Taifa Stars kushindwa kupata ushindi vs Angola COSAFA 2017 - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 28 June 2017

Taifa Stars kushindwa kupata ushindi vs Angola COSAFA 2017

Michuano ya COSAFA 2017 bado inaendelea nchini Afrika Kusini kwa michezo ya Kundi A kuchezwa, Kundi A lenye timu za Tanzania, Angola, Mauritius na Malawi kwa michezo yao ya pili imechezwa leo.

Tanzania leo imcheza dhidi ya Angola wakati Malawi ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Tanzania kwa magoli 2-0, imecheza dhidi ya Mauritius ambayo ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Angola, staa wa Tanzania Mzamiru Yassin ndio ameibuka kuwa mchezaji bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola.

Game za leo Tanzania ilicheza dhidi ya Angola na kulazimishwa sare tasa wakati game ya Malawi na Mauritius imemalizika kwa sare tasa pia hivyo Tanzania bado anaendelea kuongoza Kundi A kwa kuwa na point nne sawa na Angola ila anaongoza kwa tofauti ya magoli, michuano hii ya COSAFA 2017 timu vinara wa makundi ndio watafuzu kucheza robo fainali.

No comments:

Post a Comment