MTIHANI MZITO WA MAKIPA WAZAWA

KIPA wa Mashujaa FC, Patrick Munthali ndiye aliyekuwa kinara wa clean sheet akifikisha 12 kwa wazawa msimu uliopita Ligi Kuu Bara, ambapo amezungumzia ugumu wa kuifikia rekodi hiyo.

Munthali amesema alipata na majeraha, hivyo katika mechi sita dhidi ya Singida Black Stars, Pamba Jiji, Simba, KMC na Tanzania Prisons ndizo alipata cleansheets moja anayomiliki msimu huu.

“Mbali na majeraha ya hapa na pale yaliyonisumbua, wazawa tumekuwa na changamoto za mwendelezo ya viwango vyetu zipo sababu tofauti ukiondoa kuumia, tofauti na Simba, Yanga na Azam zinazokuwa na ubora wa juu, hivyo lazima anapatikana kipa namba moja,” alisema na kuongeza:

“Binafsi sioni kama nitazifikia hizo kutokana na hali halisi, angalau namuona Yona Amosi wa Pamba alimaliza na 11 na sasa ana tano naye si rahisi kwake, anahitaji mapambano ya kutosha.”

Kwa upande wa mshindani wake wa namba katika timu yao, Erick Johola ambaye ana clean sheet sita, Munthali alisema: “Kwa clean sheet alizonazo Johola huenda akafikia ingawa kucheza pia tunapishana, kuna wakati nacheza mimi, muda mwingine yeye.”

Yona Amosi wa Pamba Jiji alisema: “Bado ligi inaendelea sijui nitavuna kitu gani. Nikifikia sawa, nikiivunja na kuandika nyingine sawa na zisipofika pia sawa, jambo la msingi kuliko yote ni timu ifikie malengo.”

Kuhusiana na Yakoub Suleiman wa Simba, pia inaonekana kuwa na ugumu kwa upande wake baada ya kuumia na kuendelea kufanya mazoezi ya kujiweka fiti.

“Siyo jambo jepesi kwani nilipata changamoto ya majeraha na sasa naendelea na mazoezi ya ufiti, jambo la muhimu lilipo mbele yangu ni kurejesha ushindani kwenza,” alisema kipa huyo aliyemaliza msimu uliopita na clean sheet nane.

MSIMU WA 2024/25             

Msimu uliopita wa 2024/25, mzawa aliyekuwa anaongoza kwa clean sheet ni Munthali wa Mashujaa (12), alifuatiwa na Yona Amosi wa Pamba Jiji (11), Yakoub Suleiman akiwa JKT Tanzania (8), Chuma Mgeni wa Coastal Union (7), Metacha Mnata wa Singida Black Stars (7) na Zuberi Foba wa Azam (7). Ukiachana na wazawa, nafasi mbili za juu zilishikwa na makipa wa kigeni Moussa Camara wa Simba alikuwa na 19 na Djigui Diarra wa Yanga aliyemaliza na clean sheet 17.

MSIMU WA 2025/26

Ukiachana na kipa wa kigeni wa Yanga, Diarra kuongoza kwa clean sheet nane msimu huu, kinara kwa wazawa ni Johola mwenye sita sawa na Ally Salim wa Dodoma Jiji.

Kocha wa JKT Tanzania, Ahmad Ally alisema: “Kila mchezaji ana kitu chake kuhusu rekodi hizo, huenda wakazivunja ama kuzifikia kwani bado ligi inaendelea na chochote kinaweza kikatokea.”

The post MTIHANI MZITO WA MAKIPA WAZAWA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/bPR7YJD
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post