Aziz Ki: Malengo yangu ni ubingwa kwanza, mengine baadaye - EDUSPORTSTZ

Latest

Aziz Ki: Malengo yangu ni ubingwa kwanza, mengine baadaye

Aziz Ki: Malengo yangu ni ubingwa kwanza

Ni leo YANGA vs COASTAL UNION usikose kuitazama mechi hii live buree kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live buree kabisa

Kiungo wa Klabu ya Young Africans, Stephane Aziz Ki, amebainisha kwamba, malengo yake ya kwanza msimu huu ni kuona anaisidia timu yake hiyo kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

Aziz Ki ambaye ndiye kinara wa magoli katika ligi hiyo msimu huu akifunga 15, amesema baada ya lengo la kwanza kutimia, ndipo atafikiria Tuzo ya Ufungaji Bora.

“Lengo langu namba moja msimu huu ni kubeba ubingwa na sio kutwaa Kiatu cha Ufungaji Bora, ishu ya ufungaji bora itakuja baada ya kushinda ubingwa,” alisema Aziz Ki.

Aziz Ki ambaye huu ni msimu wa pili akiitumikia Young Africans, amehusika kwenye jumla ya magoli 22 kati ya 54 yalifungwa na timu yetu katika ligi, amefunga 15 na asisti 7.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz