wa mkutano mkuu tuwaelimishe wazazi wasicheze na maneno ya wanasiasa. Kuna msemo unaosema gharama ya ujinga ni kubwa kuliko gharama ya elimu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Askofu mstaafu Dk Shao, alilitaka kanisa hilo lisikae kimya na lichukue hatua ya kuzuia mafundisho potofu ndani ya kanisa, yanayotolewa na baadhi ya wachungaji.

Dk Shao alisema upungufu wa mafundisho ya kidini ni mkubwa na kuwataka wachungaji wa sharika za kanisa hilo, kutoruhusu kualika wahubiri wanaotoa mafundisho potofu kwa waumini.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
11 March

LISSU ATARAJIWA KUFANYIWA OPERATION NYINGINE MWEZI HUU

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu 

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine wa goti la kulia Machi 14, 2018 katika Hospitali ya Chuo kikuu cha Leuven, Gasthuisberg ili kumnusuru asipatikane na athari za mifupa kutojiunga kwa wakati.

Lissu amebainisha hayo usiku wa kuamkia leo wakati alivyokuwa anawafahamisha umma juu ya maendeleo ya afya yanavyoendelea huko alipo na kusema anaendelea vizuri na matibabu na sasa anaweza kusimama kwa miguu yote miwili bila ya msaada wa magongo ya kutembelea.

"Timu ya madaktari bingwa wa mifupa wanaonitibu, wamenitaarifu kwamba kasi ya mfupa wa juu ya goti kuunga ni ndogo sana na kwamba wasipoingilia kati na kurekebisha mfupa huo, itachukua muda mrefu sana kuunga na hata ukiunga baada ya huo muda mrefu, hautaunga kwa namna itakayoondoa hatari ya kuvunjika siku za mbeleni. Kwa sababu hizi, madaktari wangu wamependekeza kufanya operesheni nyingine kwenye mfupa wa juu ya goti la kulia", amesema Lissu.

Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "Niko kwenye mikono salama ya kitabibu. Madaktari wangu, Prof. Dr. Stefa Nijs na Prof. Dr. Willem-Jan Mertsemakers, ni madaktari bingwa wa mifupa wanaosifika barani Ulaya kwa utaalamu wao katika fani hiyo. Hivyo msiwe na hofu, Mungu wetu aliyeniwezesha kuwa hai sasa, ataendelea kutenda miujiza yake kupitia kwa madaktari bingwa hawa. Nitaendelea kuwataarifu maendeleo ya matibabu yangu kadri itakavyokuwa lazima na muhimu kufanya hivyo".

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana tangu Septemba 7,2017 akiwa mkoani Dodoma, na kisha kupelekwa nchini Nairobi kwa matibabu na baada ya miezi 3 alipelekwa nchini Ubelgiji kwa hatua nyingine ya matibabu.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Friday, 9 March 2018

09 March

TRUMP NA KIM JONG UN KUKUTATNA USO KWA USO

Rais Kim Jong Un kukutana na Trump

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu,na hivyo kuweka historia kufuatia kuwa kutokuwepo rais wa Marekani ambaye amewahi kuonana na kiongozi mkuu wa Korea kaskazini.

Hata hivyo mahala watakapokutana viongozi panasalia kuwa siri kwa sasa,na pia Marekani imesisitiza kuwa pamoja na kukubali ombi hilo la rais Kim Jong Un laini bado vikwazo vitasalia pale pale.

Tangazo hilo la kwamba rais Trump amekubali kukutana na Kim Jong Un,limetolewa na viongozi wa juu wa Korea Kusini uliofika mjini Washington kuwasilisha barua ya ombi hilo kutoka kwa Korea Kaskazini.

Kim pia amekubali kusitisha mpango wake wa nyuklia na majaribio yake makombora,msimamo ambao ni tofauti na aliokuwa nao rais huyo Kim Jong Un.

Hatua hii iliyofikiwa ya rais Kim Jong Un kulegeza msimamo ni matokeo ya mazungumzo mazito yaliyofanywa wiki chache zilizopita ujumbe wa Korea Kusini kukutana na kiongozi huyo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Wednesday, 28 February 2018

28 February

ORODHA YA NYIMBO 15 ZILIZOFUNGIWA NA TCRA LEO

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania

Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) imepokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA).

Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) imekataza nyimbo hizo kuendelea kurushwa kwenye vyombo vya habari mara moja, kituo kitakachokiuka amri hii kuchukuliwa hatua za kisheria.

Nyimbo hizo zina maadili ambayo ni kinyume na maadili na kanuni za huduma za utangazaji (Maudhui) 2005.
TCRA
Orodha ya nyimbo zilizofungiwa
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Monday, 26 February 2018

26 February

ANAANDIKA ZITTO KABWE; "UTAWALA HUU NI RAHISI KUUANGUSHA"


Kupitia ukurasa wake wa Twitter zitto kabwe anayaandika haya👇👇
Jambo moja nina hakika nalo kwa dhati ni kwamba utawala huu ni rahisi kuuangusha kikatiba kuliko wowote ule. Unapokuwa na Serikali yenye Mawaziri wasiokuwa Serikalini, watumishi wa umma wanaonyanyasika, Uchumi unaodidimia na dola inayokandamiza haki za watu. Nini zaidi? KURA


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Saturday, 24 February 2018

24 February

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI BAADA YA JPM KUREJEA NCHINITanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amerejea nchini kutoka nchini Uganda alikokuwa kwenye kutano wa wkuu wa nchi za Afrika Mashariki.

Mkutano huo ambao ulihusisha viongozi wa mchi zote za Jumuiya ya Afrika Mshariki, ulikuwa ni wa siku 2, ambapo pia alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Aliporejea akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza amepokelewa na mkuu wa mkoa huo John Mongela, na kujadili schangamoto mbali mbali zinazoukabili uwanja huo ikiwemo ujenzi wa jengo la abiria, ambalo ameahidi kulifanyia kazi.

Soma hapa taarifa yote

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ


Subscribe to EDUSPORTSTZ