Mwamba haendi popote, yupo sana tu Jangwani - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwamba haendi popote, yupo sana tu Jangwani

Mwamba haendi popote, yupo sana tu Jangwani

Usikose kuitazama mechi ya ligi kuu tz bara ni YANGA vs COASTAL UNION bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii LIVE bure kwenye simu bofya sasa kuidownload

Umesikia huko @soccer_laduma wameripoti kuwa Wakala wa mchezaji wa Young Africans, Aziz Ki anayefahamika kwa jina la @zambro_sport_management_ Traore amekiri kusikia taarifa za mchezaji wake kuhusishwa kuhitajika na timu kadhaa za Afrika Kusini kama vile Orlando Pirates,Mamelodi sundowns na Kaizer Chiefs.

Lakini kupitia mahojiano aliyoyafanya na kituo hicho cha #Afrika kusini Bwana Zambro amethibitisha kuwa hakuna mawasiliano rasmi yoyote ambayo yamefanyika au taarifa yoyote rasmi mezani kwake kuhusu kuhitajika kwa huduma ya kijana wake ambaye anafanya vyema na wananchi nchini Tanzania kutoka kwenye klabu hizo.

Siku kadhaa kulikuwa na taarifa kuwa Zambro yupo nchini Tanzania kujadili ofa ya mkataba mpya kutoka yangasc ambapo Aziz Ki anawatumikia kwani mkataba wake unamalizika mapema Mwishoni mwa msimu huu.

Bado Young Africans nao hawajatoa taarifa yoyote kuhusu Mkataba mpya kwa nyota huyo kwenye vyombo vya habari kama wamefikia makubaliano ya kuongeza au bado hawajafikia.

Ingawa Wananchi walishaweka wazi kuwa hawapo tayari kumpoteza mchezaji yeyote muhimu kwao.


Je, Aziz ki ataendelea kusalia kwa Wananchi au atatimka mwishoni mwa msimu?Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz