Mwanamke katika jimbo la Hawaii, Marekani huenda amepata parachichi kubwa zaidi duniani, taarifa zinasema.Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
"Lilikuwa kubwa kama kichwa changu," aliambia gazeti la West Hawaii Today.
Bi Wang amewasilisha ombi rasmi kwa Guinness World Records kutaka litambuliwe kama parachichi kubwa zaidi kuwahi kupatikana duniani.
Mwaka 2009 parachichi la kilo 2.18 (4.8lb) kutoka Venezuela lilitambuliwa rasmi kuwa kubwa zaidi duniani.
Bi Wang anasema tunda hilo lilitoka kwa mparachichi wa zaidi ya miaka 40 ambao umekuwa karibu na barabara
Jimbo la Hawaii, tunda ambalo linatoka kwa tawi lililoning'inia barabarani au linaloanguka barabarani linaweza kuchukuliwa na mtu yeyote yule na liwe lake.
Amewasilisha picha za tunda hilo kwa West Hawaii Today.
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @workmanalice
Bw Wang anatarajia kupata majibu kutoka kwa Guinness katika kipindi cha miezi miwili.
Anasema baada ya kulipima walilila tunda hilo kubwa na marafiki zake.
"Lilikuwa tamu sana. Mti huo ni mzuri sana. Tulikuwa watu 10 na hatukumaliza nusu ya parachichi hilo," anasema.
No comments:
Post a Comment