Kikwete ahoji ishu ya Pacome kudaiwa kufungiwa na FIFA, ukweli ni huu - EDUSPORTSTZ

Latest

Kikwete ahoji ishu ya Pacome kudaiwa kufungiwa na FIFA, ukweli ni huu

Pacome Zouzoua.

Kudadeki ni Yanga vs Tabora united kombe la crdb bank federation cup unaanzaje kukosa kuitazama mechi hii live buree kabisa bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live buree bofya sasa

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amefunguka kuhusu madai kuwa mchezaji wa timu hiyo, Pacome Zouzoua raia wa Ivory Coast amefungiwa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA kutokana na jina lake kutokuwemo kwenye mfumo wa usajili (TMS).

Taarifa hizo zilianza kusambaa weekend iliyopita huku zikidai kuwa kufungiwa kwa mchezaji huyo ndiko kumewafanya Yanga kushindwa kumtumia na badala yake kusingizia kuwa ni mgonjwa.

Akijibu kuhusu madai hayo, Eng. Hersi amesema taarifa hizo ni za kizushi na kipuuzi hivyo zinatakiwa kupuuzwa kwani mchezaji huyo aliumia kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Azam Fc na amekuwa nje kwa mwezi mzima sasa akijiuguza lakini kwa sasa hali yake imeimarika na anaweza kurejea uwanjani muda wowote mwalimu akimhitaji.

“Ukiwa kiongozi lazima ukubali kuwa na ngozi ngumu la sivyo unaweza kujinyonga. Mishale yote inakuja kwa viongozi, sisi ndiyo wahanga wa haya mambo.

“Jana nimetumiwa mpaka na mzee wangu Jakaya Kikwete “Vipi kuhusu ishu ya Pacome, kuna nini”? Yani imetengenezwa stori ya ajabu ya uongouongo na mimi nilijua labda kwa watu wa kawaida lakini mpaka mzee wangu akaniuliza kuna jambo gani hapa.

“Kuhusu Pacome kwamba hachezi kwa sababu kuna kesi FIFA, sijui Yanga asimtumie atakatwa pointi, ni vitu vua kipuuzi hata kukijadili haina maana. Sijui kafungiwa, sijui kuna ishu ya CAF sijui FIFA mara hana kibali cha kukaa nchini ni upuuzi tu.


“Pacome ana kibali cha kukaa nchini, amepata leseni ya TFF, amepata leseni ya CAF, kacheza mashindano yote ya CAF, kacheza Ligi, kaumia na baada ya kuumia ameitwa Timu ya Taifa. Hili lilikuwa jambo muhimu kwake kuitwa timu ya Taifa ya Ivory Coast, hawa ndiyo mabingwa wa Afrika na wana wachezaji kila sehemu duniani.

“Pacome alivyoitwa akiwa injury tulikubaliana aende ili ku-maintain position yake. Aliitwa Ijumaa na anatakiwa kuripoti Ufaransa Jumatatu. Serikali yetu kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, ile VISA licha ya ugumu wake kupatikana lakini ilitoka ndani ya siku moja na Jumatatu asubuhi akaondoka kwa ajili ya kulinda heshima ya klabu yetu,” amesema Eng. Hersi.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz