RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA ATAKA HUITISWAJI WA MJADALA WA KITAIFA KUHUSU HALI YA ELIMU NCHINI - EDUSPORTSTZ

Latest

RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA ATAKA HUITISWAJI WA MJADALA WA KITAIFA KUHUSU HALI YA ELIMU NCHINI


Rais Mstaafu, Benjamin Mkap
DODOMA: Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesema ni muhimu kuitishwa mjadala wa kitaifa ili kujadili hali ya elimu nchini

Amefafanua kuwa ni lazima taifa litafakari kwanini shule za serikali zinaendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kila mwaka

Aidha, Mkapa ameshauri mjadala huo uhusishe makundi yote ya jamii wakiwemo wadau kutoka sekta binafsi, wasomi pamoja na wananchi wa kawaida ili kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo hilo

Mkapa ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ameyasema hayo wakati wa tukio la kumkaribisha Makamu Mkuu mpya wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Egid Mubofu na kumuaga aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo aliyemaliza muda wake, Profesa Idrisa Kikula.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz