BREAKING: Simba wampa "Thank You" Kocha Benchikha - EDUSPORTSTZ

Latest

BREAKING: Simba wampa "Thank You" Kocha Benchikha

Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha

Kudadeki ni Namungo vs Simba ligi kuu tz bara unaanzaje kukosa kuitazama mechi hii live buree kabisa bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live buree bofya sasa

Klabu ya Simba imetangaza rasmi kuachana na Kocha wake Mualgeria Abdelhak Benchikha baada ya miezi mitano tu tangu ajiunge na Wekundu hao wa Msimbazi.

Simba inaachana na Benchika siku moja tu tangu Mualgeria huyo aiwezeshe kutwaa Kombe la Muungano kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jana usiku Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.

Aliwasili mwishoni mwa mwezi Novemba akasaini mkataba wa miaka miwili Novemba 28 kabla ya kuiwezesha timu kufika Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambako ilitolewa na mabingwa watetezi, Al Ahly.

Lakini Simba ikatolewa katika Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ya ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup kwa penalti 6-5 na wenyeji, Mashujaa kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.


Na kwenye Ligi Kuu hadi sasa Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 za mechi 21, nyuma ya Azam FC yenye pointi 54 na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 62 baada ya timu zote kucheza mechi 24.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz