Masau Bwire: JKT tumecheza kama Mamelodi, Mungu amewaokoa Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Masau Bwire: JKT tumecheza kama Mamelodi, Mungu amewaokoa Yanga

Masau Bwire.

Usikose kuitazama mechi ya ligi kuu tz bara ni YANGA vs COASTAL UNION bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii LIVE bure kwenye simu bofya sasa kuidownload

Ofisa Habari wa Klabu ya JKT Tanzania, Masau Bwire amesema kuwa sare waliyoipata Klabu ya Yanga dhidi ya wajeshi hao ni Mungu tu ndiyo amewaokoa, vinginevyo Wananchi wangefungwa bao nyingi.

Masau amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi kati ya JKT dhidi ya Yanga uliopigwa katika Dimba la Meja jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu.

"Matokeo haya yametuhuzunisha sana JKT Tanzania, hayakuwa matarijio yetu sisi kupata alama moja kwa Yanga lengo letu ilikuwa kupata alama zote tatu tulifanya maandalizi na ubora wa kikosi chetu ulikuwa wa hali ya juu sana, nadhani kila mmoja ameona ni nini kilichotokea.

“Lakini wakati wewe unapambana, unaonesha ubora Mwenyezi Mungu naye ana la kwake. Mungu amewaokoa sana Yanga siku ya leo (jana), na huko wanakokwenda wanamshukuru sana Mungu kwa sababu amewaokoa.


“Nadhani ndio sababu jana (juzi) walifurahi sana mechi ilipoahirishwa kuchezwa kwa sababu walijua kama wangecheza tungewafunga hata magoli manne. Huu ndio ubora wa JKT Tanzania. Kama watu wameiona ni kama Mamelodi Sundown walivyocheza pale kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa," amesema Masau Bwire.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz