WATAMBUE WALIOFUKUZWA CHADEMA LEO - EDUSPORTSTZ

Latest

WATAMBUE WALIOFUKUZWA CHADEMA LEO

  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama watatu wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa ni usaliti ndani ya chama.
chedama yawafukuza uanachama watatu leo, may 21

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama watatu wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa ni usaliti ndani ya chama.

Waliofutwa uanachama ni pamoja na aliyekua Naibu Katibu Mkuu Bara, Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro, Dickson Kibona. 
Akizungumza leo Mei 21, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha, Ole Sosopi amesema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kufuata taratibu zote za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa.

Amesema viongozi hao wamehojiwa baada ya kuwepo tuhuma za usaliti ambazo ni kosa kwenye chama hicho, Sosopi amesema Bavicha imeridhia kuwaondoa wanachama hao baada ya kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz