MTENDAJI KATA YA BUKANDWE AJILIPUA KWA AJILI YA WANANCHI - EDUSPORTSTZ

Latest

MTENDAJI KATA YA BUKANDWE AJILIPUA KWA AJILI YA WANANCHI

Rais JPM kushoto na kulia kwake ni Mtendaji wa kata ya Bukandwe, mkoani Gaita Mh, Muberwa Bakalemwa
Mtendaji wa Kata ya Bukandwe Wilaya ya Mbogwe mkoa wa Geita, Muberwa Bakalemwa ni miongoni mwa Viongozi vijana ambao wamekua mstari Wa mbele kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa rika na watu wote katika jamii. Mtendaji huyo amekua mbele kuitendea kazi kauli mbiu ya rais magufuri ya HAPA KAZI TU kutoka na jukumu zimaalilojipa katika kuhakikisha anaboresha na kuinua elimu katika kata ya Bukandwe pia ikiwa ni sehemu ya kuunga jitihada za Mh JPM katika harakati ya kuijenga Tanzania ya viwanda.

Mtendaji Wa kata ya Bukandwe Mh Muberwa Bakalemwa akishirikiana na wananchi katika ujenzi Wa darasa

Mh, Muberwa akiwa ni moja ya viongozi shujaa na makini, ameamua kujitoa kwa dhati katika kuhakikisha wananchi wa kata ya Bukandwe na viunga vyake  wanafaidika na rasilimali walizonazo na kuhakikisha anaweka mikakati itakayo andaa rasilimali watu watakao ijenga Tanzania ya viwanda.

Kupitia jitihada zake, mh Muberwa, ameweza kutambua umuhimu elimu na kuweka jitihada na mipango thabiti  kuhakikisha kila mwanafunzi anasoma katika mazingira salama na rafiki hususani katika uboreshaji na ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye maeneo yenye kero zaidi.

Mnaomo mwezi January mwaka huu, wananchi wa bukandwe wakiongozwa na viongoji wao wakata na vijiji na vitongoji waliweza kujitolea kwa dhati na kufanikisha uchimbaji wa misingi miwili ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Bukandwe.

Hawakuishia hapo, tarehe 8 na 9 mwezi huu (march), wananchi Wa Bukandwe wakiongozwa na shujaa wao Mh Muberwa, walianza ujenzi wa misingi ya majengo hayo ili kuhakikisha wanapunguza huaba wa madarasa waliyokua nayo.
Mtendaji wa kata Mh Muberwa (kushoto) akishirikiana na wananchi kuchanganya mchanga kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa shule Bukandwe

Mtendaji akiwa mstari wa mbele katika ujenzi wa msingi wa shule ya msingi Bukandwe
 Akiongea na Edusportstz Leo, Muberwa amesema haya!

"Kwanza ningependa kushukuru wananchi pamoja na viongozi wenzangu Wa taifa, mkoa, wilaya, kata, vijiji na vitongoji kwa ushirikiana wanaonipa katika safari yangu ya kuhakikisha tunaijenga Bukandwe na kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wote"

"Katika kata ya bukanydwe, tunaupungufu wa vyumba vya madarasa 6, Lakini tumeridhia ifikapo mwezi wa 12 tuwetumefikia malengo tuliyojiwekea"

"Mpaka sasa, tumeanza na ujenzi wa vymba 4 ikiwa majengo mawili, yaani kila jengo litakua na ofisi moja na darasa moja"

"Pia tunamikakati ya kujenga mabweni mawili katika shule ya sekondari ya Kanengee na zahanati mbili za Bukandwe na Nhungwiza"

Mh, Muberwa amehitimisha kwa kusema kuwa anaomba viongozi, watu binafsi na wananchi kwa ujumla kumuunga mkono kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa majengo hayo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz