MAXIME MBEYA CITY NI SWALA LA MUDA TU

KOCHA wa Mbeya City, Mecky Maxime amewapa nguvu mashabiki wa timu hiyo huku akiwaambia kwamba bado anaamini kikosi hicho kitarudi kwenye ubora wake licha ya kupoteza mechi iliyopita.

Mbeya City ilikutana na Singida Black Stars na kupoteza mechi hiyo kwa kipigo kikali cha mabao 1-4, ikiwa ni mwenyeji na kuchezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa ulioko Babati mkoani Manyara.

Akizungumza na Soka la Bongo, Maxime alisema, ni kweli wameanza vibaya katika uwanja huo mpya, lakini mashabiki wasipoteze imani kwa sababu bado ni mapema.

“Kazi yangu itaanzia hapo kuhakikisha tunakuwa bora na kuongeza umakini wa kulinda ushindi kwa kuimarisha idara ya ulinzi, lakini pia kuongeza umakini kwa safu ya kiungo na ushambuliaji ili wachezaji waweze kutumia nafasi.

“Ukiangalia kwenye mchezo uliopita tulianza vizuri sana na hata kufanikiwa kuongoza, lakini baadaye tukafanya makosa ya kuruhusu mabao kirahisi.

“Lakini niwatoe hofu mashabiki wetu wa Mbeya City kwamba huu utakuwa mchezo wa mwisho kupoteza na wataiona timu yao ikirejea kwenye ubora,” alisema kocha huyo.

Mbeya City imepoteza mechi mbili mfululizo za hivi karibuni ikiwa nyumbani, huku ikiwa haina matokeo mazuri msimu huu katika Ligi Kuu Bara ikishika nafasi ya 14 kwenye msimamo ikikusanya pointi 13 ikicheza mechi 16.

Rekodi zinaonyesha, Mbeya City msimu huu imeshinda mechi tatu pekee za ligi, sare nne na kupoteza tisa.

The post MAXIME MBEYA CITY NI SWALA LA MUDA TU appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/2hIWTqy
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post