;
EDUSPORTSTZ : Udaku

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Showing posts with label Udaku. Show all posts
Showing posts with label Udaku. Show all posts

Friday, 3 July 2020

03 July

Poshy Awajia Juu Wanawake


MREMBO ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na umbo lake kuonekana kuwavutia watu mbalimbali, Jacqueline Obeid ‘Poshy’ amefunguka kuwa wanaoongoza kwa chuki na roho mbaya ya kumchukia na kumzushia maneno ni wanawake wenzake na siyo wanaume.

Akizungumza na Risasi Vibes, Poshy alisema kuwa, amegundua kuwa kuna watu wengi au wanawake wengine hawapendi kuona mwingine anaendelea, hivyo kumuwekea kila aina ya chokochoko ili kumtibulia mambo yake, jambo ambalo linamkera.

"Watu tu wanashindwa kuelewa kuwa huku duniani kila mtu ana bahati yake, hivyo ukiona mwenzako anafanikiwa au mwanamke mwenzako anafanya vizuri, mshike mkono uzidi kumfanya ainuke ili akuinue na wewe na sio kumponda kila kukicha maana huo unaitwa ni wivu, tena wivu usiokuwa na maendeleo kabisa,” alisema Poshy, ambaye hivi karibuni habari zake zilisambaa mitandaoni kuwa ana ujauzito wa mwanamuziki Diamond jambo ambalo.


03 July

Zuchu Awa Tishio Kwa Mastaa wa Kike Bongo

Zuchu Awa Tishio Kwa Mastaa wa Kike Bongo

KAMA ameiona njia usiku, mchana ni ganda la ndizi, full kutereza; ndivyo itakavyokuwa kwa msanii Zuhura Kopa ‘Zuchu’.

Uchunguzi unaonesha kuwa msanii huyo ambaye ni memba wa mpya wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), ambaye aliweza kuchomoka kimuziki na kuwa tishio kipindi ambacho kasi ya Corona ilikuwa kubwa, anaweza kuoga utajiri nyakati hizi ambapo shughuli zote za kijamii zimefunguliwa na Serikali.

Zuchu ambaye Aprili mwaka huu alisajiliwa WCB, aliweza kufyatua nyimbo kali na kujipatia fedha kwenye mitandao huwenda kasi ya kupiga ‘mpunga’ mrefu ikaongezeka mara dufu atakapoanza kufanya shoo na matamasha mengine.

“Kwenye mtandao wa YouTube ameweza kutikisa na kupata fedha, namuona akipaa kisanii wapinzani wake wajipange, vinginevyo watarajie kupewa lifti na Zuchu,” mmoja aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwa kipindi hiki kifupi tena chenye giza la Virusi vya Corona, Zuchu alifanikiwa kuwa tishio kwa mastaa wengine wa kike Bongo kama Faustina Charles ‘Nandy’, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Vannesa Mdee ‘V Money’ na Mariane Mdee ‘Mimi Mars’ na wengine kibao.

Kuchomoka kwa staa huyo wa kike kumetabiriwa na wengi kuwa huenda anakwenda kuwa malkia wa Bongo Fleva kama alivyokuwa msanii Lady Jaydee miaka kadhaa iliyopita.


MAMBO ALIYOYAFANYA

Kipindi chote cha janga la Corona, Zuchu aliweza kuachia Extended Playlist (EP), yake ambayo ilikuwa imekusanya nyimbo sita na zote zilifanya vizuri katika mtandao wa YouTube kwa kutazamwa na watazamaji lukuki.Kishindo cha aina yake alikiweka YouTube ambapo kwa muda mfupi kazi zake zimetazamwa mara Milioni 12 ndani ya muda wa miezi mitatu tu na kumfanya Zuchu kama Zuchu kuwa juu.

Aidha, hivi karibuni aliweza kuishika Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuachia ngoma iitwayo Tanzania ya Sasa.Katika wimbo huo ambao uliwashika vilivyo viongozi wa serikali umejaa mashairi yenye kusifia mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya Magufuli.“Elimu ya msingi na sekondari bure Magufuli huyooReli yenye viwango bora standadi geji karibu inakamilika, Magufuli Hai“Baadhi ya viongozi walionesha kuvutiwa na ngoma hiyo, na kumsifia hadharani Zuchu, ni Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala.

SHOO MPYA

Kwa kipindi chote cha tishio la Corona na ujio wake msanii huyo hakuweza kufanya shoo yoyote, lakini baada ya Corona kufifia staa huyo chipukizi atafungua pazia lake la makamuzi jukwaani Juni 18 mwaka huu.Zuchu sambamba na menejimenti yake wameandaa shoo ya kufa mtu, siku hiyo ndani ya Ukumbi wa Mlimani City ambapo anatarajia kuvuna fedha ambazo huenda hajawahi kuzipata tangu amezaliwa.Inaonekana kuwa baada ya Zuchu kuonja utamu wa shoo huenda ndiyo ikawa safari moja ambayo itaanzisha nyingine.

MENEJIMENTI ITAMBEBA

Zuchu ni msanii ambaye amefanikiwa kuwa na menejimenti makini inayomsimamia, ambayo imetajwa mara kadhaa kuwa ndiyo inayomvusha kwenye msitu wa sanaa.Menejimenti hiyo ambayo iko chini ya Hamisi Tale ‘Babu Tale’, Said Fella ‘Mkubwa Fella’, pia inasimamia kazi za msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye ni bosi wa Zuchu, kwa mkono mwingine imekuwa na mipango mathubuti pamoja na platifomu ya kutosha kwenye mitandao ya kijamii ambayo ikiamua kufanya jambo, halishindikani.Ingawa hali ya Corona haijatulia dunia nzima, lakini kipindi hali itakapokuwa nzuri upo uwezekano wa Zuchu kuvuka mipaka ya nchi na kuwa msanii wa kimataifa

03 July

Waziri Bashungwa: Tanzania Kuingia Uchumi wa Kati Itavuta Wawekezaji Wengi.Waziri Bashungwa: Tanzania Kuingia Uchumi wa Kati Itavuta Wawekezaji Wengi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA),alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akiangalia bidhaa kutoka kiwanda cha kutengeneza vifaa vya Umeme cha AfriCAB alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akiangalia bidhaa kutoka kwa wajasiriamali wanaofadhiliwa na Benki ya Biashara Tanzania (NBC), alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Bidhaa zinazotokana na zao la Mkonge ambazo zinauzwa katika banda la Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) lililoko katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi wa Habari alipotembelea Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade), Dkt.Ng’wanza Kamata (Mwenye miwani) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bi.Latifa Khamis (wa pili kulia) alipotembelea Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO 

******************************* 

Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO 

Serikali imewataka Wananchi kuendelea kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini kwani chanzo cha nchi kufikia uchumi wa kati ni pamoja na wananchi wake kupendelea bidhaa ambazo wanazizalisha wao kama wao, na mafanikio yametokana na juhudi za watanzania wote wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli. 

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba) yanayofanyika katika Uiwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa amesema kuwa ili watanzania waweza kusheherekea mafanikio endelevu ya kuingia nchi zenye kipato cha kati wanatakiwa kuwa wa kwanza kutangaza bidhaa zao. 

“Kupitia mafanikio tuliyoyapata rai yangu kwa watanzania ni kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu ili mafanikio haya ya nchi kuwa kwenye orodha ya nchi zenye kipato cha kati yawe ni matunda kwa watanzania hasa kwa wakina mama na vijana wanaotafuta ajira na tukiendelea kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ndivyo tunazidi kutengeneza fursa za ajira kwa watanzania”. Alisema Mhe.Bashungwa. 

alisisitiza kuwa watanzania wanatakiwa kuangalia bidhaa za ndani Kabla hawajanunua bidhaa kutoka nje ili kuweza kukuza viwanda na kuwa na uchumi wenye kipato cha kati endelevu kwani ili Watanzania waendelea kusheherekea mafanikio haya ya kufikia kipato cha kati tunatakiwa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini. 

Alibainisha kuwa kupitia maonesho 44 ya Biashara kimataifa (sabasaba) ambapo takribani kampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi zitashiriki, kutakuwa na fursa ya wananchi kuja kununua bidhaa na kuangalia teknolojia mbalimbali zikioneshwa na taasisi na makampuni ya kitanzania, pia kupitia B2B wale ambao wapo nje wataendelea kuingia mikataba na wafanyabiashara ambao wanashiriki katika maonesho ya sabasaba hayo. 

Pamoja na hayo Mhe. Bashungwa amesema Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati inasaidia kuingia kwenye rada ya kimataifa hivyo wengi watapenda kuja kuwekeza hapa nchini


03 July

Ajali Mbaya ya Lori na Noah Yaua Watano DodomaAjali Mbaya ya Lori na Noah Yaua Watano Dodoma
Watu 5 wamefariki na 2 kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Noah lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Dodoma kugongana na lori eneo la kibaigwa jijini Dodoma .

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha. 

Amesema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa lori ambaye aliingia katikati ya barabara akitokea kwenye kituo cha mafuta bila kuangalia pande zote za barabara na kusababisha Noah kuingia uvunguni mwa lori.  

Pia ameeleza kuwa dereva wa lori ametoroka na jeshi la polisi linaendelea kumsaka huku likifanya uchunguzi zaidi wa ajali hiyo.

Kuhusu majeruhi wawili wa ajali hiyo Muroto amesema mmoja ana hali mbaya zaidi na juhudi za madaktari zinaendelea katika kunusuru uhai wake.03 July

Ukimtoa Whozu, Lulu Diva ndiyo anafuata Kuumizwa Katika Mapenzi" - Marioo
Kupitia kipande cha video fupi aliyo-post msanii Marioo "Toto Bad" ameeleza kuwa ukimtoa Whozu staa mwingine ambaye anafuatia kwa kuumizwa na kuonewa kwenye mapenzi ni Lulu Diva.


Marioo amefahamisha hivyo baada ya kupata bahati ya kuonana na Lulu Diva ambaye amemuuliza kwanini ameandika wimbo ambao baadhi ya vitu vinamuhusu yeye.

"Aaaaam Lulu Diva ni moja kati ya mastaa ambao washawahi kuumizwa au kuonewa katika mapenzi tukiachana na Whozu, sasa leo tulipata bahati ya kuonana akawa ananiuliza nimewaza nini mpaka nikaandika huu wimbo maana ndiyo wimbo anauskiliza kutwa nzima kwa hiyo nikawa namuelezea baadhi ya vitu kuhusu wimbo" ameeleza

Kwa sasa Whozu yupo kwenye mahusiano na video vixen Tunda, na Lulu Diva bado hajaweka mahusiano yake wazi japo awali aliwahi kuhusishwa kuwa na TID, Rich Mavoko na Jaguar.03 July

Tapeli Hush Puppi na Wenzake 12 Wakabithiwa Mikononi Mwa FBI Marekani...

Mwanamtandao maarufu wa nchini Nigeria @hushpuppi na wenzake 10 wamekabidhiwa kwenye mikono ya Shirika la Kijasusi (FBI) na kufikishwa nchini Marekani, eneo ambalo wanadaiwa kutenda uhalifu wao. Zoezi hilo limefanywa na polisi wa Dubai ambao waliwakamata mapema mwezi uliopita.

Hushpuppi na wenzake hao walitiwa nguvuni na kikosi kazi cha polisi wa Dubai kwa ushirikiano na Polisi wa Kimataifa kwenye operesheni iliyopewa jina la Fox Hunt 2. Wanatuhumiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo Utapeli, Utakatishaji fedha, Udukuzi, Wizi kwenye taasisi za Kibenki na Utapeli wa mtandaoni ambapo wanadaiwa kudukua barua pepe na tovuti za mabenki kisha kujihamishia fedha kwenye akaunti zao.

Mbali na kuwakuta na pesa taslimu kiasi cha TSH. Bilioni 92.7, Hushpuppi na genge lake wanadaiwa kutapeli takribani Trilioni 1 za Kitanzania kwa watu milioni 1.9 duniani. Pia wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kuhamisha fedha kiasi cha TSH. Bilioni 81 za ununuzi wa vifaa vya Upumuaji 'Ventilators'' kutoka Serikali ya Marekani kwenda kwa raia wake waishio Afrika.

03 July

Tapeli Hush Puppi na Wenzake 12 Wakabithiwa Mikononi Mwa FBI Marekani...

Mwanamtandao maarufu wa nchini Nigeria @hushpuppi na wenzake 10 wamekabidhiwa kwenye mikono ya Shirika la Kijasusi (FBI) na kufikishwa nchini Marekani, eneo ambalo wanadaiwa kutenda uhalifu wao. Zoezi hilo limefanywa na polisi wa Dubai ambao waliwakamata mapema mwezi uliopita.

Hushpuppi na wenzake hao walitiwa nguvuni na kikosi kazi cha polisi wa Dubai kwa ushirikiano na Polisi wa Kimataifa kwenye operesheni iliyopewa jina la Fox Hunt 2. Wanatuhumiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo Utapeli, Utakatishaji fedha, Udukuzi, Wizi kwenye taasisi za Kibenki na Utapeli wa mtandaoni ambapo wanadaiwa kudukua barua pepe na tovuti za mabenki kisha kujihamishia fedha kwenye akaunti zao.

Mbali na kuwakuta na pesa taslimu kiasi cha TSH. Bilioni 92.7, Hushpuppi na genge lake wanadaiwa kutapeli takribani Trilioni 1 za Kitanzania kwa watu milioni 1.9 duniani. Pia wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kuhamisha fedha kiasi cha TSH. Bilioni 81 za ununuzi wa vifaa vya Upumuaji 'Ventilators'' kutoka Serikali ya Marekani kwenda kwa raia wake waishio Afrika.

03 July

Tapeli Hush Puppi na Wenzake 12 Wakabithiwa Mikononi Mwa FBI Marekani...

Mwanamtandao maarufu wa nchini Nigeria @hushpuppi na wenzake 10 wamekabidhiwa kwenye mikono ya Shirika la Kijasusi (FBI) na kufikishwa nchini Marekani, eneo ambalo wanadaiwa kutenda uhalifu wao. Zoezi hilo limefanywa na polisi wa Dubai ambao waliwakamata mapema mwezi uliopita.

Hushpuppi na wenzake hao walitiwa nguvuni na kikosi kazi cha polisi wa Dubai kwa ushirikiano na Polisi wa Kimataifa kwenye operesheni iliyopewa jina la Fox Hunt 2. Wanatuhumiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo Utapeli, Utakatishaji fedha, Udukuzi, Wizi kwenye taasisi za Kibenki na Utapeli wa mtandaoni ambapo wanadaiwa kudukua barua pepe na tovuti za mabenki kisha kujihamishia fedha kwenye akaunti zao.

Mbali na kuwakuta na pesa taslimu kiasi cha TSH. Bilioni 92.7, Hushpuppi na genge lake wanadaiwa kutapeli takribani Trilioni 1 za Kitanzania kwa watu milioni 1.9 duniani. Pia wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kuhamisha fedha kiasi cha TSH. Bilioni 81 za ununuzi wa vifaa vya Upumuaji 'Ventilators'' kutoka Serikali ya Marekani kwenda kwa raia wake waishio Afrika.

03 July

Ishu ya Morisson yazua sura mpya ,aambiwa asiwe mkubwa kuliko timuMchambuzi wa masuala ya michezo amesema kuwa Bernard Morrison hapaswi kuwa mkubwa kuliko timu hivyo lazima uongozi uweke usawa katika hili.

Mayay amesema kuwa kutokana na mvutano uliopo kwa sasa kati ya Yanga na mchezaji huyo Morrison ilipaswa mambo yamalizwe kitaalamu na kila kitu kiwekwe sawa kabla ya kumrejesha kwenye kikosi.

Mchambuzi huyo ameongeza kuwa hakuna mafanikio ambayo mchezaji anaweza kuyapata ikiwa hatakuwa na timu hivyo ni lazima aiheshimu timu.

"Ni lazima mchezaji asiwe juu ya klabu kwa namna yoyote ile inaharibu na kupoteza uhalisia wa maisha ya wachezaji na ndio jambo ambalo huwa linawaumiza wachezaji wengine.

"Kwa suala la Morrison ilipaswa uongozi wa Yanga uweke mambo yanayoendelea bayana ili mashabiki wajue kuna nini ambacho kinaendelea.

"Ukitazama hakuna mchezaji ambaye amewahi kujulikana ikiwa hana timu hivyo ili aweze kupata mafanikio ni lazima awe na timu ambayo ni kubwa kuliko mchezaji," amesema Mayay.

Morrison jana alirejea kikosini na kuanza mazoezi na wachezaji wenzanke ambao leo wameanza safari kuelekea kwenye mchezo wa Biashara United.03 July

Rosa Ree: Natamani Kuitwa Mama

Rosa Ree: Natamani Kuitwa Mama

SEX Lady kunako anga la muziki wa Hip Hop, Rosary Robert ‘Rosa Ree’ amefunguka kuwa kwa sasa naye anatamani kuitwa mama.Akizungumza na Risasi Vibes, Rosa Ree amesema kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa siyo kuwa msanii mkubwa, bali ni kuja kuwa na familia yake akiwemo, muwe pamoja na mtoto.

“Ndoto yangu ilikuwa siyo kuja kuwa msanii mkubwa, ndoto ambayo natamani siku moja itimie ni kuja kuitwa mama, natamani siku moja nije kuwa mke bora wa familia yangu,” alisema Rosa Ree ambaye muonekano wake ni wa ‘kigumu

03 July

Chifu Alia na Mtendaji Aliyekata Mti wa Kimila “Rudisha Mizimu Yangu”Chifu wa kabila la wagogo, Henel Mazengo wa pili, amemtupia lawama Ofisa Mtendaji wa kata ya Mvumi Makulu, Chamwino jijini Dodoma kwa kukata mti wa kimila.

Chifu Mazengo ameeleza kitendo cha kukatwa kwa mti huo kimemuondolea mizimu yake aliyokuwa anatumia kwenye kazi zake za kimila na kumtaka ofisa huyo kurudisha mizimu hiyo.

“Mimi ninachotaka ni watu wangu (mizimu) warudi kwa sababu hapa nilipo siwezi kufanya shughuli zozote za kichifu kwa sababu watu wangu hawapo” amesema Chifu huyo.

Chief Henel Mazengo amebainisha kuwa yeye ameshindwa kurejesha mizimu hiyo ambayo ni nyuki wa kizimu kwa sababu imekataa kurudi kwani nyumba yao imeharibiwa.

Ofisa huyo amejitetea kwa kusema alikuwa hajui kama mti huo ilikuwa unatumiwa kwa shughuli za kimila na ndiyomaana alitoa kibali cha mwananchi kukata mti huo kwaajili ya shughuli zake za ujenzi.

Aidha ameongeza kuwa yeye pia hawezi kuwarudisha nyuki hao hivyo ameomba waende kwenye vyombo vya sheria kwani tokea ameanza kazi hapo, hajawahi kuambiwa kuwa ule mti ni wakimila na mwenye jukumu la kusema ni chifu mwenyewe ambaye hakufanya hivyo.

03 July

Irene Robert: Sijaolewa Bado Jamani!


Licha ya urembo alionao, Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili nchini, Irene Robert, amesema bado hajaolewa kama watu wengi wanavyomzushia ila yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mungu akipenda atafunga ndoa na mpenzi wake huyo.

Irene ambaye anatamba hivi sasa na ngoma yake mpya ya Nivushe, amesema wakati wa Mungu ndio wakati sahihi zaidi hivyo ukifika basi atauaga ukapela.

Kuhusu historia yake ya muziki, Irene amesema amezaliwa na kukulia kwenye familia ya wacha Mungu, na alianza kuimba kwaya kanisani tangu akiwa mdogo na ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa mwanamuziki mkubwa kama ilivyo sasa.

03 July

Rais Donald Trump Bana...Agoma Kabisa Kuvaa Barakoa "Kuvaa Barakoa ni Uchaguzi Binafsi wa Mtu"

Rais Donald Trump, ambaye siku zote amekuwa akipinga muongozo wa uvaaji barakoa uliotolewa na maafisa wa afya, amesema atavaa barakoa kama atakuwa ''katika mazingira ya watu yatakayomlazimu kufanya hivyo''.

Bwana Trump ambaye amekwepa kujitokeza mbele Umma akiwa amevaa barakoa, pia amekuwa akishikilia msimamo wake kuwa kufunika uso hakuhitaji kuwa suala la lazima katika kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.

Kauli yake aliyoitoa kwa Fox News imekuja siku moja baada ya kiongozi wa Republican kutoa wito kwa Bwana Trump kuvaa barakoa ili aoneshe mfano.

Majimbo kadhaa nchini Marekani yameshuhudia ongezeko la maambukizi na vifo siku za hivi karibuni.

Marekani sasa ina watu zaidi ya milioni 2.6 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona na vifo zaidi ya 127,000.

Rais amesema nini?
Akizungumza na kituo cha habari cha Fox Business Network siku ya Jumatano, Bwana Trump alisema : ''Ninaunga mkono barakoa.''

Alipoulizwa kama atavaa barakoa, rais alisema: ''Kama nitakuwa kwenye mazingira ambayo yatalazimu kufanya hivyo.''

Aliongeza kuwa watu wameshawahi kumuona akiwa amevaa barakoa hapo kabla.

Bwana Trump alisema ''hatakuwa na tatizo '' kuvaa barakoa mbele Umma akisema ''na ni kama anapenda'' anavyoonekana akiwa amevaa barakoa.

Lakini Rais amerejea tena msimamo wake kuwa hafikirii kuwa kufunika uso linahitaji kuwa suala la lazima nchini Marekani, kwa kuwa kuna ''maeneo mengi nchini humo ambayo watu hukaa kwenye umbali mkubwa''.

''Kama watu wanahisi vizuri kuhusu suala hilo wavae.''

Bwana Trump aliulizwa pia kama anaamini bado kuwa virusi vya corona siku moja ''vitatoweka''.

''Ninaamini'' alisema .Ndio hakika, Wakati wa sherehe zijazo za uhuru tarehe 3 mwezi Julai, watu watakaohudhuria wanaomuunga mkono hawatalazimika kuvaa barakoa wala kulazimishwa kutochangamana.

Kituo cha kudhibiti magonjwa (CDC) mwezi Aprili kilipowataka watu kuvaa barakoa au kujifunika na nguo wanapokuwa maeneo ya watu wengi ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi, Bwana Trump aliwaambia wanahabari kuwa hatafuata kanuni hiyo.

''Sidhani kama nitafanya hivyo,'' alisema wakati huo.

''Kuvaa barakoa ninapowasalimia marais, mawaziri, maikteta, wafalme na malkia- kwa kweli sioni nikivaa.''

Lakini Trump amesisitiza mara kwa mara kuwa kuchagua kufuata muongozo wa wataalamu wa afya kuhusu barakoa ni suala la uamuzi binafsi.

Mwezi uliopita, aliliambia jarida la Wall Street kuwa baadhi ya watu huvaa barakoa kama jambo la kiasiasa dhidi yake.

03 July

UDSM watengeneza kifaa tiba (VENTILATOR) kuokoa watoto wachanga
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kupitia kurugenzi ya ubunifu na ujasiliamali wametengeneza kifaa tiba (Ventilator) kwaajili ya kumsaidia mtoto mchanga mwenye matatizo ya upumuaji. 

Akizungumza katika maonesho ya 44 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam Mhandisi Majili Killo amesema wameamua kutengeneza kifaa tiba hicho ili kuweza kusaidia watoto hasa katika vituo vidogo vya afya ambavyo haviwezi kupata mashine hiyo kwa urahisi. 

Amesema kuwa Kurugenzi ya Ubunifu na Ujasiliamli iliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unahifadhi vijana wabunifu na wajasilimali kufikia ndoto zao 

“Mimi pamoja na wanafunzi wangu tulikuwa na ndoto ya kutengeneza kifaa hili maalumu (Ventilator) kwaajili ya watoto wadogo wanapozaliwa siku 0 hadi 28 na zaidi ya hapo inawezekana amezaliwa kabla ya siku (Watoto njiti) au wamezaliwa kawaida lakini akapata shida ya changamoto ya afya”. Amesema Mhandisi Killo. 

Aidha Mhandisi Killo amesema kifaa tiba hicho hakina gharama pia kinaweza kutumika mahali ambapo umeme unatumika wa sola,jenereta au betri. 

Pamoja hayo Mhandisi Killo amesema kifaa tiba hicho kinauwezo wa kuangalia mwenendo wa moyo wa mtoto kama unamatatizo. 

Hata hivyo Mhandisi Killo amesema lengo la kutengeneza kifaa tiba hicho ni pamoja kuhokoa gharama pia kusaidia vituo vidogo vya afya kuweza kupata kifaa tiba hicho kwaajili ya kumlinda mtoto.Thursday, 2 July 2020

02 July

Benard Membe: Nitagombea Urais endapo wapinzani wakiungana
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe, anasema ikiwa vyama vya upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu. 

Membe amesifia sehemu ya utendaji kazi wa Magufuli, lakini ameyataja baadhi ya mambo ambayo anasema ikiwa hayatabadilishwa, basi yataitumbukiza nchini matatani. Katika mahojiano haya maalum na mwandishi wa BBC Sammy Awami kutoka nyumbani kwake, katika kijiji alichozaliwa Membe alianza kwa kutoa tathmini ya uongozi wa Rais Magufuli


02 July

Shabiki Ataka Rosa Ree Achukuliwe na WCB "Rosa Ree Anaweza Peleka Mbio Hip Hop ya Africa"


Ameandika Silver katika ukurasa wa maoni wa Youtube:

"In my opinion. .... WCB since kondeboy aondoke saizi ni upuzi mtupu umebaki huko..... then boom zuchu akaja na kishindo ila hana malengo ....... target yake nj east Africa. ..... USHWAHILI mwingi. ...... rosaree .......... rosaree anaeza peleka mbio hawa mabinti wa wafrica akipata support vizuri.....wcb is big...... imagine ROSA AKIWA WCB. ......... HIPHOP ya east Africa isonge....... love from Kenya. ....." Silver
Baadhi ya Maoni Mengine:

Pollution G.O.A.T ameandika:
 "Rosa ree is the quuen of rap in Africa
N khaligraph Jones is the King
Hip hop is the Kingdom
How many are their subjects?"

Godfrey Raphael Ameandika:
 This girl is simply genius, have listened to some of her music and she BAAAD, Lyrically and confidence..On point.."Tazama Hapa chini Wimbo wake Mpya:
02 July

Mwigizaji wa Ghana Aliyepiga Picha za Utupu na Mtoto Wake, Aomba radhi


Mwigizaji wa Ghana wa Rosemond Brown maarufu kama Akuapem Poloo ameomba radhi baada ya kupost picha ya utupu (kama alivyozaliwa) akiwa na mtoto wake wa miaka saba.

Akuapem Poloo alipost picha hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram Jumatatu, Juni 30, 2020 kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake aliyetimiza miaka saba.

Watu mbalimbali, vyombo vya habari, walimtuhumu mwigizaji huyo pamoja na mashirika kadhaa ya asasi za kiraia, na Shirika la Haki za watoto la Kimataifa kuitaka Idara ya Upelelezi wa Jinai ya Polisi (CID) ya Huduma ya Polisi ya Ghana kuangalia jambo hilo kuwa ni kama uvunjaji wa kanuni ya ustawi wa Sheria ya Mtoto.

Pamoja na kuomba msamaha alisema; Yeye huoga bafuni pamoja na mtoto wake huyo kila wakati.

02 July

Baharia wa kike afunguka wanavyokutana navyo

 
Najua umeshasikia neno Baharia, na wengi wao wanaotumia huwa ni wanaume, sasa leo tunakukutanisha na baharia wa kike aitwaye Dilshard Multaza ambaye anatueleza kuhusianan na miasha ya ubaharia wa kike na changamoto anazokutana nazo.


Akizungumza kwenye kipindi cha Mama Mia ya East Africa Radio inayoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 4:00 Asubuhi hadi 6:00 Mchana Baharia Dilshard Multaza amesema,

"Inaniuma sana kuona Baharia wa kike anasoma halafu hapati kitu, sisi ndiyo tunafanya uwezeshaji tunataka tutambulike na tupewe heshima yetu, kwa ujumla hali ya bahari ni ngumu sana kuna muda inachafuka ghafla,tunapata majanga mengi, tunakufa, meli kuondoka na mizigo, kupoteza abiria na tunashutumiwa kwamba ndiyo tuna sababisha matatizo kwa hiyo ikitokea hivyo unapoteza muelekeo"

Mengine zaidi aliyoyazungumza kuhusiana na maisha ya baharia wa kike, mikasa na wanavyokutana navyo, tazama kwenye video hapa chini

02 July

Bilionea Laizer kamsomesha kijana huyu hadi chuo kikuu,sasa ni meneja wa mgodi wake


Kiria Laizer ni kijna ambaye amesomeshwa hadi chuo kikuu na Bilionea Laizer na kwa sasa ameajiriwa katika mgodi wake katika nafasi ya meneja

“Mimi ni mdogo wake wa mwisho kwa mama,mimi kupewa nafasi ya meneja proffesional ni mtawala,ndio maana alinikabidhi aliona kwamba na sifa hiyo na leo hii hata unaona mafanikio haya makubwa kwa sababu tulisimamia kazi kitaalamu”-Kiria