Inaelezwa kuwa, Klabu ya Azam ikitaka kumuuza Feitoto kwa Simba ni lazima waipe Yanga kiasi cha pesa shilingi bilioni moja.
Akizungumza kwa code kwenye Sport Arena, maalamu wa za ndaani Ricardo Momo, amesema wanaomtaka Fei hawawezi kutoa hiyo pesa zaidi watasubiri amalize mkataba
"Kuna mchezaji tumemwona hapa,alikuwa kwa mpinzani katoka kwa mpinzani kaenda kwa team kubwa ya tatu katika nchi yetu.
"Sasa kuna tetesi watu wamezivumisha kuwa anaweza akaenda kwa wapinzani wengine si alikuwa kwa wapinzani, wale wazee wa Dabi, alikuwa upande mmoja kwa wazee wa Dabi na mpaka kuondoka kwake kulikuwa kwa kishindo mpaka ikabidi watu waingilie kati e bwana kaeni mzungumze ili mambo yaishe
"Sasa hizi za ndaani kabisa, mkataba wa yule mchezaji wa mauziano baina ya yule giant mmoja ambae alikuwepo mchezaji na huyu giant wa tatu. Endapo wakitaka kumuuza kwenye Klabu ya humu ndani basi wao wanatakiwa wapate kiasi cha shilingi bilioni moja.
"Giant wa kwanza si huyu alikuwa mchezaji wake, ikatokea tafrani wakamuuza sasa kipengele walichowekewa hao waliyomnunua. Hata mauziano yao hayakuwa kwenye bei waloyoitaka wao kwasbaabu waliamviwa kaeni muyamalize.
"Unajua kuna mtu akitoa kauli hiyo haihitaji chochote yaani mtafanya haraka haraka ilimradi shughuli iishe yaani hiyo hata kama ingekuwa jero kwa buku jero ilimradi shughuli iishe
"Mnamchukua kwa miaka mitatu, ndani ya miaka mitatu ikitokea mnataka kumuuza huyo mchezaji basi asiuzwe ndani ya hii nchi na ikitokea mtamuuza basi sisi tutadai bilioni. Tena hiyo bilioni yenyewe ndani ya mkataba wake na hiyo Klabu yake mpya
"Hapa kuna timu inapambana na team mbili hata kwenye maswala ya ku attack, hii ndio inatakiwa sana na hata kwenye kufungwa unaambiwa wakifungwa na hawa haiumi kama wakifungwa na hao."
No comments:
Post a Comment