EDUSPORTSTZ : MAHUSIANO

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts
Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts

Tuesday, 7 April 2020

KAMWE USIOMBE AMA KULAZISHA ABAKI NA WEWE KWENYE MAISHA YAKO, KUMUACHA AENDE KUNA FAIDA HIZI .
07 April

KAMWE USIOMBE AMA KULAZISHA ABAKI NA WEWE KWENYE MAISHA YAKO, KUMUACHA AENDE KUNA FAIDA HIZI .

Kamwe usiombe ama kulazimisha mtu abaki na wewe kwenye maisha yako kinyume na matakwa yake. Kumuacha aende kunakufungulia milango ya watu bora zaidi kuja kwako.
Maisha ni mafupi mno kuumizwa na kuchukuliwa kama ni option kila siku. Ni muda mzuri sasa wa kujiwekea nafsi yako kama kipaumbele cha kwanza!!
Maana, ipo siku moja mtu atakuja katika maisha yako na kufanya yale yaliyo sahihi ambayo wengine walishindwa kwako. Siku moja atakuja mtu katika maisha yako ambaye hutakuwa na haja ya kumkumbusha kuwa unampemda.
Atakuja mtu ambaye furaha yake ni kukuona ukikuwa kifikra, kiuchumi na kupendeza kimwonekano. Mtu ambaye utamuamini nae kukuamini kwa mambo yote madogo na hata yale makubwa.
Atakuja kuwa rafiki, mfariji, mshikaji, mtu wa karibu na partner wa maisha yako ambaye mtashea nae vitu vidogo mpaka vile vikubwa. Msingi usikate tamaa, kuwa na imani, muombe Mungu.
Usiyumbishwe na maneno ya kukatisha tamaa. Jitamkie yale yaliyo mema!!#reallove #be_sweet #SeeYouAtTheTop πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
#How is volume...?


MWANAMKE SOMA ILI UPATE KUJUA NAMNA NZURI YA KUISHI NA MWANAMKE
07 April

MWANAMKE SOMA ILI UPATE KUJUA NAMNA NZURI YA KUISHI NA MWANAMKE

Nisome Mwanamke ili upate kujua namna nzuri ya kuishi na Mwanaume;
• MFANYE MWANAUME AKUZOEE KIASI KWAMBA ASIWEZE KUHAMISHA HISIA ZAKE KWA MWANAMKE MWINGINEπŸ’―
Mapenzi PEKEE hayamfanyi Mwanaume kutulia hasa ukizingatia WANAUME kwa uhalisia wao wanapenda MAPENZI MAPYA bila kuangalia UBORA WA MWANAMKE HUSIKAπŸ˜‚
Mfanye Mwanaume akumbuke huduma zako muhimu kwake kuliko kuwekeza kwenye style na mikao ya kitandani maana hayo sio MAGENI kiumeniπŸ˜‚
Wengi mnajidanganya kwa sababu mmechezwaUNYAGO etiii Mwanaume atakuwa na wewe kwa sababu ya MAUNO yako wallah sio kila Mwanaume anapenda MAUNO na niwajuavyo wanaume makini wanamtazama Mwanamke kama MSHIRIKA WA MAISHA tofauti na wanaume wachache wanaomtazama Mwanamke kama DARAJA LA MAHITAJI YAO.
Mwanaume ukimfanya akuzoee atakuwa na mambo matatu ya faida kwako;
• WOGA WA KUMSHITUKIA.
• WOGA WA KUKUKOSA.
• WOGA WA KUHARIBU NURU ALIYO NAYO KWA UWEPO WAKO.
Mwanaume kwa HULKA ni mhuni ila wakati huo huo Mwanaume ni MWOGA WA KUHARIBU ikiwa tayari NAFSI YAKE IMETWAMA KWAKOπŸ’―
Mwanaume hatulizwi kwa MAPENZI 
Bali unaweza kumtuliza Mwanaume kwa sababu ndogo mno "UPOLE WAKO" halafu watu watasema wewe mchawiπŸ˜‚πŸ˜‚
Wanawake achaneni na mambo ya KUFIKIRIKA na mjitume kumjua Mwanaume mmoja mmoja maana HAWAFANANI japo hulka yao ni sawa ndo maana unaweza kumtofautisha JUMA NA PETER😎
Jenga ushawishi wa kumfanya Mwanaume ahisi upweke uwapo mbali nae hiyo itamfanya kukosa uthubutu wa kukusaliti, Ujinga wa Mwanamke ni kuwazia KUMKAMATA MWANAUME KI MAHABA huku akisahau Mwanaume anaweza kufanya ngono na mbuzi na akifika keleleni ije kuwa weweπŸ’ƒ
Mtu anayeweza kulala na wewe na akalala na nduhuyo halafu bado unajifunza utundu kitandani ili umkamate? ShwainiiiiiπŸ™„
Maana ya maandiko kusema;
• MWANAMKE MPUMBAVU HUIBOMOA NYUMBA YAKE MWENYEWE ni wazi Mwanamke usiipe kipaumbele NGONO bali jitunze kumkabili Mwanaume mmoja umpendaye wekeza UTII na kumpa heshima kama MUME wallah hutakuwa na mshindani MOYONI mwa MumeoπŸ’―
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria πŸ”¨


Dada zangu, najua mna hamu sana ya ndoa, najua ukipata mtu ambaye anaongea ndoa! Ndoa! Ndoa! Unachanganyikiwa na kuona mwanaume ndiyo hiyo! Lakini.....
07 April

Dada zangu, najua mna hamu sana ya ndoa, najua ukipata mtu ambaye anaongea ndoa! Ndoa! Ndoa! Unachanganyikiwa na kuona mwanaume ndiyo hiyo! Lakini.....

Dada zangu, najua mna hamu sana ya ndoa, najua ukipata mtu ambaye anaongea ndoa! Ndoa! Ndoa! Unachanganyikiwa na kuona mwanaume ndiyo hiyo! Lakini ogopa sana mwanaume ambaye ana haraka sana ya ndoa! Wala sizungumzii ukatili. Lakini kama ukikutana na mwanaume, mmekaa kwenye mahusiano, iwe ni muda mrefu au muda mfupi? Anakazania sana kuhusu ndoa, lakini hamjawahi kukutana kimwili, sio kwamba wewe mwanamke hutaki bali yeye ndiyo hataki, anatoa visababu sababu vingiiii!
Wengi wanajifanya ni watu wa dini sana, anakuambia kuhusu dini lakini si mtu wa kanisani wala msikitini, au dhambi nyingine anafanya sana tyu ila hiyo anaikwepa. Mwingine umemuambia tu sitaki kufanya mapenzi kiutani utani lakini hasisitizi, najua unafurahia kwakua anakuambia kuwa siaki nikuchezee, lakini hali imebadilika, kunaweza kuwa na sababu nyingine zaidi ya hiyo, hembu chunguza kama yaliyomo yamo.
Silazima kukutana naye kimwili lakini ukiwa makini kidogo tu utajua, msisimko wake wakati mko pamoja utajua. Ana kasi sana ya ndoa, anataka kila mtu kujua kama nayeye ana mpenzi, wewe unaona kama ni mapenzi, hapana, chunguza ziadi, wewe ni mtu mzima, unajua namaanisha nini, kuwa makini katika kuchunguza kwako. Nguvu za kiume zimekua ni tatizo kubwa sana na wanaume wengi siku hizi wanaoa si kwakua wanaweza ndoa bali wanataka watu kujua kuwa hawana matatizo, presha za familia zinakua kubwa sana.

NA IDD MAKENGO


HAKUFIKISHI KILELENI LAKINI ANAKUA MALAYA WANAWAKE WENGI
07 April

HAKUFIKISHI KILELENI LAKINI ANAKUA MALAYA WANAWAKE WENGI


Wanaume wengi ni Malaya lakini kama mwanaume wako hakufikishi, wewe mwenyewe mapenzi ni mara moja kwa mwezi, hata ukipita uchi mbele yake hata hashituki hawezi kukuvamia na kukupa cha mchana lakini unaona ana wanawake wengi, si wanawake wengi tu lakini ni kama anafanya juhudu kuhakikisha kuwa unajua kuwa ana wanawake wengi, yaani anapiga nao picha za uchi, anachat nao mbele yako, anaweza kuongea na mwanamke upo tu ili tu uongee.
Anawasifia wanawake wengine na hata majirani, anaweza kumtumia pesa mwanamke mwingine wakati wewe kakunyima na akituma anahakikisha kuwa unajua. Hapo dada yangu jua kuwa huyo mwanaume ana matatizo, anafanya hivyo kwakua anajua kuwa hakuridhishi hivyo kama ukimuona na wanawake wengi wewe utawaza. “Inawezekana huko kwingine anawafikisha laba mimi ndiyo mwenye matatizo!” wanaume wengi wenye matatizo ya nguvu za kiume na hata wenye vibamia wanakua hawajiamini.
Kwakua hawajiamini wanahisi kila mtu anayewaona, marafiki zao, wazazi na kila mtu anawaona kuwa wana matatizo ya nguvu za kiume au vibamia. Kwa maana hiyo basi suluhu kwao ni kuonyesha watu kuwa wao ni Malaya, marafiki zao wawaone kama Malaya wawaone kama ni watu wa wanawake wengi ili hata kama ukilalamika, ukimtangaza watu waseme “Mbona ana wanawake wengi kiasi hiki huyu hana tatizo!”
Hata wewe atakutia shaka utawaza hawa wanawake wasingeweza kumng’ng’ania wanakupigia simu wanakutukana kama aisingekua anawakuna vizuri mimi ndiyo mwenye tatizo. Lakini ukweli nikuwa huna tatizo mwanaume wa namna hiyo atakua anahonga sana na unajua wanawake na pesa watafanya chochote. Wanakutukana na kukupigia simu huku wakimng’ng’ania kwakua wanajua anawahudumia. Lakini wengine ni ule ulimbukeni tu, kama ambavyo wewe ulimkubali mwanzo ukidhani atabadilika.
Kama ambavyo inawezekana wewe ulidhani mkioana nguvu zitarudi nao wanadhani kua wanaweza kukupindua na wakaolewa kisha nguvu za huyo mwanaume zikarudi wakafurahia wao. Wengine wanahangaika tu wakiamini kuwa mwanaume ni mwanaume na hata kama hana nguvu basi wanaweza kuvumiliana na wakawa na furaha kitu ambacho si kweli. Kwa maana hiyo kama wewe hakuridhishi na kila siku nikubadilisha wanawake wala huna haja ya kuwa na presha kwani hakuna anachofanya huko nnje cha zaida ya kile anachokufanyia wewe.
NB; Kama una mwanaume wa namna hii, kama unataka kujua namna ya kuishi na mwanaume wa namna hii au kumsadia tatizo lake basi hakikisha unasoma Kitabu cha “MWANAUME; Namna ya kukabiliana na tatizo la nguvu za kiume na maumbile madogo” ni Kitabu cha watu wazima tu na bei yake ni Shilingi elfu kumi tu (10,000/-) Kukipata unalipia kwa M-Pesa no. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 baada ya hapo Kitabu unatumiwa kwa njia ya Whatsapp, Email au Facebook.


Monday, 6 April 2020

Je..!! Wajua Namna 9 za Kumpenda Mpenzi wako kwa Vitendo..!! Soma hapa kwa Kujua vitu hivyo..
06 April

Je..!! Wajua Namna 9 za Kumpenda Mpenzi wako kwa Vitendo..!! Soma hapa kwa Kujua vitu hivyo..

Kwel ukiambiwa utaje makabila matatu... - Warembo WA Kilimanjaro ...

Kama ilivyo mambo mengine kuwa “affection” ni swala la kujifunza, baadhi ya wanaume waliokuzwa/kulia kwenye jamii yenye mfumo Dume (Waafrika kwa ujumla) huwa hawajui kuonyesha hilo hitaji, ebu tuliite “kupenda kwa vitendo” hivyo huenda sio kwamba hataki bali hajui.
Kwa maana hiyo sio mbaya ikiwa wewe mwanadada ukamfundisha nini cha kufanya, ikiwa na wewe ulikuwa hujui basi jifunzeni wote ili kuwa na uhusiano bora wenye furaha.
Nitaorodhesha mambo machache ambayo wanawake wengi huwa wanapenda kufanyiwa ili wajue kweli wanapendwa kihisia na kivitendo.
1-Hakuna kitu wanawake wanazimia kama kukumbatiwa na kupigwa busu mara kwa mara.
2-Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha umekumbatia na kubusu hata kama kalala(hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio).
3-Mwambie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati/mayai/viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi.
4-Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda kwenye kituo cha daladala unafanya hivyo kabla hujakanyaga vumbi la nje.
5-Onyesha unajali kwa kumjulia hali kwa sms au sauti mara baada ya kufika kwenye mihangaiko yako na vilevile kumbuka kufanya hivyo kabla hujaondoka eneo la shughuli zako pia hakikisha unamueleza utakuwa saa ngapi nyumbani au kama kuna mahali unapitia basi mfahamishe utakuwa huko kwa muda gani n.k.
6-Ufikapo nyumbani kumbatia na busu mdomoni sio shavuni, badala ya kukimbilia kusema yaliyojili huko utokako.
7- Mnunulie vijizawadi mara kwa mara, wazaramo hununuliwa Khanga au hereni na mikifu ya dhahabu, Wazungu hununuliwa maua, kadi au vidani vya madini tofauti, kuna wengine ukipeleka kitoweo (aina ya nyama) basi umemaliza kezi mwana mama anafurahi kweli-kweli sasa wewe fanya kile unachomudu sio kila siku wala kila mwezi..
8-Msaidie kusafisha meza/jamvi mara baada ya mlo wa jioni, ikiwa umechoka hata yeye kachoka pia hivyo mkikutana nyumbani mna-share kufanya usafi ili kuokoa muda.

9-Lolote litakalo tokea kila la kheri, lakini hakikisha unabusu na kukumbatia kabla hujaanza kukoroma.

Usisahau kushare post hii.πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome


06 April

MWANAUME, HIVI UNAJUA KWANINI NI MUHIMU KUMFIKISHA KILELENI MWANAMKE WAKO, MANAPOKUWA MNAPEANA UTAMU

Related image

KUNA kitu kimoja tu ambacho Susan* anatamani maishani mwake. Sio pesa, sio gari wala si vipondozi, bali ni kupata burudani tosha la mapenzi.
Anasema maishani mwake, hajawahi kufikia kilele cha tendo ndoa hata mara moja.
“Sijawahi kufikia kilele cha tendo la ndoa. Kwangu shughuli ni shughuli tu. Ninavumilia tu kwa sababu nampenda mpenzi wangu kwa dhati,” asema Bi Susan na kuongeza kuwa wakati mwingine anachukia tendo hili ili asiache kwenye njia panda.
Ili kuhakikisha kwamba kamwe havujiki moyo wakati wa shughuli, wataalamu wanasema Susan anaweza kutumia mbinu za kisasa za kufanya mapenzi.
Wanasema imegunduliwa kwamba kwa kubadilisha staili za kula uroda wachumba wanaweza kuridhishana kikamilifu na kufikia kilele cha shughuli hii muhimu.
“Kwa kutumia staili tofauti za kulishana uroda wachumba huridhishana kikamilifu,” asema mwanasaikolojia Kathy David.
Wataalamu wengi wa mapenzi wanakubaliana kwamba wachumba wanapotumia mbinu tofauti za kuburudishana kitandani, wanaridhishana na wanawake wanafikia kilele cha tendo la ndoa.
Kulingana na mwanasaikolojia Bi David aliye pia mwandishi wa vitabu vya mapenzi wachumba wanaotumia ubunifu wakati wa burudani kitandani wanaridhishana vilivyo.
Bi David asema sio siri kwamba wanaume wengi wamekuwa wakiwapoteza wachumba wao kwa kukosa kuwaridhisha kitandani.
“ Ni kweli watu wengi na hasa wanaume  wamekuwa wakiwapoteza wachumba wao wa kukosa kuwapagawisha wakati wa tendo la ndoa.
Hata hivyo wanaotumia ubunifu na kutumia staili tofauti huwa hawana tatizo lolote,” asema na kuongeza kuwa  utaalamu wa kurushana roho  ndio msingi wa ndoa na uchumba wowote ule.
Bi David asema wachumba wanapasa kuwa wakibadilisha mbinu ili kufanya penzi kunoga na kupatiana  shibe la burudani.
Anasema ubunifu na staili  tofauti za kurushana roho huongeza ladha tendo la ndoa.
“Unaweza kutia nakshi burudani faraghani kwa kutumia mitindo mbalimbali ya kula uroda inayoendelea kuvumbuliwa  kila siku,”asema na kuongeza kuwa kizazi  cha wakati huu hakiridhishwi  na mitindo ya zamani wanayosema imepitwa na wakati.
“Hizi sio nyakati ambazo mwanamke alikuwa akilala chali na kusubiri mwanaume apande juu  yake. Kila mmoja ana wajibu wa kuchangia kufanikisha  tendo la ndoa,” asema.
Kulingana na Bi David mwanamke anaweza kumfanya mwanaume alipuke kwa raha kwa kuwa juu yake na kumwongoza  akiwa nahodha  wa mechi kitandani.
“Mwanamke anaweza kuchukua usukani  na kuwa nahodha wa mechi na kumfanya mchumba wake kuridima kwa raha  ya ajabu. Na kwa sababu nahodha uelewa na kufahamu mechi vilivyo, ushindi lazima upatikane,” asema.
Anaeleza kwamba wanawake  wanaojua kuwaelekeza  mwanamume  wanapocheza rumba kitandani  huwapagawisha  kimapenzi.
“Muulize mchumba wako kinachomtia kichaa mnapolishana  asali. Mwelekeze ipasavyo huku ukiwasiliana na hisia zako mnapoelea katika bahari ya mahaba ,” asema.
Wataalamu wa mahaba wanasema watu wengi hukosa kuwafikisha  wachumba wao katika kilele cha mapenzi kwa kutojiwachilia wakati wa tendo la ndoa tatizo  ambalo baadhi ya mitindo ya kisasa inalenga kutatua.
Kulingana na Bi Libby Keatinge mwanasailokojia  mwenye uzoefu mkubwa wa maswala ya mapenzi, ni muhimu kujiwachilia ili kupata matokeo bora ya raha wakati wa kulishana tunda.
Anasema ulaji uroda hufanikiwa ipasavyo ikiwa kuna  mawasiliano ya mwili na akili. Bi keatinge asema baadhi ya staili za kisasa za kufanya mapenzi zimenuiwa kuimarisha hali hiyo.
“Unaweza kubadilisha maisha yako ya mapenzi kwa  kuchagua baadhi ya mbinu ambazo wataalamu wamevumbua ili kupamba burudani na mchumba wako.”asema.
Kwenye kitabu Discovering Erotic Sex,  Bi Keatinge anaorodhesha  baadhi ya mitindo iliyothibitishwa kukata kiu cha penzi cha wanaoitumia.
Anasema mitindo hiyo humpatia mwanamke  fursa ya kutawala wakati wa kucheza goma kitandani na mpenzi wake.  Hata hivyo mtaalamu huyu asema sio staili zote za kisasa  zinawafanya  vidosho  kuwa rubani wa ndege ya mapenzi.
“Staili za kisasa  zimebuniwa ili kuleta usawa na kuhakikisha kila mmoja ametawala uwanja kwa awamu tofauti. Itatengemea aina ya mtindo na eneo la kusakatia goma,” asema.
Kusimama
Wataalamu wanakubaliana kwamba mawasiliano ya kihisi, kimwili na kiakili ndio msingi wa kufanikisha  tendo la ndoa.
“Mnaweza kufanya mapenzi mkisimama, mkiinama mkichuchumaa, kwenye bafu,sakafuni kwenye zulia, mezani  kwenye kochi na hata ndani  ya gari. Hizi zote ni staili na maeneo ya kufanyia mapenzi. Hata hivyo cha muhimu ni mawasiliano kati ya mwili, akili na hisia zako  zitakazokupeleka katika kilele cha tendo lenyewe,” asema.
Bi David asema mazingira ya kusakatia mechi pia huchangia  kufanikiwa kwa staili yoyote ya kufanya mapenzi. “ Ikiwa unatumia mbinu yoyote ya  kufanya mapenzi katika mazingira yasiyofaa  ni vigumu kufikia kilele cha mlima wa ashiki,” asema katika makala yake kwa jina 5 things men think about sex.
Kulingana na  Bi Keatinge wachumba wanaweza kufufua maisha yao ya gono  na kujenga upya tajiriba ya  kutifua vumbi kitandani kwa kutafuta na kutumia staili zinazowafaa.
Hata hivyo anasema ni hatari kumlazimisha mchumba wako kutumia staili isiyompendeza akisema ni kama kusukuma gari ya moshi mlimani.
Bi Keatinge asema kumshinikiza mrembo kutumia staili asiyoitamani ni kumwongezea mateso na anaweza kukuchukia maisha yake yote.
“Wachumba wanafaa kukubaliana  staili zinazowafaa kuburudishana. Ni makosa kumlazimisha kiosha roho wako kutumia staili asiyoitamani kwa sababu itamwongezea mateso,” asema jambo ambalo watu wengi wanakubaliana nalo.
Anasema wachumba hawafai kukubali chochote kiwe kikwazo katika juhudi za kusaka shibe la uroda. “ Kila mmoja anapasa kumhusisha  mchumba wake katika kila hatua hadi amfikishe katika kilele cha mlima wa mahaba,” asema.


πŸ‘‰ Mambo 6 ambayo ni siri ya mwanamke na sio rahisi kukwambiaπŸ‘‡βœ”
06 April

πŸ‘‰ Mambo 6 ambayo ni siri ya mwanamke na sio rahisi kukwambiaπŸ‘‡✔

πŸ‘‰ Mambo 6 ambayo ni siri ya mwanamke na sio rahisi kukwambia ...


1. Idadi ya wapenzi wake wa zamani

Wanaume wengi hupenda kujua wao ni wangapi kuwa na mwanamke Fulani. Lakini mwanamke kamwe hawezi akakwambia wewe ni wa ngapi. Kumuuliza jambo hili kunamkera sana mwanamke na ndio maana mara nyingi hawezi akakwambia ukweli.

2. Anakulinganisha na mpenzi wa zamani

Mwanamke mara nyingi anakulinganisha na mpenzi wake wa zamani japokuwa hawezi kukwambia waziwazi. Wakati mwingine tabia hii huwafanya wanawake kuwatamani wapenzi wa zamani na hata kurudiana nao endapo watakosa mtu aliye bora kuliko mpenzi wake wa zamani.

3. Kasoro zako

Mwanamke kamwe hawezi kukwambia kasoro zako. Wanawake wanajua kumfichiaa mpenzi wao mambo wasiyotaka yajulikane kwa wengine na kwa mpenzi wake. Wanajua njia za kiujanja za kutumia ili kufichua siri zako zote. Mwanamke hawezi kukwambia kasoro zako kwa kuogopa kukuumiza.

4. Mapungufu yake

Mwanamke hawezi kukwambia mapungufu yake labda kwa kuhofia kusheshwa thamani. Wanawake ni wasiri sana kwa mapungufu yao. Wanajua vyema hofu zinazomuandamana, vitu vinavyowakosesha usingizi na mambo yanayowalemea maishani japo sio rahisi kuonyesha. Kwa nje anaweza akaonekana yuko vizuri na hana tatizo kumbe ndani ana matatizo au mapungufu. Anaweza kufanya yote kufunika upungufu wake!
5. Huwa unampagawisha mpaka anakosa la kusema
Hili halisemi kabisa mwanawake kwa sababu anaona haya kutumia maneno ya wazi kueleza raha unayompa. Maneno ya kuzuzua ni himaya ya wanaume, lakini wakati mwingine wapo wasioweza kuficha.

6. Haumridhishi katika tendo la ndoa


Wanawake wengi hawapendi kusema kama hawaridhiki Kwenye tendo la ndoa. Wanawake wanahitaji kuandaliwa vilivyo kwa dakika 10, 20 ama nusu saa. Mara nyingine wanaume huwahi kabla mwanamke hajawa tayari na hivyo kushindwa kuridhika lakini hawezi kusema.
Usisahau kushare post hii.πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome


06 April

Jinsi ya Kutambua Kama ni Mtoto wa Kike/kiume Wakati wa Ujauzito ?

Tumbo
Wazoefu wanaamini kuwa endapo utakuwa umebeba uzito mdogo tumboni na tumbo dogo mtoto atakuwa ni wa kiume.

Chunusi 
Uwepo wa chunusi nyingi na mara kwa mara ni ishara kuwa umebeba mtoto wa kiume wakati ngozi kuwa laini sana kupita awali ikimaanisha ni mimba ya mtoto wa kike.

Haja ndogo 
Endapo mama mjamzito anatoa haja ndogo rangi nyeusi kuna uwezekano mkubwa amebeba mtoto wa kiume huku nyeupe au rangi ya mawimbi ikimaanisha jinsia ya kike.

Miguu

Kuwaka moto na kuwa laini ina maanisha mimba ya mtoto wa kike wakati miguu kuwa na mikono ya baridi ni mtoo wa kiume.

Mapigo ya moyo 
Hii hutumiwa na wataalamu wa afya ambapo mapigo chini ya 140 ni mtoto wa kiume na ikiwa ni zaidi ya 140 ni mtoto wa kike.

Nywele
Mwanamke anapokuwa mjamzito na nywele zikaota au kukua kwa kasi inamaanisha mtoto aliyenae tumboni ni wa kiume wakati kinyume chake ni jinsia ya kike.


06 April

Nini Sababu za Kuchepuka ? Je Kuchepuka ni Asili au Tabia ?

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana na malalamiko ya kila kukicha ya wanandoa wengi kutokuwa waaminifu. Wapo waliokabiliana na misuguano, mapigano na magomvi mengi kwasababu ya jambo hili na wapo ambao tayari wameshaamua kutengana. 

Watoto wa familia nyingi sana wamebaki kuwa wahanga wa tatizo hili na bado hakuna dalili za tatizo hili kupungua. Kila mmoja akiulizwa anatoa sababu yake binafsi ya kwanini ametoka au alitoka nje ya ndoa yake, sababu hizi zinamfanano na baadhi zinatofautiana pia. Katika makala hii nimejaribu kuangalia baadhi ya sababu ambazo mara kwa mara zimeripotiwa na wanandoa wengi wanaokuja kwenye ushauri kwenye ofisi zetu. 

Hii inafanya sababu hizi kuwa halisi na zitakazokupa msaada ukizielewa maana haziko kinadharia tu bali zimetokea katika maisha halisi ya ndoa za watu kama wewe. Pamoja na yote haya ukweli unabaki kwamba matendo ya kukosa uaminifu kwenye ndoa au mahusiano yana athari mbaya sana na athari hizi zinaweza kuambatana na maumivu makali na wahusika kuwa maadui badala ya wapenzi kama walivyokuwa awali.

Sababu ya 1: Kutoridhishwa katika tendo la ndoa


Kumekuwepo na malalamiko mengi na yatofauti baina ya wanandoa wanaume na wanawake katika suala hili. Wanaume wanalalamika kwamba wake zao mara baada ya kuolewa na hususani wakishapata watoto wanaanza kuwa wazembe na wasiojituma kwenye tendo la ndoa kama walivyokuwa awali. Tafiti zinaonyesha kwamba mara mwanaume anapohisi kutoridhishwa kwenye tendo la ndoa ananafasi kubwa zaidi ya kutoka nje mapema kuliko mke wake. Wanawake wanauvumulivu wa ziada na kwa wale waliotoka nje ya ndoa zao walifanya hivyo baada ya uvumilivu wa miaka mingi na kukosa tumaini. Kutoridhishwa katika tendo la ndoa kunaweza pia kusababishwa na maumbile ya mwili, kwa mfano watu wenye miili mikubwa na uzito mkubwa hupata shida kwenye kuwaridhisha wenzao ukizingatia kwamba tendo la ndoa ni zoezi la kimwili “physical exercise”. Mtu wa jinsi hii anaweza kushindwa kwasababu ya ukubwa wamwili, kushindwa kuutuma mwili wake kadri anavyotaka na pia wengine kuishiwa pumzi au kuchoka mapema na hivyo kufika kileleni mapema sana. Hali hii husababisha kutoridhika kwa wanawake wengi sana kwenye ndoa.

Sababu nyinginezo zilizotajwa za wanandoa kutoridhishana kwenye tendo la ndoa ni kama vile, uchafu, harufu zisizo nzuri, uelewa mdogo wa namna ya ufanywaji wa tendo hilo, makuzi na mapokeo, mambo yanayohusiana na mila, utamaduni au imani pamoja na magonjwa.

Sababu ya 2: Kutokupata tendo la ndoa kwa muda mrefu

Waathirika wa sababu hii ni wanaume kuliko wanawake. Tunaposema muda mrefu, hili ni suala la tofauti kwa mwanaume na mwanamke. Kwa mwanaume wiki moja yaweza kuhesabika ni muda mrefu kulingana na mazoea yaliyokuwepo kwenye ndoa hiyo. Kisayansi na kibaiolojia, mwanamke anauwezo wa kustahimili au kuvumilia kukaa bila kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu kuliko mwanaume. Baadhi ya tafiti pia zimeonyesha kuwa watoto wengi wa nje ya ndoa wanazaliwa katika vipindi ambavyo tendo la ndoa lina shida, hii inamaanisha nyakati za ugonjwa, ujauzito, magonvi makubwa au vipindi vingine vilivyofanya mwanaume asipate tendo la ndoa ndipo ambapo aliamua kuenda pembeni na huko kukatokea mimba na baadaye mtoto. Utaelewa ukubwa au kiasi cha tatizo kwa kuangalia ukweli kwamba kwenye ndoa nyingi, wanaume ndio wanaoongoza kwa kuwa na watoto nje ya ndoa na sio wanawake. Katika jambo hili la kutokupeana tendo la ndoa kwa muda mrefu, tumekuwa tukishauri kwamba kila mwanandoa ahakikishe anaweza kuzuia migogoro isiathiri tendo ndoa ili wasikae muda bila kulifanya, na kama kuna safari au utengano wa lazima baina yao basi kuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara na ikibidi wanandoa watembeleane au kuwa pamoja zaidi ya kutokuwa pamoja. Umbali una athari kubwa sana kwenye ndoa nyingi. Kwa mara nyingine niseme hili, kunyimana tendo la ndoa kama adhabu au kwa matakwa yeyote binafsi hakujengi bali kunabomoa, kwasababu wengi wamejikuta wakitoka nje ya ndoa zao kwasababu hii.

Sababu ya 3: Hofu zinazohusiana na tendo la ndoa

Kati ya vitu vinavyowasumbua wanandoa wengi hususani wanaume kwenye kushindwa kushiriki tendo la ndoa au kulikinai kabisa ni suala zima la kuwa na hofu au woga wowote ule. Hofu na woga katika eneo hili huweza kuletwa na vyanzo tofauti kama vile masengenyo na kejeli pale mtu anavyojaribu kuomba kupata tendo la ndoa au hata baada ya kushiriki tendo hilo. Maranyingine maneno haya yanaweza kurushwa kama utani lakini yanapoingia kwenye moyo wa mwanandoa mhusika yanajenga hofu kubwa akidhani kwamba unamaanisha. Hofu nyingine yaweza kutokea kwenye dhihaka zinazofanywa pale mmoja anapoonyesha kutokufurahishwa au kutoshelezwa na mwenzake. Hapa kunatofauti ya kijinsia, mwanamke anahitaji busara ya hali ya juu kwenye kuongea na mume wake kumwambia kama hajaridhika, pale mwanamke anapoamua kutumia dhihaka, matusi au maneno makali, humwondoa kabisa mwanaume kwenye uwezo wake wa tendo wakati mwanaume huyuhuyu akienda kujaribu pembeni anajikuta bado yuko vizuri wakati kwa mkewe alishindwa, hilo linapotokea inakuwa ngumu sana mwanaume huyu kurudi au kupenda tena kufanya tendo la ndoa na mkewe. Fahamu kwamba hofu ya aina yoyote ni kikwazo na sumu kubwa ya tendo la ndoa, na athari zake ni kubwa zaidi kwa mwanaume kuliko mwanamke.

Sababu ya 4: Penzi kupoa au kufa

Penzi linapopoa au hata linapokufa huwa hali huwa inaonyesha wazi kabisa. Kwenye kupoa mhusika anaweza kuanza kujihisi ndani ya moyo wake kutompenda mwenzake kama alivyokuwa akimpenda awali. Inawezekana mwenzake hajagundua kuanzia mwanzoni kwamba penzi la mpenzi wake limepoa ila kama hali ya kupoa huku itaendelea lazima itagundulika. Baadhi ya vitu dhahiri vitakavyoweza kukufanya ufahamu kwamba penzi la mwenzako limepoa au kufa nikwamba kuna mambo ambayo uliyazoea kuyaona yakifanywa kawaida hautayaona tena. Kuna vitu vilikuwa vikifanywa pasipo kukumbushana sasa utalazimika kuviomba ili ufanyiwe, utaona kila kitu kinakuwa kigumu kumhusu mwenzako na hata uongeaji au kujibu kwake kunakuwa na walakini. Kwenye tendo la ndoa nako maranyingi ndiko kwenye kuonyesha taa nyekundu mapema, ule ushiriki, furaha na bashasha zilizokuwapo awali mkiwa kwenye tendo hauzioni tena, tendo la ndoa linafanywa kama jukumu la kawaida na maranyingine hata hamu ya kushiriki haipo. Hapa ndipo mmoja hukinai hiyo hali ya kulazimishana tendo la ndoa, au kupeana kwa masharti au kunyimwa au hata mmoja kupoteza hamasa ya kulifanya tendo hilo na mtu asiyekuwa na hisia naye. Huo unakuwa mwanzo wa mmoja au wote kutoka nje ya mahusiano au ndoa. Penzi ni kama moto, ukiwashwa pasipo kuchochewa hupoa au hata kuzima kabisa. Wengi wanapoingia kwenye ndoa wanadhani mkishaoana basi mambo yanajiseti yenyewe tu, mapenzi yanajichanulia yenyewe tu, la hasha! Lazima kuwepo na jitihada za dhati za wanandoa kuhakikisha wanachochea penzi lao, kulilinda na kulipalilia ili liendelee kumea, kunawiri na kuzaaa matunda.


Sababu ya 5: Ushawishi wa marafiki

Wako watu wengi sana kwenye ushauri wa wanandoa na hata wale wasiowanandoa ambao wamekiri kuchepuka kwasababu ya kushawishiwa na marafiki. Ni lazima ukafahamu nguvu waliyonayo marafiki. Usipokuwa na hekima ya juu ya kuweza kuchagua nani wa kuwanaye rafiki na nani sio basi utajikuta unapelekeshwa kila upande hata kule usipopenda utapelekwa kwasababu tu nguvu ya maamuzi haiko kwako tena bali iko kwa marafiki zako. Yamkini unasema mimi ni rafiki tu sifanyi vile wanavyovifanya wao, mimi nasikiliza na kuchangia tu hoja zao, lakini ngoja nikwambie, taratibu utasikiliza, taratibu utaanza kuchangia na taratibu utavutika kuyafanya yale wanayoyafanya. Yamkini wao kuchepuka ni hadithi ya kwaida na kwako sio kawaida, ukiendelea kukaa nao kidogokidogo utaanza kuona kuchepuka sio kitu cha kushangaza sana maana wengine nao wanafanya, na utaanza kidogokidogo na mwisho utakuwa mtaalamu. Wako waliofundishwa kiutaniutani leo hii ni wataalamu kuliko walimu wao. Jifunze kuwa na msimamo. Jifunze kuchagua marafiki wanaokujenga na sio kukubomoa. Jifunze kufanya maamuzi binafsi yenye busara na yasiyokufungulia milango ya majuto. Kumbuka ukijakujuta hautokula majuto hayo na hao marafiki zako. Utayala mwenyewe na wanaokuhusu. Ni hasara na anguko kwao na familia yako na ndugu zako.


Sababu ya 6: Ushawishi wa kilevi (pombe au madawa)


Wako watu wanaojiamini sana na wanajihisi wenye uwezo wa kujizuia, lakini mara wanapokuwa katika ulevi wowote ule hushindwa kujizuia. Hili liko kwa wanawake na hata wanaume. Tabia ya ulevi wowote hupunguza uwezo wa mtu wa kufikiria ilivyo sahihi “rational thinking”. Unaweza kukuta watu wameketi pamoja na wanaheshimiana lakini kwa kadri wanavyoendelea kulewa wanaanza kushikana maungo na kila mmoja anaona nisawa tu, heshima na nidhamu waliyokuwa nayo awali imeshapeperukia dirishani kwasababu ya ushawishi wa ulevi “the influence of alcohol”. Hali hii ina majuto sana maana mtu anajikuta kasha shiriki ngono na mtu mwingine, ama mtu anayemjua au hata asiyemjua pasipo utashi wake. Majuto yanakuwa makubwa zaidi maana mara nyingine hata usiri unakuwa haupo, heshima na nidhamu yako yote inaathirika. Ziko baadhi ya pombe ambazo badala tu ya kukuondolea aibu, zinaweza kukulegeza mwili na viungo na kuongeza hamu ya ngono. Ndio maana watu wanaotumia vilevi wanashauriwa kuwa na wenza wao katika nyakati hizi ili walao kujizuia kuingia mitegoni. Watu wengi tuliowahoji nyakati za ushauri wanakiri kwamba safari ya kuingia kwenye mahusiano ya kingono na watu wanje ilisindikizwa zaidi na matumizi ya kilevi au vilevi, na wengine wanaendelea kukiri kwamba ni ngumu kuchepuka bila kuwa na kilevi akilini.

Sababu ya 7: Kutostahimili ukaribu usio na mipaka

Wapo watu wengi ambao wamejikuta wakikamatika katika mahusiano ya kingono na wale waliowaita marafiki wakaribu. Mwanzoni alionekana kama rafiki, mnashauriana, mnasaidiana, mnasindikizana, mnatembeleana, na wala haukuwahi kudhani mngefikia hapo mlipofikia. 
Lakini kwasababu mlishindwa kuwamakini kwenye kuilinda mipaka ya urafiki wenu, sasa uhusiano wa kawaida na waurafiki umekuwa uhusiano wakingono. Hali hii huathiri uthamani wa urafiki baina ya watu na maranyingine waliokuwa marafiki wanaweza kujakuwa maadui kabisa. Ukaribu zaidi na mtu wa jinsia ya tofauti na wewe huwa sio mzuri sana kwa afya ya mahusiano au ndoa yenu. Yamkini unajitetea kwamba hakuna kinachoweza kutokea lakini fahamu kwamba hata kikija kutokea hautakuwa na ujasiri wa kusema kwamba kuna kilichotokea. 
Heri kuziba ufa kuliko kujenga ukuta. Ninakushauri kwamba watu wote ambao uko nao karibu nivema wafahamike kwa mwenza wako, epuka urafiki wa sirini, na mikutano ya sirini. Mkutano na rafiki ambaye ukonaye karibu na wajinsia tofauti kamwe usifanyike maeneo yakificho au sehemu ambayo mkopekeyenu. Yamkini nia na dhumuni lenu sio ovu lakini mazingira shawishi yanaweza kuwafikisha ambako hamkupanga kufika. Kuwa na ujasiri wakuiweka mipaka ya urafiki wenu bayana, na rafiki yako au rafiki zako waiheshimu mipaka yako. Iheshimu mipaka hiyo maana usipoiheshimu mipaka yako na wengine kamwe hawawezi kuiheshimu mipaka hiyo. Pia ukitaka watu waheshimu mipaka yako na wewe pia iheshimu mipaka ya wengine. Na mwisho ni kwamba kamwe usimwamini yeyote kwa asilimia 100, Jilinde uwapo mazingira yeyote.


Sababu ya 8: Kulipiza kisasi (revenge)

Aina hii ya kuchepuka huwa kwa wanaume na wanawake ingawa inaripotiwa zaidi kuonekana kwa wanaume kwasababu ya ukweli kwamba maranyingi wanaume wanaweza wakakwazika na bado wasifunguke kuelezea walivyokwazwa lakini wakati huohuo wanakiu ya kulipiza kisasi kwa maumivu waliyoyapata tofauti na wanawake ambao wao kufunguka ni rahisi na ni kawaida kwao. Wanaume kwa kawaida wanaweza kuamua kutoka nje ya ndoa kwasababu tu amekasirishwa na kuona haheshimiwi katika mambo flani kwenye mahusiano au familia. Kwamfano akihisi hasikilizwi, hapewi kipaumbele, hahudumiwi, anachosema hakifwatwi anavyotamani havifanywi basi kuna uwezekano mkubwa akaanzisha mahusiano pembeni kwa siri.

Tafiti za kisaikolojia zinasema kwamba mwanaume anapochepuka kwa msukumo wa hali kama hizi ile hali ya kujihisi anafanya kosa “guilty conscious” inapungua au kupotea kabisa na kwahivyo anaweza kujihesabia haki kabisa kwa kile anachokifanya. Hii inaweza kumfanya aendelee kuchepuka kwa muda mrefu zaidi tofauti na mwanamke ambaye hata hali hii ikijitokeza wengi huwa wanajihisi kuhukumiwa na kujisikia vibaya moyoni. Kuchepuka kwa kulipiza kisasi hutokea pia nyakati ambazo mwanandoa mmoja anahisi kuwa mwenzake ana mahusiano nje, iwe kuna ushahidi au nitetesi, wengine jambo hili humsukuma na yeye kufanya hivyohivyo ili kutafuta uwiano au kujisuuza nafsi. Kwa bahati mbaya matokeo ya tabia hizi yamekuwa hasi zaidi na kwa wengi imepelekea kuharibu mahusiano na ndoa. Ninashauri kwamba yanapotokea maumivu au makwazo ya aina yeyote yasihifadhiwe moyoni au kuonewa aibu kuzungumzwa maana visasi havilipi balihuongeza maumivu na uharibifu zaidi.

Sababu ya 9: Tabia ya asili, mfano, laana au urithi

Pamoja na kwamba mahusiano nje ya ndoa au kwa jina maarufu sikuhizi “kuchepuka” ni tabia na mazoea ya mhusika lakini tusisahau kwamba ziko kesi ambazo ni zaidi ya tabia. Ziko nyakati ambazo tunashuhulikia kesi ya ushauri ambayounaona wazi tabia ya mtu flani sio ya kujitakia au matamanio ya kawaida lakini kuna udhihirisho wa nguvu inayomsukuma kufanya ngono. Mtu anawezakuwa hatamani kabisa au hapendi anachokifanya lakini atajikuta tayari ametumbukia kwenye ngono na baada ya kufanya tendo hilo anajuta sana lakini bado kesho au keshokutwa atarudi kule kule. Ziko koo au familia ambazo zina laana kwenye maeneo haya, unakuta idadi kubwa ya wanaume au wanawake kwenye familia au ukoo flani wana watoto nje ya ndoa, watoto waliopatikana kabla ya ndoa au watoto wanaopatikana nje ya ndoa lakini mtu akiwa ndani ya ndoa. Hapa namaanisha mtu ana mke lakini tunasikia watoto wanaletwa au wanasemekana wamezaliwa na baba huyu. Kesi nyingi, na vikao vingi vya usuluhishi vinaketi vikijaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo. Labda mke anaweza kukimbia kwa kuchoshwa na akaolewa mwingine lakini bado mume anaendelea kuleta watoto wanje tu.

Iko mifano ya familia ambazo baba aliwahi kufahamika kuwa na tabia hizi za kuchepuka, na kwa bahati mbaya watoto wake wakiume au hata wakike nao wakaandamwa na roho ile ile ya baba yao. Yawezekana isiwe baba ikawa ni mama aliwahi kuwa na tabia hizi, alivyokuwa binti kabla ya kuolewa au hata akiwa na mume wake lakini kile kitu watu walichowahi kukiona kwa mama au baba sasa wanakiona kwa watoto wao. Hili ni suala la kurithi, na pia laweza kuwa suala la roho inayotembea. Masuala ya namna hii ni magumu kidogo kuyaelewa maana yanaonekana kwa jinsi ya mwilini lakini nguvu yake sio ya jinsi ya mwilini, na kwahivyo uelewa wake unaweza kuchanganya kidogo lakini fahamu tu kwamba yako dhahiri zaidi ya uwazavyo. Kuyashuhulikia kimwili, au kuyashuhulikia kama vile chanzo ni tabia za kawaida ni ngumu sana kuleta suluhisho. Mambo ya kiroho hayanabudi kushuhulikiwa kiroho. Na endapo kwenye ushauri tunakutana na kesi za namna hii tunamshauri mhusika au wahusika kulishuhulikia jambo kiroho zaidi. Kwa bahati nzuri wahusika wanapoelewa na kuanza mchakato wa kiroho ufumbuzi huwa rahisi sana.

Mwisho niseme kwamba hali yeyote ya kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yako inanafasi kubwa sana kwenye kuleta uharibifu. Wako walioharibu ndoa zao na zikapasuka wakati bado walikuwa wanazipenda ziendelee kuwepo. Japokuwa kuchepuka hufanywa kwa siri kubwa lakini maranyingi siri hizi huwa ni za muda mfupi na kuna nyakati zinavuja au kuibuliwa na hapo ndipo machungu, majuto na machozi hutokea. Inawezekana kabisa majuto na machozi yakakupa nafasi ya kujirekebisha na kuiboresha ndoa yako iliyopata nyufa baada ya kuchepuka lakini pia inawezekana kabisa ukajuta, ukalia sana na bado usiiokoe ndoa yako maana yamkini mwenzako hatokuwa tayari kuendelea na wewe. Kama unaipenda ndoa yako basi utailinda, na mojawapo ya namna ya kuilinda ni kuwa mwaminifu.