PICHA ZA WANYAMA ZILIZOPENDWA NA KUCHEKESHA MWAKA 2013 - EDUSPORTSTZ

Latest

PICHA ZA WANYAMA ZILIZOPENDWA NA KUCHEKESHA MWAKA 2013




Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za kuchekesha na kusisimua za wanyama zilizopigwa mwaka huu, miongoni mwa picha hizi ikiwa moja ya dubu wanaoonekana kukoleza uhusiano wao pamoja na nyingine ya sili.


Picha hizi ziliteuliwa kushindania tuzo za picha za ucheshi za wanyama mwaka huu, katika vitengo vitano.

Jumla ya picha 3,500 ziliwasilishwa kwa mashindano hayo.

Shindano hili huandaliwa kuchangisha pesa na kusaidia shirika la kutetea uhifadhi wa wanyama la Wakfu wa Born Free.Picha hii ya Tibor Kercz ilipewa kichwa 'Nisaidie'

Mshindi wa jumla Tibor Kercz kwa picha hii yake ya bundi anayeonekana kuhitaji usaidizi kujishikilia vyema kwenye tawi mti alitunukiwa kikombe ambacho kilitengenezwa na wanaume na wanawake wenye ulemavu kutoka Tanzania.

Kadhalika, alipewa vifaa zaidi vya kupigia picha.

Alishinda pia tuzo kwenye kitengo cha picha ya kuvutia zaidi ya mtandaoni pamoja na kujishindia safari ya kwenda mbugani Kenya.

Kabla ya picha hii ya Andrea Zampatti kushinda kitengo cha picha za ardhini, picha hii yake ya panya anayeonekana kuangua kicheko ilisambazwa sana mitandao ya kijamii mapema mwaka huu.Raha mustarehe!

Na ingawa bahari ni kubwa, picha hii iliyoshinda kitengo cha picha za chini ya bahari inaonesha viumbe wanaweza bado kukaribiana sana.Picha hii ilipewa kichwa 'kofi'

Kitengo cha picha za angani, picha hii ya njiwa mmoja wao akionekana kufuata njia ya moshi wa ndege, iliyopigwa na John Threlfal Preston, Lancashire ndiyo iliyoshinda.

Hapa chini ni baadhi ya picha nyingine zilizofanya vyema.Twende kanisaniKunani?NibebeHaki miliki ya pichaJEAN-JACQUES ALCALAY/ BARCROFT IMAGESMapenzi tele
Eti nini!?



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz