BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Showing posts with label UWANJA WA MASTAA. Show all posts
Showing posts with label UWANJA WA MASTAA. Show all posts

Thursday, 27 December 2018

27 December

Wasanii Matajiri Duniani 2018

Wasanii  Matajiri Duniani
Wasanii  Matajiri Duniani

Orodha ya  wasanii matajiri duniani inaendelea kubadilika kila mwaka.

Mamilioni ya watu yamzeidi kustaajabu kwa namna jinsi ya wasanii wa Hollywood na Broadway wanavyozidi kuwa kwenye orodha ya wasanii majatajiri duniani.

 Watu wengi ujiuliza ni msanii wapi waliokatika orodha hiyo: je msanii wako pendwa yupo katika orodha hiyo!? Hebu tuweke wazi kwa sasa.

Endelea kusoma ili kujua majina ya wasanii nyota duniani ambao wameweza kuingia kwenye orodha ya wasanii 10 tajiri duniani.

Mariah Carey
10. Mariah Carey: $ 510
Mamilioni ya mashabiki  Mariah Carey wanatambua kazi ya mwanadada huyu anayezidi kutamba katika orodha wasanii tajiri duniani. Ukiachana na kazi ya muziki mariah anamiliki perfume yake inayonuliwa na mamilioni ya watu duniani.

Jay-Z:
9. Jay-Z: $ 810 Milioni
Utajiri wa mwanamuziki Jay Z ulipanda kwa asilimia 30 mwaka jana na kufikisha utajiri wake hadi $810m (£626m), kwa mujibu wa jarida la Forbes.Lakini. Zaidi ya hayo, nembo yake ya biashara Rocawear na ndoa na Beyonce imemfanya kuwa tajiri sana.

Bono
8. Bono: $ milioni 600
 Huyu pia nimoja ya wasanii wanao miliki mkwanja mrefu duniani. Anamiliki utajiri wa zaidi ya dola  milioni 60. 
Msaini huyu ametamba kutokana brand yake ya U2  aliyokuwa maarufu na  kumpatia  faida kubwa. Pia amewekeza katika umiliki wa 5 star hoteli.

Celine Dion
7. Celine Dion: $ milioni 630
Kila mtu bila alitarajia kuona star huyu kuwa  katika jarida maarufu la Forbes juu ya wasanii matajiri duniani. 
Kibao chake kunachojulikana kwa jija "My Heart Will Go On" kinasemekana kuwa moja ya chanzo cha utajiri wake. 
Licha ya kutabiliwa kuporomoka katika orodha ya wasanii  matajiri  mwanadada huyo ameendelea kuwemo katika listi ya wasanii 10 matajiri duniani.

Diddy
Diddy: $750m (£579m).
Forbes waliandaa orodha yao wakizingatia mapato ya miaka ya nyuma pamoja na stakabadhi za kifedha, thamani ya mali inayomilikiwa na wanamuziki hao na pia kwa kuzungumza na wachanganuzi, mawakili, mameneja na wataalamu wengine katika tasnia ya muziki.

Dr.Dre:
5. Dr.Dre: $ 780 milioni
Msanii na rapa wa zamani wa NWA Dr Dre kwa sasa ana utajiri wa $780m baada ya kuuza Beats kwa Apple mwaka 2014 kwa $3bn (£2.3bn).

Baada ya kuuza Beats, alinunua jumba kubwa la kifahari Los Angeles la ukubwa wa futi 14,000 mraba kwa $40m (£31m).

Rapa ambaye pia ni mmiliki mwenza wa Cash Money Records Bryan "Birdman" Williams ana utajiri wa $110m (£85m
Headphones zake Beats By Dre zinasemekana kuwa moja ya bidhaa zake zinazozidi kumuweka juu.


Madonna
4. Madonna: $ milioni 800 
Madonna hawezi kuitwa Madonna kama yeye haijawahi kuingia katika orodha ya wasanii  tajiri duniani.Madona ni staa wa pop wa kwanza wa kike duniani kuwa bilionea. Madona katika safari yake ya maisha amewahi kuajiriwa katika mugahawa wa chakula.

Herb Alpert
3. Herb Alpert: $ 900 milioni
Herbert Alpert alizaliwa 31st March 1935, ni raia wa USA.Anaeleza kuwa alianza kujishughulisha na muziki akiwa na miaka 8.

Anautajiri wa Dollar Million 900 ambazo ni sawa na Tsh Trillion 2 na billion 7 na million 240.


Si kingine bali ni kipaji tu ndio kimemuweka hapo alipo.

Paul McCartney
2. Paul McCartney: $ bilioni 1.1
Paul McCartney ni msanii mwenye utajiri wa dola bilioni 1.2. Inasemekana utajiri wake umetokana na mauzo ya mashairi na tungo za mziki kwa wasinii wengine.

Andrew Lloyd Webber
1. Andrew Lloyd Webber: $ bilioni 1.2 
Huyu ndiye msanii anayemiliki mkwanja mrefu zaidi duniani kutokan a na kazi ya sanaa ya mziki. Utajiri wake umetokana na live show ambazo Zimemfanya kufahamika ulimwenguni.

 Kipaji na jitihada binafsi ni moja ya vigezo vilivyowafanya wasinii hawa kuwa kumiliki mkwanja mrefu na kuendelea kupendwa zaidi duniani.

Sunday, 16 September 2018

16 September

‛MPENZI′ WA DIAMOND HALI MBAYA KIAFYA


Hawa ilibainika kwamba ametopea katika ulevi wa pombe kali lakini alisaidiwa na kuacha
PICHANI:Hawa Hassan akiwa na Diamond katika picha ya video ya wimbo wa Nitarejea
 Nitarejea ni moja ya nyimboi ambazo zilitikisa vilivyo na kumtambulisha Zaidi mwanamuziuki Diamond Platnum ukiachilia vibao vingine kama Kamwambie na Mbagala.Wimbo huo uliokuwa kwenye mahadhi ya Zuku ulikutanisha vichwa matata viwili,Diamond na Hawa.

Ukiachilia mbali wimbo huo lakini pia stori kubwa ilikuwa ni mahusiano ya Diamond na Hawa,ikielezwa kwamba walikuwa wapenzi wa muda mrefu tangia kipindi Diamond akiwa anauza mitumba maeneo ya Tandale,hivyo watu walianza kuwatupia macho kwa karibu lakini ghafla penzi hilo lilikufaa Mwanadada Hawa kupotea masikioni na machoni mwa wapenda burudani.
Watangazaji Soud Brown na Kwisa wanaoendesha kipindi cha Shilawadu kupitia Clouds Tv waliwahi kumtembelea msanii huyo Hawa Hassan mara ya kwanza baada ya ripoti kuzagaa ya kwamba msanii huyo ametopea katika matumizi ya vilevi hasa pombe za kienyeji(Gongo ikiwemo) na kufanya naye mazungumzo ambapo msanii huyo alikiri kutumia Gongo.Baada ya mazungumzo hayo Hawa alipata msaada na kufanikiwa kuacha kabisa ulevi ikiwa ni pamoja na kuu nganishwa na Pilli Missana Sober House.

Lakini imeelezwa kwamba hali yake imekuwa mbaya tena na ikizidi baada ya kupata tatizo la Ini ikielezwa kwamba yawezekana ni kutokana na Ulevi.

Kupitia ukurasa wa Shilawadu,Soud Brown aliandika;
“Dah... Nimemtembelea Dada Yetu Msanii Hawa Kusema Kweli Hali Yake Mbaya, Tumbo Lake Kubwa Kama Ana Ujauzito wa Miezi 9 Kasoro, Ana tatzo la Ini, mwili unajaa maji na inabd mara kwa mara akatolewe Maji gharama ni kubwa mno kwa familia Yao”
Aliendelea kueleza tena;

“Hii ni mara ya Tatu Shilawadu Wanakutana Na Hawa, Mara Ya Kwanza Mwaka Jana Ambapo Tulimkuta Akiwa Amebobea Kwenye matumizi Ya Uraibu Aina Ya Gongo, Baada ya mazungumzo Hawa akakubaliana na sisi kuwa Yupo Tayari.Kuachana na Matumizi hayo tukamuunganisha na pillimissanah_sober_house  Akasaidiwa kuacha na akaacha kabisa, Bahati mbaya Baadae Ameanza kusumbuliwa na Ini (Huenda liliathiriwa na uraibu ule) Sasa Hv Hawa anaumwa Sana, Halali ucku Mbavu zinamuuma”
Katika taarifa yake hiyo kwa Umma wa Watanzania mtangazaji huyo alimalizia kwa kuandika; 

“Dada Pili Misana Pamoja na Familia Ya Hawa wanapambana ili kuinusuru Afya Ya Hawa, Watanzania, Wasanii Wenzake Na Wote mnaopata Taarifa hizi Tunawasihi na Tunajisihi Tumshike Mkono Hawa...  
Kutoa Ni Moyo Sio Utajiri, Namba Ya Mama a Hawa Ni +255 762 31 35 87Friday, 14 September 2018

14 September

OMMY DIMPOZ AMLILIA DIAMONDDiamond na Ommy Dimpoz waliwahi kuwa marafiki wa kutupwa kabla upepo haujabadilika
Pichani:Wasanii Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz
Jamii nzima ya wapenda burudani Tanzania na Afrika kwa ujumla WA nafahamu fika kwamba Jana,tarehe 13 ya Septemba ilikuwa siku maalumu mwa mwanamuziki KIPENZI cha watu Tanzania na Afrika Mashariki pamoja na watu wengine wote waliozaliwa siku kama hiyo Ulimwenguni.
Yawezekana kwa OMMY Dimpoz ILIKUWA ni siku ya FURAHA zaidi hasa kufuatia matatizo amabayo ameyapitia KIPINDI cha nyuma ambao aliugua kiasi kufika hatua ya kufanyiwa upasuaji wa koo Nchini Afrika Kusini,huku hali MBAYA ikimrudia wiki tatu zilizopita na kuamsha kazi ya ziada kwa watu mbalimbali kumuombea Uzima na AFYA.
Katika mahojiano aliyoyafanya na Millard Ayo,Ommy alieleza chanzo cha maradhi yake kuwa aliwekewa sumu kwenye chakula na mtu ambaye ALIKUWA na lengo la kumtoa roho.
Hayo wakati yanamkuta na kumfanya apitie mtihani mgumu kstika maisha yake watu wote wa sanaa waliwekeza nguvu zao huko kwa maombi na kumjulia hali Mara kwa mara.Lakini kitu cha ajabu ni kwamba aliyewahi kuwa rafiki yake kipenzi Diamond pamoja na meneja wake Mubenga hawakuwahi kumjulia hali hata siku moja.Moja ya Maneno aliyoyaongea OMMY alisema "kuumwa kwangu imekuwa ni ibada kwangu pia"
Katika siku yake hiyo ya kumbukumbu ya kuzaliwa ommy dimpoz aliandika kirefu ujumbe ufuatao;
ommydimpozLeo 13th September ni kumbukumbu yangu ya siku ya kuzaliwa. 

Namshukuru sana Mwenyezi Mungu (ALHAMDULILAAH) kwa kunipa nafasi ya kuuona mwaka mwingine, kwani niliyoyapitia katika kipindi cha takribani miezi 5 kama ingekuwa sio mapenzi yake yeye (M/Mungu) basi ingekuwa imebaki history. 
Nilichojifunza kipindi hichi chote ni kuwa kuumwa ni Ibada na sisi kama binadamu hatujakamilika leo unaweza kuwa mzima na kesho ukawa mahututi kitandani, ndio maana nimeamua kushare picha ambayo nilipigwa nikiwa ICU japo nafahamu sio kitu kizuri kupost picha kama hii kwenye mitandao ila nia yangu ni kujaribu kukumbushana sisi kama Binadamu kuwa kuna leo na kesho kwahiyo tusiishi kwa chuki na Uadui maana hatujui kesho yetu itakuwaje!! Kuna kipindi wakati nimelazwa nilikata tamaa ya kuishi nikaona labda muda wangu umekwisha lakini hapo Hospital akaletwa mgonjwa mwingine ambae alikuwa pembeni yangu alishambuliwa na majambazi kwa risasi tisa mwilini lakini madaktari wakafanikiwa kuokoa maisha yake na akapona so nikajiuliza mimi ni nani nikate tamaa ya kuishi na nikajifunza kwamba kuugua sio kufa, Ni vyema tukipata nafasi basi tuwaombee na kuwafariji wagonjwa kwani wanayoyapitia ni magumu mno. Kwasasa namshukuru Mwenyezi Mungu naendelea vizuri na bado niko kwenye recovering,

pia nawashukuru watu wote ambao mmekuwa mkiniombea dua nipone kwa haraka kuanzia mashabiki mpaka wasanii wenzangu na kila mtu aliyeniombea kwa imani yake Nashukuru sana. Mungu awabariki sana.
:
Pia Shukran za dhati kwa Familia yangu, Marafiki zangu wa Karibu, Management yangu ROCKSTAR FAMILY @officialalikibana my lovely Manager @sevenmoshaambaye amehangaika na mimi mfano wa Mama Mzazi na mtoto wake pamoja na my Big Brother Governor @joho_001 ambaye ameniuguza kwa kipindi hichi chote chini ya uangalizi wake na Madaktari kuanzia Kenya Mpaka South Africa.
ASANTENI SANA NA INSHAALLAAH KWA UWEZO WA ALLAAH I WILL COME BACK STRONGER 💪🏽🙏❤
14 September

DIAMOND KUTIMIZA AHADI NA IRENE UWOYA


Pichani:Mwanamuziki Diamond Platnumz kushoto na mwanamitindo Irene Uwoya kulia
Kile kitendawili ambacho kimetegwa huenda punde kikapata jibu bila ya hata mtegaji kupewa mji ili atupatie jibu.Na kwa hakika hii italeta faraja kubwa sana na furaha kwa wapenda burudani na familia kwa ujumla kwani mpaka sasa imeonekana kuwa tatizo kwa Msanii huyo
Ukiachilia mbali skendo inayomuandama kwa sasa kuhusiana na uwepo wa fununu ya kwamba ameendewa kwa sangoma ili afungwe na kutulizwa mzuka na sangoma kunakodaiwa kutekelezwa na mlimbwende,video vixen na mwanamitindo Hamisa Mobetto,skendo ya kutoonyesha upendo wowote kwa OMMY DIMPOZ,Msanii Diamond Platnumz amedhamiria kufanya jambo hili.

September 6 kulizuka sintofahamu baada ya mwanamuziki staa kutoka kiwanda cha BURUDANI Tanzania na mkali wa kibao cha #jibebe Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram kupost picha ya mwanadada mkali kunako kiwanda cha filamu na mitindo hapa bongo Irene UWOYA.
Sio kawaida kabisa kwa diamond kutumia ukurasa zake za mitandao ya kijamii kupost watu ambao hana malengo nao,na inaaminika ya kwamba ukiona hivo basi JUA kuna jambo.
Kupitia mitandao mbalimbali ikiwepo you tube kumekuwa na ripoti kwamba kuna uwezekano mkubwa ndoa ya Dogo Hanna na Irene Uwoya UKAWA inevunjika hasa baada ya Irene Uwoya kusafiri peke yake kuelekea Dubai ambao haijafahamika rasmi naenda kufanya nini na ndicho kipindi ambacho Diamond ambaye ni CEO wa WCB Company alipompost na kuzua mjadala.WENGI wanaamini ya kwamba Diamond anaweza kumuoa Irene Uwoya hasa kutoka na na kuonekana anajielewa sana tofauti na WANAWAKE wengine kadhaa ambao Diamond KATIKA nao kimapenzi ukimuondoa Zari.

Pichani:Hamisa Mobetto,Diamond Platnumz na Zarina Hassan

Lakini moja kati ya mambo ambayo yameanza kujitokeza ni kwamba tayari Irene kashapewa shavu kupitia WAsafi Tv kuhost project ya shindano ka Niko Jibebe ambao inefahamika kwamba atakuwa Jaji mkuu.
Pamoja na mwanamuziki mkali kutoka A-town anayetamba na kibao cha #banana Dogo Janja kuelezea kutokuwa na wasiwasi na mkewe na kwamba anamuamini huku akisisitiza kwamba kamwacha mkewe aende ughaibuni peke yake kwani hawawezi fuatana KILA mahali lakini bado kuna zusha maswali hata kuonekana ukaribu Wao INSTAGRAM ukiwa unepungua.

Watu wanaendelea kusubiri Kuona ahadi ya Diamond aliyoitoa MWEZI February,2018 kwa Mama yake na mashabiki wake kwamba lazima AKE mwaka huu kufuatia kuachana na Zari KATIKA hali ya kutatanisha,bado ni kitendawili,nani atamuoa kati ya WANAWAKE watatu wa mwanzo Wema  Sepetu,Hamisa Mobetto aliyezaa nae mtoto MMOJA na Zari AMBAYE NAPATA naye Watoto wawili huku akiongezeka Irene Uwoya.

TAFADHALI NINI MAONI YAKO,NANI ANAMFAA DIAMOND KATI YA WANAWAKE WANNE HAPO JUU?.Saturday, 2 June 2018

02 June

DIAMOND PLATNUMZ REKODI MPYA YOUTUBE


Mwanamuziki anaefanya vema katika kiwanda cha bongo fleva diamond platnumz amekuwa akiiwakilisha vyema tanzania kwenye suala ya rekodi mbalimbali.

Diamond platnumz amekuwa akiweka rekodi mbalimbali kupitia mtandao wa youtube kwenye video zake mbalimbali.

Hivi karibuni channel yake ilikuwa miongoni mwa channel zenye subscribers millioni moja.

Lakini jana aliweza kutoa video yake ya pili kutoka kwenye album yake ya Aboy from tandale inayokwenda kwa jina la IYENA ikiwa imetanguliwa na African beauty

Iyena aliyomshirikisha Rayvany imefikisha watazamaji milion moja(M1) ndani ya masaa 19 tu toka video ilipoweka youtube

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Friday, 1 June 2018

01 June

HATMA NA MAAMUZI YA HAKIMU KUHUSU KESI YA HALIMA MDEE

Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee 

HATMA NA MAAMUZI YA HAKIMU KUHUSU KEZI YA HALIMA MDEE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa ahirisho la mwisho katika kesi  inamyomkabili mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli

Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambaye leo ametoa ahirisho hilo la mwisho kwa upande wa mashtaka baada ya wakili wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita kudai kesi ilipangwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, hawana shahidi ikiwa ni mara ya tatu.

Hakimu Simba amepanga kesi hiyo kusikilizwa tena Juni 29, 2018 kwa mashahidi wa upande wa mashtaka kuanza kutoa ushahidi.

Mdee anadaiwa kufanya kosa hilo Julai 3, 2017 Makao Makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni ambapo anadaiwa kutoa lugha ya matusi kwa Rais Maguifuli kwa kusema "anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Friday, 25 May 2018

25 May

ZARI AWEKA WAZI HISIA ZAKE KWA IVAN DON

Pichani; zari na marehemu don wakiwa na familia yao
Ikiwa mwaka mmoja sasa umepita tangu kifo cha alikuwa mume wa zarithebosslady na moja ya watu waliounda kundi la rich gang ivan don.

Kupitia ukurasa wake wa instagram zari ameweza kuweka hisia zake na kusema kwamba hii wiki itakuwa na kwa ajili ya kumuenzi ivan kwa kumkumbuka yale ambayo walishea wote wakiwa pamoja.

zari ambae aliweza kupata watoto watatu wa kiume na ivan kabla ya kukutana na diamond ambae pia amemzalia watoto wawili na kufanya jumla ya watoto watano.

zari amesema kuachana nae hakumfanyi asimkumbuke kwani hakuna ubaya wowote aliufanya kwake na bado ataendelea kuwa kwenye kumbukumbu ya maisha yake kwani walifanikiwa kuwa wote katika maisha.
25 May

ALICHOKISHAURI NAPE LEO BUNGENI KWA MAWAZIRI WA JPM

 Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye, amewataka Mawaziri katika serikali ya awamu ya tano kuwa na tabia ya kusikiliza ushauri na kukubali kukosolewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye,

Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye, amewataka Mawaziri katika serikali ya awamu ya tano kuwa na tabia ya kusikiliza ushauri na kukubali kukosolewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.


Nape amesema hayo leo Mei 25, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, wakati wa kuchangia hoja mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na kuwataka Mawaziri hao kuiga mfano wa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu wake kwani ni watu ambao wanakubali kupokea ushauri.

“Wito wangu kwa Mawaziri wengine igeni mfano wa Kalemani, ukiambiwa jambo usilolipenda, wewe ni kiongozi kubali, sikiliza, mimi naamini Kalemani atakwenda vizuri, zipo changamoto kwenye Wizara yako, lakini ninaamini ukiendelea kuwa msikivu yale ambayo yapo juu ya uwezo wako mimi najua watu watakusamehe, lakini yale ambayo yapo ndani ya uwezo wako ukisikiliza na ukayatekeleza tutakuunga mkono” amesema Nape.

Mbunge huyo aliendelea kumwaga sifa kwa Waziri Kalemani kwa kufanikiwa kuiunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara katika Gridi ya Taifa pamoja na kupeleka Meneja wa TANESCO katika Mkoa wa Lindi.

Kwa upande mwingine Nape ameishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuligawa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi kwa kutenganisha majukumu ya uzalishaji na usambazaji na kutaka serikali kuingia ubia na sekta binafsi ili umeme uzalishwe katika kiwango kikubwa.

CREDIT TO EATV

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Tuesday, 22 May 2018

22 May

MASHARTI ALIYOYATOA BABA WA MAREHEMU KANUMBA KWA LULU

Baba Kanumba alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake mkoani Shinyanga, ikiwa ni siku chache baada ya mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa kujitokeza hadharani na kuoneshwa kutofurahishwa na kitendo cha Lulu kubadilishiwa adhabu kutoka kifungo cha miaka miwili jela hadi kifungo cha nje.
Elizabeth Michael ( LULU)

MUNGU ametenda! Ndiyo maneno ya kwanza kutoka kinywani kwa baba wa aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Steven Charles Kanumba, Charles Kusekwa Kanumba mara baada ya kuanza mahojiano huku akieleza alivyofurahishwa na kitendo cha aliyekuwa mpenzi wa mwanaye, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kutolewa gerezani na kumpa masharti mazito mwanadada huyo.

Baba Kanumba alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake mkoani Shinyanga, ikiwa ni siku chache baada ya mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa kujitokeza hadharani na kuoneshwa kutofurahishwa na kitendo cha Lulu kubadilishiwa adhabu kutoka kifungo cha miaka miwili jela hadi kifungo cha nje.

HANA TATIZO NA MTU

Tofauti na mama Kanumba ambaye alionesha kutaka Lulu abaki gerezani, baba Kanumba alisema kuwa, kutolewa kwa mrembo huyo ni mpango wa Mungu.

HUYU HAPA BABA KANUMBA

Baba Kanumba alisema kuwa, kwanza Lulu kutolewa gerezani na kubadilishiwa kifungo cha nje ni mpango wa Mungu na alifurahishwa mno na kutoka kwake hivyo kwenye moyo wake hana kinyongo naye hata kidogo.

“Kila kitu hapa duniani hupangwa na Mungu na kila kinachotokea ni mapenzi yake, siwezi kulaumu kwa nini Lulu ametoka bali nimefurahi kwa sababu hata angefungwa miaka mia moja, Kanumba tayari alishafariki dunia, hawezi kurudi duniani.

MCHA MUNGU

“Silaumu kwa sababu mimi ni mcha Mungu hivyo Mungu ndiye amesema suala hilo lifikie tamati kwa namna hiyo, wanaopinga na kusema siyo haki, hayo ni mawazo yao maana kama ni kifo cha mwanangu kiliniuma sana, lakini sasa siwezi kumlazimisha Mungu afanye mimi binadamu ninavyotaka maana hata neno lake linatufundisha kwamba tusamehe,” alisema baba Kanumba.

AMPA MASHARTI MAZITO

Pamoja na kufurahishwa na suala la Lulu kutolewa gerezani na kupewa kifungo cha nje, baba Kanumba alimpa Lulu masharti mazito kwamba kama anataka maisha yake yaende vizuri, awe na familia nzuri kama watu wengine na amani moyoni, anatakiwa kwenda kufanya usafi kaburi la Kanumba kama ni kulia, alie na hapo atakuwa ameacha balaa na mikosi yote.

“Kwa mila za kabila letu la Kisukuma ni kwamba, Lulu alitambulika kama mke wa Kanumba maana hakuna mwanamke mwingine tunayemfahamu sisi hivyo natamani angeachiwa huru kabisa asiwe na kifungo cha nje na aende tu kufagilia kaburi la mumewe Kanumba na hapo atakuwa amemaliza na kuwa huru.

“Lulu kama anataka awe na familia, yaani aolewe, apate watoto wazuri na amani katika maisha yake, aende tu kufagilia kaburi la Kanumba na hapo atakuwa ameacha kila nuksi, balaa na mikosi hapohapo na atakuwa huru kabisa, ndiyo mila zetu zinavyosema,” alisema baba huyo.

ASIPOFANYA ITAKUWAJE?

Baba huyo aliendelea kueleza kuwa, endapo Lulu hatafuata na kufanya masharti hayo, basi atakuwa na wakati mgumu mno kwenye maisha yake kwa maana damu hiyo na mzimu wa Kanumba utakuwa ukimfuatilia na anaweza asiolewe au kupata familia, yaani watoto.

“Kinachotakiwa hapa, Lulu anatakiwa afuate tu hayo masharti ya kimila niliyompa, lakini asipofanya hivyo atajikuta akikosa amani katika maisha yake kwani kufanya hivyo kunamuepusha na kufuatiliwa na ule mzimu au damu ya Kanumba ambayo itamtesa na kujikuta akikosa furaha na amani,” alisema baba Kanumba.

MTU WA KARIBU ANENA

Mmoja wa watu wa karibu na familia ya Lulu ambaye aliomba hifadhi ya jina, alipotakiwa kuzungumzia masharti hayo ya baba Kanumba, alisema kuwa, familia imeyapokea na yanatekelezeka.“Kikubwa kwanza familia inamshukuru Mungu kwa kitendo cha kubadilishiwa adhabu ya gerezani na kumalizia kifungo chake cha nje.

“Unajua jambo lenyewe kama alivyosema baba Kanumba ni mipango ya Mungu tu. Familia haikutegemea kabisa kama Lulu anaweza kubadilishiwa adhabu.

“Unajua kama familia, baada ya hukumu ya miaka miwili kutolewa na Mahakama Kuu, Novemba, mwaka jana, licha ya kumuombea Lulu atoke, lakini kibinadamu tulikuwa tunajua ndiyo mpaka amalize miaka yake miwili gerezani ndiyo atoke,” alisema mtu huyo na kuongeza:

“Lilipokuja lile la msamaha wa Rais, nalo familia iliona tu ni kama Mungu anasikiliza maombi na kumpunguzia ile robo ya kifungo, lakini hakuna aliyekuwa anajua kwamba Lulu anaweza kutoka mapema hivi akiwa angali na miezi sita tu gerezani.”

MITANDAONI KWACHAFUKA


Mara baada ya Lulu kubadilishiwa kifungo hicho, mitandaoni kulichafuka kwa watu kumzungumzia mrembo huyo huku wengi wakionesha kufurahishwa na kitendo hicho.“Ni jambo la kheri sana. Lulu anapaswa kumshukuru Mungu kwa sababu sidhani kama alitegemea kama siku moja anaweza kutoka katika mazingira kama yale,” alichangia mdau mtandaoni.

Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii walisema kuwa, Lulu ni binti ambaye alikuwa ana msaada mkubwa katika familia yake hususan mama yake mzazi hivyo kitendo cha yeye kurudi uraiani kinaleta faraja kubwa.

Walisema kama mzazi, kitendo cha kutomuona mwanaye kwa muda mrefu kilikuwa kinampa mawazo na hivyo sasa ni wakati wa kuanza ukurasa mpya wa maisha ya furaha.

TUJIKUMBUSHE

Mwishoni mwa mwaka 2017, Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam ilimuhukumu Lulu kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake, Kanumba, lakini Mei, mwaka huu mahakama hiyo ilimbadilishia adhabu na kumpa kifungo cha nje ambapo amekuwa akifanya kazi za kijamii kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar.

MCHANGANUO ULIVYOKUWA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Magereza, mfungwa yeyote (isipokuwa wa kunyongwa na kufungwa maisha) anapoingia tu gerezani anapata msamaha wa theluthi moja ya kifungo chake.

Hivyo Lulu alipoingia tu gerezani, alipata msamaha huo ambapo alipunguziwa theluthi hiyo na kubakiwa na miezi 16 badala ya ile 24 aliyohukumiwa mahakamani.

RAIS AMUOKOA

Baadaye, Rais Dk John Pombe Magufuli kupitia msamaha alioutoa Aprili 26, mwaka huu jijini Dodoma katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar aliwapunguzia wafungwa mbalimbali nchini robo ya vifungo vyao ambapo Lulu naye alinufaika na msamaha huo.

Hivyo kutoka kwenye miezi 16 iliyobaki, Lulu akabakiwa na miezi 12. Baadaye, Mahakama Kuu kupitia vipengele vya sheria, iliweza kumbadilishia kifungo Lulu baada ya kutumikia nusu ya kifungo chake yaani miezi 6.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. 

Monday, 21 May 2018

21 May

JE SUGU ANATAKIWA KUOMBWA MSAMAHA? MAJIBU YAKE HAYA HAPA

 Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amedai kwamba anatakiwa kuombwa msamaha kutokana na hukumu aliyopewa ya kutumikia kifungo jela bila sababu za msingi.
Joseph Mbilinyi

Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amedai kwamba anatakiwa kuombwa msamaha kutokana na hukumu aliyopewa ya kutumikia kifungo jela bila sababu za msingi.

Sugu amesema hayo leo Mei 21, 2018 katika viwanja vya Bunge Jijini, Dodoma ikiwa ni kikao chake cha kwanza cha bunge kuhudhria tangu ameachiwa huru baada ya kuhudumu kwa siku 73 katika Gereza la Ruanda, Mbeya, ameongeza kwamba bila kujali ni nani amempa msamaha lakini anastahili kuombwa msamaha kwa hukumu aliyopewa.

“Mimi naamini sikutakiwa kuwa ndani, na unapozungumzia suala la msamaha nabaki najiuliza, napewaje msamaha na mtu ambaye amekufunga, mtu ambaye wanasema ulimfedhehesha, kitu cha msingi sio nani kanipa msamaha, mimi siamini kana nastahili kupewa msamaha bali natakiwa kuombwa msamaha kwa kufungwa kiholela na kutoka kiholela” amesema Sugu.

Mbunge huyo ameongeza kuwa wafungwa pamoja na askari katika Gereza la Ruanda walishangaa kumuona mbunge huyo katika Gereza hilo, Sugu amesema “wafungwa na askari walinipokea vizuri, kwanza walishtuka sana kuona Mbunge ameletwa kwa kesi ambayo haileweki kwahiyo nilikuwa na kazi kama kiongozi ya kuwatuliza”  

February 26, 2018 Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya iliwatia hatiani Sugu na Emmanuel Masonga Katibu wa CHADEMA nyanda za juu kusini na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, lakini wawili hao waliachiwa huru Mei 10, 2018 kwa msamaha wa Rais Magufuli alioutangaza katika sherehe za sikukuu ya Muungano April 26, 2018.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ
21 May

WATAMBUE WALIOFUKUZWA CHADEMA LEO

  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama watatu wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa ni usaliti ndani ya chama.
chedama yawafukuza uanachama watatu leo, may 21

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama watatu wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa ni usaliti ndani ya chama.

Monday, 14 May 2018

14 May

SABABU ZILIZOFANYA JESHI LA MAGEREZA KUMUACHILIA LULU

Jeshi la Magereza limeeleza kuwa muigizaji Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ameachiliwa Mei 12, 2018 kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuenda kutumikia kifungo chake nje ya gereza 'community service'
Jeshi la Magereza limeeleza kuwa muigizaji Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ameachiliwa Mei 12, 2018 kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuenda kutumikia kifungo chake nje ya gereza 'community service'
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam na kusema kwa mujibu wa Sheria ya Magereza Sura ya 58 kifungu Na. 49 (1),(2)(3) mfungwa yeyote (isipokuwa mfungwa wa kunyongwa na wa maisha) mara baada ya kupokelewa gerezani hupata msamaha wa theluthi ya kifungo chake 1/3 ambapo Lulu alipata msamaha huo na alitakiwa kuachiwa huru Marchi 12, 2019.

Aidha, taarifa hiyo iliendelea kufafanua baadhi ya mambo kuwa katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Rais Magufuli kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa msamaha wa robo ya adhabu kwa wafungwa wote waliokuwa na sifa za kunufaika na msamaha huo.

"Kufuatia msamaha huo mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael naye alinufaika na msamaha huo na hivyo kutakiwa kutoka gerezani Novemba 12, 2018", imesema taarifa hiyo

Pamoja na hayo, taarifa hiyo imeendelea kwa kusema "kwa mujibu wa Sheria Na. 3 (2)(a) cha Sheria ya Huduma kwa Jamii ya mwaka 2002 wafungwa ambao vifungo vyao havizidi miaka mitatu hunufaika na utaratibu huo ambao unampa fursa mfungwa kutumikia kifungo chake nje ya gereza kwa kufanya shughuli au kazi zisizo na malipo kwa manufaa ya jamii. Mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, kutokana na kukidhi vigezo vya kisheria na kuonesha tabia njema akiwa gerezani amenufaika na utaratibu huo".


Muigizaji Elizabeth Michael alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mnamo Novemba 2017, kwa kosa la kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake Steven Kanumba.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Friday, 11 May 2018

Wednesday, 9 May 2018

09 May

TRUMP ATANGAZA RASMI KUACHANA NA MKATABA WA NYUKLIA WA IRAQ

Rais Donald Trump wa Marekani

Rais Donald Trump ametangaza kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa Nyuklia wa Iran. Ameuita mpango huo kuwa umeoza na ni kero kwa raia wote wa Marekani.

Amesema mpango huo hauwezi kuleta amani hata kama Iran ikikubaliana na kila kitu kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo uliosainiwa mwaka 2015 chini ya utawala wa aliyekuwa rais taifa hilo Barack Obama.

Rais wa Iran amekosoa hatua ya Marekani kujitoa na kudai kuwa haiheshimu makubaliano yake. Akienda kinyume na mataifa ya Ulaya yaliyofikia makubaliano hayo,Trump amesema kuwa watarejhesha vikwazo vya kiuchumi vilivyoondolewa dhidi ya Iran kupitia makubaliano hayo ya mwaka 2015.

Israel na Saudi Arabia kwa pamoja wamepongeza.Viwazo vya vinatarajiwa kuanza dhidi ya Iran ndani miezi mitatu hadi mitatu.

Trump awali alilalamikia mkataba huo kwamba ulikuwa unaiwekea Iran vikwazo kwa muda tu na kwamba ilishindwa kusitisha mpango wake wa makombora na kwamba Iran ilipewa kiasi cha dola bilioni 100 kwaajili ya kutokomeza silaha na ugaidi huko mashariki mwa kati.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ

Tuesday, 1 May 2018

01 May

WAFAHAMU WATU 12 WALIOWAHI KUFIKA KWENYE MWEZI
Mtu wa mwisho kutembea kwenye Mwezi, Gene Cernan, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

Alikuwa kamanda wa chombo cha safari za anga za juu cha Apollo 17 mwaka 1972 na miongoni mwa watu watatu waliofika mwezini mara mbili.

Lakini kuna watu wengine 11 waliomtangulia kufika na kuukanyaga Mwezi. Ni nani hao?


Neil Armstrong (1930 - 2012) na Edwin 'Buzz' Aldrin (alizaliwa 1930)


Armstrong ni maarufu sana kwa maneno yake baada ya kuwa mtu wa kwanza kuukanyaga Mwezi: "Hatua moja ndogo kwa mwanamume mmoja, hatua moja kubwa kwa binadamu."

Buzz Aldrin alimfuata.


Wakiwa kwenye Mwezi, Neil na Buzz waliweka bendera ya Marekani na kuacha bango lililokuwa na ujumbe, "Hapa, wanaume kutoka sayari ya Dunia walikanyaga Mwezi kwa mara ya kwanza Julai 1969, AD (Baada ya Kuzaliwa kwa Yesu). Tulifika sote hapa kwa amani kwa niaba ya binadamu wote."

Charles 'Pete' Conrad (1930 - 1999)


Apollo 12 ilipaa angani kukiwa na tufani na radi, hali iliyosababisha nguvu za umeme kuzimika muda mfupi baada yao kuruka angani.

Conrad mwishowe alipoukanyaga Mwezi, alisema kwa sauti: "Whoopee! Bwana, hiyo huenda ilikuwa hatua ndogo kwa Neil, lakini kwangu imekuwa kubwa sana."

Alan L Bean (alizaliwa 1932)


Bean ni msanii pekee ambaye amewahi kusafiri nje ya sayari ya dunia.

Michoro na picha zake kwa hivyo zina uhalisia fulani kuhusu hali ilivyo kwenye Mwezi.

Alan Shepard (1923 - 1998)


Shepard anakumbukwa kwa kupiga mipira kadha ya gofu kwenye Mwezi akitumia kipande kidogo cha chuma.

Kutokana na kiwango cha chini cha nguvu mvutano (graviti), mipira hiyo ilikwenda mbali sana kuliko inavyowezekana kwenye Dunia.

Edgar D Mitchell (1930 - 2016)


Mitchell alikuwa binadamu wa kwanza kupeperusha picha za runinga za rangi kutoka kwenye Mwezi. Alibeba pia jiwe la uzani wa kilo 43.5 kutoka mwezini pamoja na mchanga na akarejea navyo duniani.

David Scott (alizaliwa 1932)


Scott ni maarufu sana kutokana na stempu zake.

Bila idhini ya Nasa, alisafiri na stempu za posta hadi mwezini akiwa na mpango wa kuziuza baada ya kurejea nazo duniani. Hakusafiri anga za juu tena.

James B Irwin (1930 - 1991)


Irwin alipokuwa safarini, maafisa ardhini waligundua alikuwa akikabiliwa na matatizo ya moyo.

Lakini kwa sababu alikuwa akipumua oksijeni asilimia 100 na nguvu mvuto huko kwenye Mwezi zilikuwa chini, waliamua hakuwa hatarini.

Mpigo wa moyo wake ulirejea kawaida aliporudi duniani.

Hata hivyo, alifariki kutokana na mshtuko wa moyo miezi kadha baadaye.


John Young (alizaliwa 1930)


John Young ndiye mwana anga aliyehudumu muda mrefu zaidi katika historia ya Nasa, kufikia sasa.

Wakati mmoja, aliingia na kipande cha mkate kilichotiwa mboga kwenye chombo cha anga za juu safarini.

Wakuu wa Nasa hawakufurahishwa na hilo. Lakini Young aliendelea na kazi na alisafiri anga za juu mara sita.

Charles M Duke Jr (alizaliwa 1935)


Duke aliweka historia alipougua surua wakati wa mafunzo ya wahudumu wa ziada wa Apollo 13.

Aliwaweka hatarini wahudumu na kulazimisha mmoja wa wana anga kubadilishwa.

Harrison 'Jack' Schmitt (alizaliwa 1935)


Schmitt alikuwa mwanasayansi wa kwanza kwenda anga za juu.

Alikuwa kwenye Apollo 17 na alikaa siku tatu kwenye Mwezi akiwa na Gene Cernan.

Alirusha nyundo pekee waliyobeba mbali na pia aliacha vifaa vyake vya kupimia kwenye Mwezi.

Saturday, 28 April 2018

28 April

HII NDIO TASWIRA YA YANGA SIKU MOJA KABLA YA MCHEZO WAKE NA SIMBANi siku moja pekee ambayo ni leo Jumamosi imesalia kuelekea mechi kubwa ya vigogo wa katika soka la Tanzania Simba na Yanga watakaokutana kwenye Uwanja wa Taifa kesho Jumapili.

Simba na Yanga zinakutana kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara zikiwa na kumbukumbu ya kwenda sare ya bao 1-1 kwenye mechi ya raundi ya kwanza.

Yanga inaenda kuchuana na Simba ikiwa mgeni huku ikiwa haina uhakika wa kuwatuma baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa hawana hali nzuri kiafya tangu msimu huu wa 2017/18 uanze.

Wachezaji hao ni Donald Ngoma na Amis Tambwe ambao wamekosekana kwenye mechi lukuki kutokana na kuandamwa na majeruhi.

Ingawa uongozi wa Yanga umekuwa ukitangaza kuwa wachezaji hao kuwa wako fiti kila inapotokea wanakuwa na mechi, wamekuwa wakishindwa kuonekana Uwanjani sababu ya majeruhi kuwaandama.

Mbali na wawili hao, Ibrahim Ajibu, Andrew Vincent na Kelvin Yondani ndiyo waliorejea kikosini baada ya kupatwa na majeruhi siku kadhaa zilizopita.

Urejeo wa wachezaji hao unaleta manufaa kwa kikosi cha Yanga ambacho kimetawaliwa na vijana wengi kwa msimu huu baada ya wakongwe baadhi kuonekana kwa nadra Uwanjani kwa sababu tajwa hapo juu.

Credit to sarehejembe


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
28 April

BADNEWS- HII HAPA TAARIFA YA KIFO CHA MH ABAS KANDORO


Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro 

TANZIA: Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro amefariki dunia usiku huu wa Ijumaa, Aprili 27, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibu.

Kabla ya hapo, Kandorro alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kabla ya kustaafu utumishi wake, Kandoro alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kabla ya kumwachia Amos Makalla.

Aidha, Abbas Kandoro aliwahi kushika nafasi ya ukuu wa mikoa katika zaidi ya mikoa sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Singida na Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ameandika;EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Friday, 27 April 2018

27 April

MKUTANO WA KIM JONG NA RAIS WA KOREA KUSINI MOON JAE-IN WALETA FARAJA


Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amekutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kwenye eneo la mstari wa kijeshi uliowekwa kuyagawa mataifa hayo mawili tangu vita vya Korea mwaka 1953.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN, limemnukuu msemaji wa Rais Korea Kusini, Yoon Young-chan, akisema kuwa kikao hicho cha viongozi hao wawili kimedumu kwa dakika 100.


Yoon ameongeza kuwa mkutano huo ambao unaajenda kuu tatu utaangazia masuala ya nchi hizo mbili ikiwemo silaha za nyuklia na kuboresha mahusiano, na kutafuta makazi ya amani rasmi.

Mwishoni mwa mwezi March mwaka huu Kim Jong-un alifanya ziara nchini China na kukutana na Rais Xi Jinping mjini Beijing. Hiyo ilikuwa ziara yake ya kwanza kufanya nje ya taifa lake la Korea Kaskazini.

Ujumbe aliouandika Kim Jong-un kwenye kitabu cha wageni

Kim Jong-un akisaini kitabu cha wageni wakati Rais Moon Jae-in akiwa amesimama pembeni yake.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ