;
SOMA ALICHOPOST LAZARO NYALANDU HUKU AKITOA ANGALIZO - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 23 February 2018

SOMA ALICHOPOST LAZARO NYALANDU HUKU AKITOA ANGALIZOAliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mhe Lazaro Nyalandu amejikuta akipata wakati mgumu kuuaminisha umma kuwa jina linalotumika mitandaoni kutangaza safari ya kwenda Israel sio lake, hii ni baada ya Watanzania wengi kuomba nafasi baada ya tangazo la kwenda kuzuru nchini huko kutangazwa mtandaoni

Mhe Nyalandu amesema kuwa akaunti hiyo ya Facebook ambayo inatumia jina lake, sio yake hivyo watu wote waliojaza fomu na kumpatia namba mtu huyo wasiendelee kufanya hivyo kwani ni tapeli wa mitandaoni.

“Fake News alert❗Habari hii ya kupeleka watu Israel sio ya kweli na Account iliyotumika kuandika sio yangu. Tafadhali ipuuzeni. So many sad people out there wanaokaa kutungia wenzao UONGO. Sad!,”ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuutarifu umma na kuweka tangazo hilo.

Tayari zaidi ya watu 400 wameshaomba kwenda kuzuru nchini Israeli baada ya tangazo hilo kuwekwa na mtu huyo anayejiita Lazaro Nyalandu.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB