MCHAMBUZI wa Soka nchini Saleh Ally ‘Jembe’ amesema Msemaji wa Yanga Haji Manara anapaswa kupewa nafasi ya kusikilizwa lakini pia kama ikibainika ana makosa basi sheria ichukue mkondo wake.
Jembe ameyasema hayo katika kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na Global TV na Global Radio ambapo amesisitiza kuwa kwa namna ya uelewa wake ni kwamba Kamati ya Maadili haihukumu matusi bali inahukumu makosa kulingana na kanuni.
Amesisitiza pia watanzania waache kasumba ya kubambikiza makosa au kutetea makosa kwani mchezo wa mpira wa miguu unaendeshwa kwa sharia na kanuni ambazo zipo na zinaeleza wazi lakini pia kamati za maadili zipo na zinajua majukumu yake kwahiyo ziachwe zifanye kazi zake.
Jembe amesisitiza Kamati ya Maadili iachwe ifanye kazi yake juu ya sakata la Manara na Rais wa TFF Wallace Karia
“Mimi ushauri wangu ni kwamba iende kwa mujibu wa kanuni kama atapatikana na hatia baada ya kumsikiliza mi ningependa wamsikilize na nina amini wameshasema watamsikiliza, kwahiyo akisikilizwa basi watende haki na kama akibainika na hatia basi hatua staki zichukuliwe.” amesema Jembe
Jembe pia ametahadharisha wale wanaotumia fursa hiyo kumtetea au kumchonganisha Manara waiache Kamati ya Maadili ifanye kazi yake.
Aidha amesisitiza kuwa kitendo alichokifanya Manara dhidi ya Rais wa TFF hakihusiani na Klabu yake ya Yanga ambayo anafanyia kazi kwani hilo ni jambo ambalolinamhusu yeye binafsi.
Live video
ReplyDelete