Type something and hit enter

On

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba March 16, 2018 amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza taswira mbaya juu ya serikali badala yake kuwa na mitazamo chanya.

Ameyasema hayo katika kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum, Ester Mmasi.

Amesema wanafunzi hawatakiwi kufanya harakati ili wawe adui wa serikali kwani serikali yenyewe haina muda wa kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.

“Nilishawahi kufanya harakati nikiwa chuoni na nilipewa jina la Chifu, majina yangu yamekuja kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya ajenda za Taifa ambazo niliona hazina manufaa,” – Dk Mwigulu Mchemba.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment