TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO - EDUSPORTSTZ

Latest

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO

Mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowsky

Real Madrid imekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 29, kutoka Bayern Munich msimu ujao . (Mundo Deportivo - in Spanish)

Burnley iko tayari kuongeza mshahara wa kipa Nick Pope ili kuizuia Newcastle United kumnyatia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye ameitwa katika kikosi cha Uingereza kwa mara ya kwanza kwa sasa analipwa mshahara wa £15,000 kwa wiki hukoTurf Moor. (Sun)
Ashley Young, 32

Manchester United imeongeza kandarasi ya miezi 12 ya beki Ashley Young, 32, katika klabu hiyo hadi 2019. (Mail)

Takriban wachezaji 10 wa Manchester United katika kikosi cha kwanza akiwemo Michael Carrick, 36, anayestaafu na kiungo wa kati ambaye kandarasi yake imekwisha Marouane Fellaini, 30, pamoja na Zlatan Ibrahimovic, 36, huenda wakaondoka Old Trafford msimu huu (Express)

Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanaamini beki wa kushoto Luke Shaw, 22, ananyanyaswa na meneja Jose Mourinho baada ya kukosolewa pekee kufuatia ushindi wa mechi ya kombe la FA dhidi ya Brighton siku ya Jumamosi. (Telegraph)

Kiungo wa kati Nemanja Matic amesema kuwa viwango vya juu vya kocha Mourinho vinaweza kumfanya kuwa vigumu kufanya kazi naye lakini akaongeza kuwa anafurahia kucheza chini ya usimamizi wa raia huyo wa Ureno (Independent)

Kipa wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, 25, amemtaka mchezaji mwenza Andres Iniesta kusalia katika klabu hiyo .Kiungo huyo wa kati anaangazia uhamisho wa kucheza nchini China.. (Sky Sports)

Nahosha wa Paris Saint-Germain Thiago Silva anasema kuwa ana hakika kwamba mshambuliaji wa Brazil Neymar atasalia katika klabu hiyo, licha ya mchezaji huyo kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Real Madrid.(Canal+ via ESPN)Image captionNeymar

West Brom inataka mshambuliaji wa Numencia na Uhispania Guillermo, 24, kwa dau la £2m msimu ujao wakati ambapo klabu hiyo inakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja msimu ujao. (Sun)

Aliyekuwa beki wa Arsenal na Uingereza Sol Campbell anasema kuwa amefanyiwa mahojiano ya kuwa mkufunzi wa klabu ya Grimsby Town lakini akafurushwa na klabu hiyo ya daraja la pili kwa ukosefu wa uzoefu.. (Sky Sports)

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz