ALICHOKIANDIKA TUNDU LISSU KUHUSU HUKUMU YA SUGU KISHERIA - EDUSPORTSTZ

Latest

ALICHOKIANDIKA TUNDU LISSU KUHUSU HUKUMU YA SUGU KISHERIA

Kupita ukurasa wa Instagram mh tundulissu mbuge tiketi ya chadema ameyaandika haya kuhusu hukumu ya sugu na mwenzake inayohusu kumkashifu Rais Jpm.
Waheshimiwa wangu salaam kutoka Ubelgiji. Nawapeni pole nyingi kwa yaliyomkuta Mh. Sugu na Goddie Masonga siku ya leo.

Naomba kuzungumzia suala hili kwa kirefu kidogo. .

Kwanza, hukumu ya leo sio mwisho wa mjadala mahakamani. Bado kuna fursa, nay haki, ya rufaa High Court na, ikibidi, Court of Appeal.

Pili, hukumu ya leo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote huo. Kuna haki ya dhamana pending appeal. Ndivyo ambavyo tumefanya kwa viongozi na wanachama wetu wengi in the past. .

Tatu, hukumu ya leo haina athari yoyote kwa ubunge wa Sugu. Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi, na kwa makosa ya 'utovu wa uaminifu.' Uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu. .

Nne, pamoja na kwamba sijaona nakala ya hukumu, adhabu ya kifungo bila faini kwa kosa la kwanza ni kinyume na sentencing principles. Hii ni mojawapo ya hoja zetu zilizoshinda katika kesi ya Mh. Juakali High Court mwaka jana. .

Tano, hata kama atakaa gerezani muda wote huo, hukumu za kesi za kisiasa kama hii hazijawahi kuwapunguzia heshima wapigania haki popote pale duniani. .

On the contrary, kifungo cha aina hii ni beji ya heshima kwa kila mpigania haki na uhuru. Orodha ya mifano ni ndefu sana: Nyerere (ijapokuwa yeye alilipa faini), Kenyatta, Mandela, Mugabe, Fidel Castro, etc. .

Alichokifanya hakimu leo ni kuwaongeza Sugu na Masonga kwenye orodha hii ya heshima. They'll come out even bigger and stronger than when they went in. .

Sita, naunga mkono pendekezo la Mh. Zitto kwamba wabunge wetu wote warekodi maneno aliyofungiwa nayo Sugu na kuyaweka mitandaoni ili watukamate na sisi pia. .

Instead of agonising, let's organise and make this issue bigger and bigger mpaka wakimbie wenyewe au watukamate na kutufunga wote. .

Na sio wabunge tu, tuhamasishe kila mwanachama wetu na kila anayechukizwa na uonevu huu ayarudie maneno haya ili nao wakamatwe na kufungwa. .

Tumlazimishe Magufuli na watu wake waamue: waigeuze nchi nzima kuwa gereza moja kubwa, au akubali kusemwa kwa maneno na lugha asiyoipenda. Hiyo ndio maana pekee ya freedom of speech in a democracy. .

Nawatakieni kila la kheri katika hii safari ndefu ya kuelekea kwenye haki.


  EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz