EDUSPORTSTZ : MICHEZO

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Monday, 6 April 2020

06 April

MAMA YAKE GUARDIOLA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSUMBULIWA NA VIRUSI VYA CORONA

KLABU ya Manchester City imethibitisha kifo cha mama wa kocha wao mkuu, Mspaniola Pep Guardiola kwa ugonjwa wa COVID 19.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamethibitisha leo kwamba Dolors Sala Carrio amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 82 mjini Manresa, Barcelona.
Taarifa ya Man City imesema: "Familia ya Manchester City  inasikitika kutangaza kifo cha mama yake Pep, Dolors Sala Carrio kilichotokea leo huko Manresa, Barcelona baada ya kusumbuliwa na virusi vya corona. 

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola (kulia) akiwa na mama yake, Dolors Sala Carrio aliyefariki dunia leo kwa ugonjwa wa COVID 19 

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamethibitisha leo kwamba Dolors Sala Carrio amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 82 mjini Manresa, Barcelona.
Habari hizo za kusikitisha zinakuja wiki kadhaa tangu Guardiola achangie Pauni 920,000 kusaidia mapambano dhidi ya mlipuko wa virusi vya corona nchini Hispania katika mfuko wa Angel Soler Daniel Foundation.  
Mfuko huo umepewa jina la Daktari wa Santpedor ambaye alifariki duna miaka ya 1970 - mji ambao ametokea Guardiola.


06 April

WADAU WA KUNDI LA SPORTS VISION WAMPIGA JEKI JELLAH MTAGWA, BEKI WA ZAMANI WA TAIFA STARS ANAYEUMWA KWA MUDA MREFU

Wadau wa michezo wa kundi la Whatsapp la Sports Vision, Bakari Malima (kulia) na Mkala Fundikira (kushoto) wakimkabidhi msaada wa jumla ya Sh. 500,000 beki wa kimataifa wa zamani wa Tanzania, Jellah Mtagwa (katikati) anayesumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu walipomtembelea nyumbani kwake, Magomeni Kagera Jijini Dar es Salaam leo.

Wanachama wa kundi la Sports Vision walijichangisha fedha hizo kwa lengo la kumsaidia Jellah Mtagwa, ambaye kama Bakari Malima (kulia) wote ni mabeki wa kati wa zamani wa Taifa Stars, klabu za Yanga SC na Pan Africans kwa vipindi tofauti. Jellah alianzia Yanga miaka ya 1970 akamalizia Pan miaka ya 1980, wakati Malima aliibukia Pan miaka ya 1990 mwanzoni akamalizia Yanga mwishoni mwa miaka hiyo


Sunday, 5 April 2020

05 April

TYSON FURY ANATAKA KUPGANA NA JOSHUA KWANZA KULIKO KURUDIANA TENA NA WILDER

BONDIA Tyson Fury 'Gypsy King' anataka zaidi pambano la kuunganisha mataji ya dunia ya uzito wa juu dhidi ya Muingereza mwenzake, Anthony Joshua kuliko kupigana kwa mara ya tatu na Mmarekani Deontay Wilder. 
Fury anayeshikilia taji la WBC ambaye sasa amefikisha mapambano 30 ya kushinda akiwa hajapoteza hata moja zadi ya droo kwenye pambano la kwanza na Wilider, anataka kuwa bingwa asiyepingika wa uzio wa juu duniani.
Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa pamoja na timu yake wanajaribu kushawishi pambano dhidi ya Wilder liwekwe pembeni kwanza apiga e na Joshua, bingwa wa mataji ya WBA, WBO na IBF.

Tyson Fury anataka zaidi pambano la kuunganisha mataji dhidi ya Anthony Joshua kuliko kupigana tena na Deontay Wilder PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Waingereza hao wote tayari wana ratiba ya mapambano yajayo - Fury dhidi ya Wilder na Joshua dhidi ya Kubrat Pulev Uwanja wa Tottenham Hotspur.
Pambano kati ya Joshua na Pulev lilipangwa kufanyika Juni 20 Kaskazini mwa London na sasa limesogezwa mbele hadi Julai 25 kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona duniani kote.


05 April

KIKOSI TIGER YA MBEYA 1993 STEVEN MAPUNDA ‘GARRINCHA’ NDANI

KIKOSI cha Tiger ya Mbeya mwaka 1993 kikiwa Uwanja wa Karume Dar es Salaam kabla ya mechi Benki Kuu (BoT) ya Dar es Salaam Daraja la Pili (sasa) la Kwanza kutoka kulia 
Kipa Mzambia, Baldwin Sisinawa, Raymond Simkoko, Remy Mkama, Medard Barongo, Nebo Bukumbi, Thomas Kasulamemba, Steven Mapunda ‘Garrincha’, kocha Hassan Mlwilo (marehemu) na Nassib Tondogoso.
Waliochuchumaa; Eiphraim Mwakalasa ‘Kimti’, Yahya Mchatta, Bahati Mwamlima, Karabi Mrisho (marehemu), Elibariki Kitundu na kipa Ramadhani Lulandala. BoT ilishinda 3-1.


05 April

KLABU KUBWA NCHINI ZINAZIDIWA MAARIFA NA WASANII MAARUFU

Na Ally Kamwe, DAR ES SALAAM
UKIPITIA ripoti ya mwaka ya mapato ya klabu nyingi duniani, utaona zinategemea vyanzo vikuu vitatu vya mapato, ambavyo ni Haki za Matangazo ya Televisheni, Mauzo ya bidhaa za klabu na Mapato ya Viingilio vya mechi.
Wakati huu Ligi zikiwa zimesimama kwa sababu ya janga la maambukizi vya virusi vya corona au COVID 18, baadhi ya Klabu zimeanza kutetereka kiuchumi
Kwanini? Jibu ni rahisi sana. Vyanzo vyao vya mapato vimeathirika na virusi vya Corona. Mechi hazionyeshwi, mauzo ya bidhaa za klabu yameshuka, hakuna pato la viingilio.
Nguvu pekee iliyosalia ni fedha za wadhamini. Wenye Brand kubwa, wananufaika na madili makubwa waliyosaini.
Je, umeshawahi kujiuliza, Ni njia gani timu inaweza kuendelea kuzalisha mapato hasa katika kipindi hiki? 
Kuna fursa ya dhahabu kupitia DIGITAL PLATFOM za klabu ( Website, YouTube,  App, Instagram, Twitter na Facebook).
Ngoja nikwambie kitu, Februari 20, 2017, Manchestee United ilimwajiri Phil Lynch kama CEO wa kitengo cha MEDIA.
Kabla ya ajira hiyo, Lynch alishawahi kufanya kazi katika kampuni ya Yahoo na Sony Pictures. Miongoni mwa Kampuni kubwa sana duniani.
Kazi yake kubwa pale Old Trafford ilikuwa ni kutafuta jinsi gani Man United itatengeneza fedha zaidi kupitia mitandao
Kitu cha kwanza Lynch alichokifanya kwenye kazi yake ni kutofautisha kati ya FANS na FOLLOWERS.
Cha pili ilikuwa ni kufanya tafiti ya kujua ni tofauti ya umri gani unaofatilia mitandao yao? Wakati gani wanasomwa/kutazamwa sana, content zipi zinauza, na wana wafuasi sana maeneo gani duniani.
Ajabu ni kuwa, TANZANIA inashika nafasi ya 4 katika zile 5 a juu zinazoongoza kufatilia habari za Manchester United kupitia mitandao.
Lengo langu si kutaka kukuonyesha jinsi United wanavyofanya kazi, lengo ni kutaka kukuhabarisha kuwa IDARA HII YA HABARI ya United inachangia  11% ya pato la Timu kwa mwaka. 
Na kipindi hiki ambacho, matumizi ya mitandao yameongezeka, inatajwa United Idara hii itachangia kwa 17%. 
Nirudi kwenye hoja, juzi na jana, mmekuwa mkinitajia wapiga picha bora wa Klabu zetu za VPL
Jambo zuri zaidi, Wakuu wa Idara za klabu za Azam FC, Simba SC walishiriki kutaja vijana wao
Kaka yangu Dismas TEN nae akamtaja kijana wake Chicharito, kama mpiga picha bora. Ni kweli, vilabu vyetu vina wapiga picha bora, lakini tumeshawahi kujiuliza kama kweli KLABU ZETU zina vitengo bora vya Habari?
Tunawatumiaje hawa wapiga picha bora tulionao kutengeneza pato la klabu?
Simba wako active sana Instagram. Lakini YouTube kwenye hela iliyonyooka, wanadorora. Hawako active
Azam pia. Wanaposti kwa kusuasua. Yanga ndio aibu. Klabu kubwa mpaka leo haina akaunti ya Youtube iliyo active.
Wasanii wa Kitanzania wanaingiza fedha nyingi sana kwa mwezi kupitia biashara ya mitandao. Inawezekana vipi klabu yenye mashabiki zaidi ya Milioni 10 iwe na mapato SEFURI kwenye biashara ya mtandao? Kuna kitu hakiko sawa.
Vita imekuwa ni kugombea Followers ambao tunashindwa kujua thamani yao katika jicho la kibiashara.
Nafikiri umefika wakati sasa, Viongozi na Mashabiki kuanza kuwahoji Wakuu wao wa vitengo vya habari, MNA FAIDA GANI KWA TIMU YETU?
(Ally Kamwe ni mwandishi wa habari na mchambuzi wa Azam TV, unaweza kumfollow @allykamwe)


Saturday, 4 April 2020

04 April

KOCHA WA AZAM FC ASEMA WACHEZAJI WAKE WAPO KATIKA WAKATI, LAKINI HAKUNA NAMNA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema kwamba anafahamu wachezaji wake wapo katika wakati mgumu kufuatia klabu kusitisha maozezi ya pamoja kutoka na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona (COVID19).
“Najua ni wakati mgumu kwa wachezaji, wanataka kufanya mazoezi na kucheza, sio kukaa nyumbani, lakini wakati huu unahitaji kutuunganisha na kuwa na nguvu zaidi katika siku zijazo. Nawatakia kila mtu Tanzania na mashabiki wa Azam afya njema," amesema Cioaba.
Kocha huyo raia wa Romania, amekuwa akitoa programu za mazoezi binafsi kwa wachezaji katika kupindi hiki walichokuwa nyumbani kwa ajili ya tahadhari ya ugonjwa wa virusi vya CORONA (COVID - 19).
“Nadhani ni muhimu kwamba katika wakati huu mgumu tunaopitia kuonyesha umoja, mshikamano na uelewa," alisema. 
Machi 17, mwaka huu TFF ilisimamisha Ligi Kuu ya Tanzania Bara pamoja na mashindano yake mengine yote, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona duniani kote.  
Ligi Kuu ilisimama huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa pointi zake 71, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 54 baada ya timu zote kucheza mechi 28, wakati vigogo, Yanga SC ni wa tatu kwa pointi zao 51 za mechi 27 na Namungo wa nne wakiwa na pointi 50 za mechi 28.
Hali ni mbaya kwa Singida United inayoshika mkia kwa pointi zake 15 za mechi 29, nyuma ya Mbao FC pointi 22 mechi 28, Alliance FC pointi 29, mechi 29, Mbeya City pointi 30 mechi 29 na Ndanda FC pointi 31 mechi 29.


Friday, 3 April 2020

03 April

SIMBA SC YAWASHITUKIA WATU WANAOSAINI MIKATABA KWA NIABA YA KLABU BILA KUPEWA RUHUSA

Na Mwandishi Wetu, DARES SALAAM
UONGOZI wa Simba umesema kwamba haujatoa mamlaka kwa mtu yoyote au kundi la watu kuingia makubaliano au kusaini mikataba  kwa niaba ya klabu. 
Taarifa iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Senzo Mbatha Mazingisa mapema leo Jijini Dar es Salaam imesema kwamba mikataba na makubaliano yote yanayohusu klabu hiyo ni lazima yasainiwe katika ofisi zao tu.
“Imefahamika kwamba kuna baadha ya watu, makundi ya watu wamekuwa wakiingia makubaliano, mikataba na taasisi, kampuni nyingine wakijiwasilisha kama wafanyakazi, wawakilishi wa Kampuni ya Klabu ya Simba,”amesema Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Senzo Mbatha Mazingisa na kuongeza;
“Tunapenda kuujulisha umma kuwa, Simba haijatoa mamlaka kwa mtu yoyote au kundi la watu kuingia makubaliano au kusaini mikataba  kwa niaba ya Simba. Pia umma unajulishwa kuwa mikataba na makubaliano yote yanayohusu Simba ni lazima yasainiwe na Simba katika ofisi zetu,”.

Adha, Mtendaji huyo Mkuu wa Simba SC, Mazingisa ambaye ni raia wa Afrika Kusini amesema klabu inatoa rai kwa umma kuchukua tahadhari na watu au makundi ya watu wanaojiwasilisha kama wafanyakazi, wawakilishi wa klabu kwa ajili ya manufaa yao binafsi. 
“Simba inakemea vikali vitendo vya namna hii na inaomba wananchi kutoa taarifa za watu au makundi ya watu wa namna hii kupitia ofisi ya Mtendaji Mkuu,”ameongeza Mazingisa, mwenye uzoefu wa kufanya kazi na klabu kubwa kama Orlando Pirates FC, Platinum Stars za kwao za kampuni ya Ligi ya Afrika Kusini (PSL).
Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC ipo chini ya Mwenyekiti, Mohamed ‘Mo’ Dewji, Makamu wake, Salum Abdallah Muhene ‘Try Again’ na Wajumbe Hussein Kitta Mlinga, Dk. Zawadi Ally Kadunda, Suleiman Haroub Said, Asha Ramadhani Baraka na Mwina Mohammed Kaduguda, ambaye pia ni kaimu Mwenyekiti wa klabu baada ya kujiuzulu Swedy Nkwabi.


Thursday, 2 April 2020

02 April

TFF YAZUIA WADAU KUFIKA OFSINI KWAKE KARUME, SASA SHUGHULI ZITAENDESHWA KWA SIMU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), imezuia kuanzia sasa watu kufika kwenye ofisi zake zilizopo Uwanja wa Karume Ilala Jijini Dar es Salaam na badala yake watakuwa wakihudumiwa kwa njia ya simu.
Taarifa ya TFF leo imesema kwamba wamechukua hatua hiyo kama sehemu ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona (COVID 19) unaoitikisa dunia kwa sasa.
“Ili kuwakinga wadau wa mpira wa miguu na maambukizi ya virusi vya corona, kuanzia leo Aprili 2, 2020 hadi itakapotangazwa vinginevyo. Sekretarieti ya TFF inawaomba wadau watumie mawasiliano ya simu na barua pepe na pale panapokuwa na ulazima ndipo wafike katika ofisi zetu kwa ajili ya kuhudumiwa,”imesema taarifa ya TFF leo.
Taarifa iliyosainiwa na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo imeelekeza namba za mawasiliano kwa masuala mbalimbali zipo kwenye ukurasa wa Instagram wa shirikisho hilo.
Na hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Mtendaji Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kusema kwamba mustakabli wa msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utaamuliwa na vikao maalum iwapo janga la maambukizi ya virusi vya corona litaendelea.
Kidau alisema kwamba kama janga la COVID 19 litaendelea, msimu huu utategemea maamuzi yatakayofanywa na vyombo vinavyosimamia na kuendesha Ligi Kuu kwa pamoja na Kamati ya Utendaji ya TFF.
“Bado ni mapema sana kusema tumefuta msimu pamoja na kwamba msimu unaweza kwenda hadi Juni 31,” amesema Mtendaji Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao mapema leo alipozungumza na vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam.
Machi 17, mwaka huu TFF ilimesimamisha ligi zake zote ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona duniani kote.  
Pia TFF ilivunja kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa inajiandaa na fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zilizopangwa kuanza Aprili 4 hadi 25, mwaka huu nchini Cameroon ambazo pia zimeahirishwa kwa sababu ya COVID 19.
Kwa ujumla CAF ilisimamisha mechi zote za kufuzu za mashindano ya Afrika kwa ushauri wa Shirika la Afya Dunani (WHO) kufuatia mlipuko wa virusi vya corona hadi hapo itakapaoamuliwa vinginevyo.
Ligi Kuu ilisimama huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa pointi zake 71, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 54 baada ya timu zote kucheza mechi 28, wakati vigogo, Yanga SC ni wa tatu kwa pointi zao 51 za mechi 27 na Namungo wa nne wakiwa na pointi 50 za mechi 28.
Hali ni mbaya kwa Singida United inayoshika mkia kwa pointi zake 15 za mechi 29, nyuma ya Mbao FC pointi 22 mechi 28, Alliance FC pointi 29, mechi 29, Mbeya City pointi 30 mechi 29 na Ndanda FC pointi 31 mechi 29.


Wednesday, 1 April 2020

01 April

MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA NA EUROPA LEAGUE YASOGEZWA MBELE HADI JULAI NA AGOSTI

HATUA zijazo za michuano ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League zimeripotiwa kusogezwa hadi Julai na Agosti kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona linaloendelea duniani kote. 
Mechi zote za timu za taifa zilizopangwa kuchezwa Juni zimeahirishwa ili kuupisha msimu wa 2019-20 ukamilishwe.
Taarifa hiyo imetolewa na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) baada ya mkutano uliofanyka kwa video leo. 
Mechi, mashindano na ligi zote za soka Ulaya zimesitishwa tangu katikati ya Machi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, ulioanzia Wuhan huko China mwishoni mwa mwaka jana.

Michuano ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League imesogezwa mbele hadi Julai na Agosti kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona 


01 April

HATIMA YA LIGI KUU MSIMU HUU HADI SASA HAIELEWEKI, TFF YASEMA VIKAO MAALUM VITAAMUA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema kwamba mustakabli wa msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utaamuliwa na vikao maalum iwapo janga la maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona (COVID 19) litaendelea.
Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao mapema leo alipozungumza na vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam.
Kidau amesema kwamba kama janga la COVID 19 litaendelea, msimu huu utategemea maamuzi yatakayofanywa na vyombo vinavyosimamia na kuendesha Ligi Kuu kwa pamoja na Kamati ya Utendaji ya TFF.
“Bado ni mapema sana kusema tumefuta msimu pamoja na kwamba msimu unaweza kwenda hadi Juni 31,” amesema Mtendaji Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao mapema leo alipozungumza na vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam.
Machi 17, mwaka huu TFF ilimesimamisha ligi zake zote ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona duniani kote.  
Pia TFF ilivunja kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa inajiandaa na fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zilizopangwa kuanza Aprili 4 hadi 25, mwaka huu nchini Cameroon ambazo pia zimeahirishwa kwa sababu ya COVID 19.
Kwa ujumla CAF ilisimamisha mechi zote za kufuzu za mashindano ya Afrika kwa ushauri wa Shirika la Afya Dunani (WHO) kufuatia mlipuko wa virusi vya corona hadi hapo itakapaoamuliwa vinginevyo.
Ligi Kuu ilisimama huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa pointi zake 71, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 54 baada ya timu zote kucheza mechi 28, wakati vigogo, Yanga SC ni wa tatu kwa pointi zao 51 za mechi 27 na Namungo wa nne wakiwa na pointi 50 za mechi 28.
Hali ni mbaya kwa Singida United inayoshika mkia kwa pointi zake 15 za mechi 29, nyuma ya Mbao FC pointi 22 mechi 28, Alliance FC pointi 29, mechi 29, Mbeya City pointi 30 mechi 29 na Ndanda FC pointi 31 mechi 29.


01 April

KINDA MWINGINE WA TANZANIA, SAID JUNIOR ASAJILIWA NA KLABU YA ABU DHABI KWA MKATABA WA MIAKA MITATU

Mshambuliaji wa Mbao FC Said Khamis Said, maarufu kama Said Junior amejiunga na klabu ya Baniyas SC ya Al Shamkha, Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE) kwa mkataba wa miaka mitatu, akijunga na chipukizi mwingine, John Tibar George aliyesajiliwa kutoka MFK Vyskov ya Daraja la Pili ya Czech, baada ya kuzichezea Ndanda FC na Singida United za nyumbani 


Tuesday, 31 March 2020

31 March

MJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA KLABU YA SIMBA, IDDI MBITA AFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI DAR

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba, Idd Hashimu Mbitta amefariki dunia Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam.
“Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi, Iddi Mbita kilichotokea leo Alfajiri ya Machi 31, 2020 Jijini Dar es Salaam,” imesema taarifa ya SImba SC leo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya klabu ya Simba SC, Mohamed ‘Mo’ Dewji amesema kwamba ameumizwa mno na kifo cha Mbitta kwa sababu wamesoma pamoja shule ya Arusha, wamekuwa marafiki wa muda mrefu.
“Pumzika kwa amani mpendwa wetu Iddi. Tumesoma pamoja Arusha School, urafiki wetu tukaurithisha hadi kwa watoto wetu kuwa marafiki na sisi kuendelea kufurahia mechi za Simba pamoja. Pumzika kwa amani rafiki yangu, nasi tuko njiani. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un,”amesema Mo Dewji.
Naye Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Brigedia Hashimu Mbitta kufuata msiba huo.


Sunday, 29 March 2020

29 March

KIUNGO WA SIMBA SC, FRANCS KAHATA NYAMBURA AGAWA LITA 10,000 ZA MAJI SAFI KWAO MATHARE KUSAIDIA JAMII DHIDI YA CORONA

KIUNGO wa Simba SC, Francis Kahata Nyambura leo ametoa msaada wa maji safi lita 10, 000 katika eneo la Mathare nyumbani kwao, Jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19.
Kahata aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC ya Dar es Salaam bada ya kuwasili kutoka Gor Mahia ya kwao, Kenya ametoa msaada huo baada ya mashabiki wake wa eneo hilo kumuomba.

Friday, 27 March 2020

27 March

DK MSOLLA AWASIMAMISHA ‘WABISHI’ WAWILI KATIKA ORODHA YA WAPINGA UDHAMINI WA GSM

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Yanga SC umewasimamisha wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji, Salim Rupia na Frank Kamugisha kuanzia leo Machi 27, 2020 hadi hapo mkutano mkuu utakapofanya maamuzi kwa mujibu wa katiba.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa klabu, Dkt. Mbette Mshindo Msolla leo, imesema kwamba uamuzi huo umefikiwa leo baada ya kikao cha siku mbili mfululizo kilichofanyika Dar es Salaam kuanzia Mach 26 hadi 27.
Na hatua hiyo imefuatia kutokea sintofahamu iliyosababisha mdhamini wa klabu, Kampuni ya GSM kusitisha kutoa misaada iliyo nje ya mkataba wake.
Aidha, Kamati ya Utendaji ya Yanga imepokea na kukubali maombi ya wajumbe wengine watatu, Rodgers Gumbo, Shijja Richard na Said Kambi kujiuzulu nafasi zao na kwamba nafasi ya mjumbe wa kuchaguliwa itajazwa mara moja kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) wa Katiba ya Yanga.
Wakati huo huo Kamati ya Utendaji wa Yanga imewasilisha barua GSM kujibu barua yao yenye kumbu kumbu namba GSMGROUP/YANGA/LETTER/2/2020 ya tarehe 24/03/2020 kuhusu kujitoa udhamini wa maswala yasiyo ya kimkataba. 
Taarifa ya Mwenyekiti, Dk. Msolla imesema kwamba Barua hiyo imewasilishwa baada ya maamuzi ya pamoja ya kikao cha Kamati ya Utendaji leo.
Shijja na Kambi walikuwa Wajumbe wa kuteuliwa wakati Rupia, Kamugisha na Gumbo ni miongoni mwa Wajumbe waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Mei 5, mwaka jana Jijin Dar es Salaam.
Sasa Kamati ya Utendaji Yanga inabaki na Wajumbe watano wa kuchaguliwa ambao ni Hamad Islam, Mhandisi Bahati Faison Mwaseba, Dominick Ikute, Arafat Haji na Saad Khimji pamoja na Dk. Athumani Kihamia pekee wa kuteulwa chini ya Mwenyekiti Dk. Msolla na Makamu Mwenyekiti, Frederick Mwakalebela.


27 March

MAGWIJI AFRIKA WAUNGANA KATIKA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

MAGWIJI wa soka Afrika wameungana kutoa video fupi ya kampeni dhidi ya maambukizi virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 iitwayo #MikonoSalama na #MsishikaneMikono.
Video hiyo ya sekunde 98 imehusisha wachezaji wakiwa katika maeneo wanayoishi ikisistiza kunawa mikono na kuepuka kushikana mikono, ambayo husababisha kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19, unaotikisa dunia nzima kwa sasa.
Wawakilishi wa vizazi tofauti wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Anthony Baffoe wameshiriki video hiyo.

https://ift.tt/2xpUrFF

Hao ni pamoja na Roger Milla, Joseph Antoine Bell wa Cameroon, Herita Ilunga, Tresor Lomana Lualua wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), El Hadji Diouf, Alassane N’Dour, Khalilou Fadiga na Diomansy Kamara wa Senegal.
Wengine ni Mustafa El Haddaoui wa Morocco, Jean Ssenide wa Uganda, Wael Gomaa wa Misri, Fatau Dauda wa Ghana na Vincent Enyeama wa Nigeria.
Akina Diouf na Lualua wamezungumza kwa lugha na lafudhi za kwao, Wolof ya Senegal na Lingala ya Kongo ili kufikisha ujumbe kwa watu wa nchini mwao, wakati Mganda Ssenide ni mwanamke pekee katika kampeni hiyo.
Kutokana na ugonjwa wa COVID-19, CAF imesimamisha mashindano yake yote hadi hapo itakapoamuliwa vingnevyo – hiyo ikiwa ni kuunga mkono agizo la Shirika la Afya Duniani (WHO), FIFA na wengine katika mapambano dhidi ya janga hilo.


27 March

MJUMBE YANGA SC AWA WA KWANZA KUJIUZUKU TUHUMA ZA KUUTILIA SHAKA UDHAMINI WA GSM

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Shijja Richard amejiuzulu wadhifa huo leo, kufuatia tuhuma za kuhusishwa katika orodha ya wajumbe wanne wa klabu wanaodaiwa kuutilia shaka udhamini wa kampuni ya GSM.
Shijja, Mwandishi wa habari za michezo wa zamani, amesema kwamba ameamua kwa hiari yake kujiuzulu nafasi zote za uongozi katika klabu yangu ya Yanga. 
“Yanga ni kubwa kuliko mimi na kuliko mtu yeyote. Yamezungumzwa mengi lakini mimi sitazungumza chochote. Wakati utaongea. Ukweli hata usipousema, huwa una tabia ya  kujitokeza wenyewe japo taratibu lakini huwa unadumu milele,”amesema Shijja katika taarifa yake.
Shijja aliyewahi kugombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliopita na kuangushwa na Wallace Karia ni mmoja kati ya Wajumbe wanne wanaodaiwa kumpinga mdhamini wa klabu, kampuni ya GSM.
Pamoja na kuwa na mkataba wa udhamini wa vifaa vya michezo, kampuni ya GSM imekuwa ikijitolea kufanya mambo zaidi kuisaidia Yanga, lakini inadaiwa baadhi ya Wajumbe akiwemo Shijja, Salum Rupia, Rodgers Gumbo na Frank Kamugisha wanadaiwa kutilia shaka hilo.