DAVIDO ADONDOKA AKIPANDA JUKWAANI KUTUMBUIZA - EDUSPORTSTZ

Latest

DAVIDO ADONDOKA AKIPANDA JUKWAANI KUTUMBUIZAMsanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido amejikuta akipoteza mzuka baada ya kujikwaa wakati akipanda kwa mbwembwe jukwaani tayari kwa kutumbuiza nchini Rwanda.

Davido ambaye alikuwa anaonekana kama tayari ameshapata ulabu ilimchukua sekunde kama 30 kukaa kimya jukwaani akivalishwa tena phone masikioni ambazo zilikatika alipojikwaa wakati akipanda jukwaani.

Hata hivyo, baada ya ajali hiyo ndogo Davido aliendelea kutumbuiza ambapo maelfu ya watu walihudhuria kwenye show hiyo ambayo ipo kwenye ziara ya Davido ijulikanayo kwa jina la “30 billion africa tour 2018” iliyofanyika kwenye uwanja wa mpira wa taifa wa Amahoro.

Akiwa nchini Rwanda, Davido ametoa msaada wa dola $5,000 sawa na Tsh milioni 11.2 kwenye shule ya muziki nchini Rwanda
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz