;
EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 9 July 2020

09 July

Bushoke Amrudisha K-Lynn Kwenye Game

Bushoke Amrudisha K-Lynn Kwenye Game

KAMA ilivyokawaida mpendwa msomaji wa kolamu hii ya Yupo Wapi kukuletea waliowahi kuwa mastaa na kisha kupotea, ambapo leo nimekuletea mwanamuziki wa kizazi kipya Ruta Bushoke ambaye alipata ustaa kufuatia ukali wa ngoma zake kadhaa ikiwemo Barua, Mume Bwege, Dunia Njia pamoja na Nalia kwa Furaha aliyoshirikiana na K-Lynn na Usiende Mbali aliyoshirikiana na Juliana Kanyomozi na nyinginezo.

Baada ya kimya cha muda mrefu, Bushoke ameanzisha bendi yake iitwayo Urithi ambayo inapiga nyimbo zake pamoja na kugonga kopi ya nyimbo zilizowahi kutamba enzi hizo.

Maongezi kati ya Bushoke na paparazi wetu yalikuwa kama ifuatavyo.

Risasi: Bushoke kwanza mashabiki wa burudani wangependa kujua historia yako kiufupi ulivyoanza muziki.

Bushoke: Mimi natoka kwenye familia ya mzee Maximmilin Bushoke ambaye ni mwanamuziki mkongwe, hilo ndilo kuu lililosababisha nianze muziki nikiwa mdogo sana tukiwa tunaishi Dodoma.

Risasi: Enhe ikawaje?

Bushoke: Nikiwa nasoma Shule ya Msingi Makore iliyopo Dodoma, nilijiunga na wanafunzi wenzangu tukaanzisha kundi letu lililoitwa Makore Exagone, hapo ndipo mzuka wa muziki ukaanza kunipanda.

Risasi: Kuna kipindi ulikuwa ukitoa ngoma kali kila baada ya muda fulani, lakini sasa hivi umekuwa kimya kiasi cha kupigwa ‘ovateki’ na wasanii wanaochipukia nyuma yako kama kina Diamond, Harmonize, Mbosso, Aslay na wengineo?

Bushoke: Muziki wa zamani kipindi chetu na sasa hivi ni tofauti, sisi tulikuwa tukiweka nguvu kubwa kwenye muziki lakini wenzetu wanaweka nguvu kubwa kwenye kiki kuliko muziki, unakuta mwanamuziki eti analindwa na mabaunsa kibao mpaka unajiuliza huyo adui akudhuru kwa lipi? Hivyo, hizi kiki zao ndiyo zinawapandisha kwakuwa

Mashabiki wa siku hizi nao wanapenda vitu hivyo.

Risasi: Kwani wewe hupendi kiki?

Bushoke: Mimi sipendi kabisa hizo kiki zao haswa hizo za mabaunsa, napenda kuishi huru katika jamii.

Risasi: Ngoma yako uliyoshirikiana na K-Lynn; Nalia kwa Furaha, ilikuwa gumzo ndani na nje ya Bongo, vipi kwasasa unapowasiliana naye mnajadiliana nini kuhusu muziki?

Bushoke: Tunajadiliana mambo mbalimbali ya kimaisha, lakini suala la yeye kuendelea na muziki tangu aolewe isingekuwa rahisi kwakuwa muziki una mambo mengi, naye mumewe alikuwa mtu mzima, hivyo haikuwa rahisi na hata sasa mumewe amefariki lakini bado kuna masuala ya familia anafuatilia kuyaweka sawa, ila akitulia ntamshauri aje tuendeleze kipaji chetu maana akiachana kabisa na muziki, ni sawa na kuua kipaji chake.

Risasi: Vipi ratiba ya bendi yako Urithi ikoje.

Bushoke: Urithi Band kama kawa kila Alhamisi na Jumamosi tunapiga shoo hapa Dodoma ambapo ndiyo tumepiga kambi kwasasa.

Risasi: Vipi kuhusu familia umeoa?

Bushoke: Bado kidogo sijaoa, ila namshukuru Mungu nina watoto watatu ambapo wakike wawili na wakiume mmoja

09 July

Afariki Akimwokoa Mwanaye Nyumba Ikiteketea

Afariki Akimwokoa Mwanaye Nyumba Ikiteketea

INASIKITISHA sana! Mwanamke mmoja amemwokoa mtoto wake kwa kumrusha kupitia kibarazani wakati ajali kubwa ya moto uliotokea na kuteketeza nyumba yao ya gorofa ya tatu huko Phoenix, Arizona, Marekani.

Inaripotiwa ndani ya nyumba alikuwepo mama na mtoto ambapo kwenye hiyo video mama anaonekana akimuokoa mtoto wake kwa kumrusha chini kupitia kibarazani na kutajwa kuwa mwanamke shujaa.

Kwa mujibu wa ABC NEWS, mama huyo alifariki kwa kuwa alikuwa ameungua sana lakini alipambana na kuhakikisha amefika kibarazani na kumrusha mtoto wake chini ambapo alidakwa na watu wawili.

09 July

GSM Watupa Kombora Simba SC

GSM Watupa Kombora Simba SC

MKURUGENZI Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said, amesema kuwa ni aibu kwa timu hiyo kumaliza msimu bila ya kubeba kombe, huku akiahidi kupambana kulichukua Kombe la Azam Sports Federation.

Kauli hiyo ni salamu tosha kwa watani wao Simba wanaotarajiwa kupambana nao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili hii ukiwa ni mchezo wa nusu fainali.

Simba tayari mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na jana Jumatano walikabidhiwa kombe lao baada ya kucheza dhidi ya Namungo kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

Akizungumza na Spoti Xtra, Said ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili Yanga, alisema kuwa GSM haijawahi kushindwa, hivyo kama wadhamini watahakikisha wanafanya maandalizi makubwa ya timu yao kwa kuwafunga Simba na kuchukua kombe hilo.

Said alisema kuwa, Yanga ni kati ya klabu kubwa Afrika, hivyo ni aibu kwao kumaliza msimu huu bila ya kombe lolote, hivyo amewataka mashabiki wa timu hiyo kuungana kwa pamoja katika kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba kwa kujitokeza uwanjani kuwasapoti wachezaji.

“Ni aibu kwa timu kubwa kama Yanga katika ukanda huu wa Afrika kushindwa kuchukua kombe, hivyo kama wadhamini tumepanga kufuta aibu hiyo kwa kuhakikisha tunafanya kila liwezekano lililokuwepo ndani ya uwezo wetu ili tuchukue ubingwa huu.

“Tumeandaa kambi nzuri na bonasi za wachezaji kuelekea mchezo ujao wa nusu fainali dhidi ya Simba, lengo ni kuwaongezea morali wachezaji ya kupambana ili malengo yetu ya kuchukua kombe hilo yatimie,” alisema Said.

09 July

Anunua Barakoa ya Dhahabu Kujikinga na Corona

Anunua Barakoa ya Dhahabu Kujikinga na Corona

MWANAUME mmoja nchini India ametumia Sh milioni 8.6 kununua barakoa ya dhahabu ili kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.

Barakoa hiyo yenye uzito wa gramu 60, iliwachukua wasanifu wa bidhaa hiyo siku nane kumtengenezea mfanyabiashara Shankar Kurhade, barakoa hiyo maalumu.

“Ni nyembamba na ina mashimo madogo madogo yanayokuwezesha kupumua, sina uhakika iwapo itanilinda dhidi ya virusi, lakini nachukua tahadhari nyingine,” alisema Shankar.

Anapoondoka kwake kuelekea kwenye shughuli za kila siku, mfanyabiashara huyo hupenda kujistiri kwa dhahabu ikiwemo mshipi wake, shanga na mkufu vyote vyenye uzito wa takriban kilo moja.

Kurhade alisema alipata wazo la kutengenezewa barakoa ya dhahabu baada ya kuona katika vyombo vya habari mwanaume mmoja akivalia iliyotengenezwa kwa fedha.


"Kutokana na upekee wa hii barakoa yangu, nimekuwa nikipata usumbufu kutoka kwa watu ambao wanataka nipige nao selfie,” alisema.

Tangu kuibuka kwa maambukizi ya Virusi ya Corona duniani Desemba mwaka jana na kuanza kusambaa sehemu mbalimbali duniani, Nchi ya India imefanya uvaaji wa barakoa kuwa jambo la lazima katika maeneo ya umma.

Hadi kufikia Julai 6, mwaka huu, nchi hiyo ilikuwa na idadi ya watu 700,000 walioambukizwa Corona huku watu 19,707 wakipoteza maisha kutokana na virusi hivyo ambavyo vimechukua uhai wa watu 540,000 duniani.
09 July

Niyonzima Ashusha Presha Yanga SC

Niyonzima Ashusha Presha Yanga SC

AKIUKOSA mchezo wa jana Jumatano wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, kiungo mchezeshaji fundi wa Yanga raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima, ameibuka na kutamka kuwa mashabiki waondoe hofu kwani anaendelea vizuri kiafya na Mungu akijaalia atakuwepo sehemu ya kikosi kitakachowavaa Simba.

Kiungo huyo alishindwa kumaliza mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United baada ya kuchezewa vibaya dakika ya kumi na kusababisha apate jeraha la goti ambalo limemuweka nje na kuzua hofu ya kuukosa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation utakaochezwa Jumapili hii.

Akizungumza na Spoti Xtra, Niyonzima alisema kuwa hivi sasa anaendelea vizuri huku akiendelea na matibabu ya majeraha yake ili kuhakikisha anakuwepo sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya Simba.

Niyonzima alisema kutokana na matibabu anayoendelea kuyapata, ana uhakika mkubwa wa kucheza pambano hilo, hivyo mashabiki waondoe hofu, kikubwa waendelee kumuombea ili apone vizuri.“Nafahamu umuhimu mkubwa wa mchezo wetu wa nusu fainali dhidi ya Simba ambao ni lazima tupate matokeo mazuri ya ushindi.

“Ninaamini matokeo mazuri ya ushindi yatatutengenezea rekodi na kubwa zaidi kwetu wachezaji ni kufuzu hatua ya fainali na hatimaye kulichukua kombe hilo ili tushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

“Wachezaji wote malengo yetu ni kuhakikisha tunalichukua kombe hilo ili tucheze michuano ya kimataifa kwa ajili ya sisi wachezaji tujitengenezee soko nje ya nchi ambayo ndiyo malengo yetu,” alisema  Niyonzima.

Wakati Niyonzima akitoa kauli hiyo, kuna hatihati ya nyota wengine wa Yanga kukosekana katika mchezo huo ambao ni Juma Abdul na Papy Tshishimbi, huku Balama Mapinduzi akikosekana rasmi. Hawa wote ni majeruhi.

09 July

Mwalimu Aliyembaka Mwanafunzi Wake na Kisha Kufunga Naye ndoa AmefarikiAliyekuwa mwalimu katika jimbo la Washington ambaye uhusiano wake na mwanafunzi ulifanya akafungwa gerezani na kukashifiwa kote duniani ameaga dunia kwa ugonjwa wa saratani akiwa na umri wa miaka 58.
Mary Kay Letourneau alipatikana na hatia ya mauaji ya daraja la pili ya kubaka mtoto mwaka 1997 baada ya kupata ujauzito na Vili Fualaau alipokuwa na umri wa 12 au 13 na yeye alikuwa na umri wa miaka 34.
Alijifungua mtoto wao wa pili akiwa gerezani 1998.
Baada ya kumaliza kifungo chake, wanandoa hao walioana 2005, hatahivyo, walitengana baada ya miaka 12.
Waliki wa Bi. Letourneau, David Gehrke ameviambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba Bi. Letourneau amekufa nyumbani kwake akiwa na watoto wake na Bwana Fualaau.
Bi. Letourneau alikuwa mama aliyeolewa na watoto wanne wanaoishi Seattle alipoanza uhusiano na mwanafunzi wake wa darasa la sita.
Awali, alihudumia kifungo cha miezi kadhaa tu gerezani lakini baada ya kuachiliwa huru alipatikana akifanya ngono tena na kijana huyo huyo mdogo.
Mama huyo aliyekuwa mwalimu alirejeshwa tena gerezani na kuhudumia kifungo cha miaka saba. Binti zake wawili aliopata na kijana Fualaau awali walitunzwa na familia ya mume wake.
Inasemekana kwamba mama huyo amekuwa mgonjwa kwa miezi sita kabla ya kutokea kwa kifo chake.
Mama huyo alikuwa mkatoliki na ni binti ya aliyekuwa mbunge wa Republican, John G. Schmitz. Lakini taaluma ya baba yake kisiasa ilifikia ukingoni baada ya kujitokeza kwa kashfa ya kwamba alikuwa na watoto wawili nje ya ndoa.09 July

Mama Sepetu Asakwa kwa Kuharibu Nyumba ya Serikali
MJANE wa aliyekuwa Makamu Jaji Mkuu wa Zanzibar, Jaji Mkusa Isaac Sepetu, Mama Salma Mkusa Sepetu, anasakwa na vyombo vya dola kwa tuhuma ya kuharibu vibaya nyumba ya Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) aliyokuwa akiishi na familia yake baada ya shirika hilo kumtaka ahame.

 

Imeelezwa kuwa baada ya mumewe kufariki alipewa notisi ya kuhama, lakini aliomba aachwe kwanza katika nyumba hiyo ambayo alidai kuwa walitumia gharama kubwa kuiremba na kuitia mapambo ya kila aina na kwamba hakuwa na deni.  Hata hivyo, ombi lake lilitupiliwa mbali.

 

Imeelezwa kwamba, mama huyo alitoa malalamiko akidai kwamba ZHC ilimtaka kuhama na kukabidhi funguo za nyumba waliyokuwa wakiishi na marehemu mume wake maeneo ya Michenzani Block namba 9/116.

 
09 July

Ilikuaje: Nilijikuta Kwenye Chumba Cha Kuhifadhi Maiti ilhali Sikuwa NimeagaLeo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa na Dennis Mwaura ambaye amepitia changamoto nyingi. Mwaura hakuzaliwa akitembea na vijiti vya kujisaidia ila aliumia alipokuwa anafanya mazoezi ya densi.

“Nimelelewa na nyanya yangu kwa maana wazazi wangu walitengana nikiwa mtoto mdogo, nilipokua nilianza kucheza nyimbo kanisani kama ‘b boy’ yaani kijana na kuonyesha ushupavu wake

Siku moja nikifanya mazoezi ya densi nilisikia uchungu kwa uti wa mgongo, nilienda nyumbani kesho yake nilienda kanisani lakini nilikuwa na uchungu mwingi

Nilitoka kanisani nikaenda nyumbani, niliomba Mungu anipe usingizi Mungu alisikia maombi yangu, nilipoamka nilikuwa najaribu kuchukua simu lakini mkono haukuwa unasonga

106580405_3009701509098941_7717603221806741100_n

Baada ya muda pia nilisongesha miguu lakini haikusonga, hapo ndipo nilijua nimepooza hata miguu.” Alieleza Mwaura.

Cha kushangaza ni kuwa baada ya kuamka haikuwa Jumapili bali alipomwambia rafiki yake amuonyeshe simu ni saa ngapi alipomuonyesha ilikuwa Alhamisi saa kumi na moja.

“Ni jambo ambalo liliniumiza sana, rafiki yangu aliyekuwa anavuta bangi aliambia jamaa zangu lakini hawakuchukulia kama ni jambo muhimu

Nilikaa kwa miezi mitatu kwa nyumba bila kupokea matibabu yoyote, baada ya kupelekwa hospitali nilikaa kwa miezi nane bila ya hata rafiki na jamaa kuja kunitembea

Hata mama yangu hakuja, mama yangu aliniacha tu hamna kitu chochote kilitokea kati yetu.” Alizungumza.

Kuna wakati Dennis Mwaura alijipata kwenye chumba cha maiti sababu ni ipi? hili hapa jibu

“Nilipokuwa kwenye wadi nilikuwa natetemeka sana nilikuwa nafungwa kichwa ili nisianguke, siku moja vile madaktari huwa wanakuja kubadilisha awamu usiku mmoja watu kumi waliaga kwenye wadi yangu

Huyo daktari alikuja na kuniuliza mimi ni nani kwa maana sikuwa na watu wa kunitembelea, aliniambia kuwa ni mimi nilikuwa natoa watu kafara

Baada ya hapo walileta wagonjwa wengine bali waliaga na usiku huo, siku iliyofuatia walileta wahubiri ili waje kuomba walinitoa nguo na kubaki na kaptura

Siku iliyofuatia madaktari walikuja kuita majina ya wagonjwa kila mmoja alikuwa hai isipokuwa mimi, walitayarisha kila kitu nikapelekwa kwa chumba kidogo cha kuifadhi maiti

Niliamka nijifunike blanketi nilijipata niko uchi kumbe nilikuwa kwa chumba cha kuifadhi maiti, nilipoamka na habari kufikia yule daktari alisema kwa kimombo ‘the devil has come again.”

Kwa mengi zaidi tembelea mtandao wetu wa kijamii wa youtube.

09 July

‘Asante Baba For The Top Up,’Zari Amshukuru Diamond kwa Kumnunulia Gari


Je, Diamond na Zari wamerudiana? Wawili hao wamekuwwa katika mahusiano mema hivi maajuzi  baada ya Diamond na Zari kukosana na msanii huyo kukataa kuwasaidia watoto wake kwa muda wa miaka miwili.

Mwanawe Zari aweka bayana uhusiano kati ya mamake na Diamond
Diamond alianza kuzungumza na wanawe na kisha kuwasaidia, baaada ya zari kupitia kwenye mitandao ya kijamii kusema kuwa hajakuwa akiwasaidia wanawe.

“TWO YEARS DOWN THE LINE DIAMOND REALISED WHAT HIS MISTAKE WAS WHERE HIS PROBLEM WAS AND HE SAID, HE IS NOT GONNA LET THIS CONTINUE AND HE DECIDED TO BE IN HIS KIDS’ LIFE. SO HE STEPPED UP, WHY CAN’T I GIVE CREDIT FOR THAT?” Aliandika Zari.

Siku ya kusherehekea kina baba duniani, Zari aliposti picha huku akimuonyesha Diamond mapenzi tele, awali kupitia kwenye mitandao ya kijamii Zari aliposti picha ambayo iliwaacha wengi wakizungumza na kuulizana maswali yasiyo na majibu.

Mama huyo wa watoto watano alimshukuru aliyekuwa mumewe huku wengi wakisema Diamond alimsaidia kununua gari hilo.

“ASANTE BABA T FOR THE TOP-UP.” Aliandika Zari.

Je, Diamond ndiye alimtumia pesa kununua gari hilo au mambo vipi?

09 July

Kocha Wa Simba Agomea Mastaa Wake Kupanda Lori

Kocha Wa Simba Agomea Mastaa Wake Kupanda Lori

Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck amegomea wachezaji wake kupanda gari la wazi lililoandaliwa maalum na uongozi wa klabu hiyo kwa lengo ka kutembeza kombe la ubingwa.

Simba iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere majira ya sa 2:40 asubuhi kisha kuendelea kukaa ndani mpaka pale walipoanza kutoka saa 9:18 asubuhi.
Kocha wa Simba ndiye aliyeanza kutoka nje ya vyumba vya uwanja huo na kuelekea upande yalipokuwa yamepaki magari ya mashabiki na gari maalum ambalo liliandaliwa kuwabeba wachezaji.

Kisha baada ya dakika moja akarudi tena ndani lakini wakati akiwa mlangoni akaonekana kuanza kuzozana na mwanadada Lispa Hatibu ambaye ni msaidizi wa ofisa Mtendaji mkuu wa Simba Senzo Mazingisa.

Mabishano hayo yalidumu kwa dakika moja kabla ya wahudumu wa uwanja na kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola kuwasihi waache ndipo Lispa alipoamua kuondoka kwa hasira huku akifoka.

Inadaiwa chanzo cha mzozo huo ni Sven kugoma wachezaji kupanda gari la wazi ambalo lilipangwa kupita katika barabara mbalimbali za Dar es Salaam mpaka makao makuu ya klabu hiyo Msimbazi huku yeye akitaka timu kwenda moja kwa moja kambini kujiandaa na mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga itakayofanyika Jumapili.