Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limepanga makundi ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 17.
Fainali hizo zitazopangwa nchini India baadae mwaka huu, zitashuhudia Tanzania ikishiriki kwa mara ya kwanza ikitokea Barani Afrika.
Timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imepangwa Kundi D na timu za Ufaransa, Canada na Japan.
Timu nyingine kutoka Afrika zitakazoshiriki Fainali hizo ni Morocco iliyopangwa Kundi A na Nigeria iliyoangukia Kundi C.
Fainali hizo zimepangwa kuanza kuunguruma Oktoba 11 hadi 30.
No comments:
Post a Comment