Pacha wa Pacome' aliyetajwa Simba aomba kusepa ASEC - EDUSPORTSTZ

Latest

Pacha wa Pacome' aliyetajwa Simba aomba kusepa ASEC

Serge Pokou

Baada ya kugawa dozi nzito mnyama simba kesho anakipiga dhidi ya wakata miwa kagera sugar usikose kuitazama mechi hii ya kibabe live bure kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live buree kabisa unafeli wapi au unaogopa nini bofya sasa na kama hutaipenda hii app we ifute tu ila najua uitaipenda kwasababu ina mambo mengi matamu

Kiungo mshambuliaji wa Asec Mimosas, Serge Pokou ameomba rasmi kuondoka klabuni hapo huku akihusishwa na Simba inayoelezwa inampigia hesabu kali.

Fundi huyo wa mguu wa kushoto ambaye aliwahi kuifunga Simba hapa nchini wakati timu hizo zilipokutana Ligi ya Mabingwa alisema ingawa ana ofa nyingi lakini amevutiwa na ofa ya Tanzania.

“Nina ofa nyingi ikiwemo moja ya hapo Tanzania, lakini bado sijajua wapi nitakwenda ingawa napenda kuja kufanya kazi Tanzania, kuna marafiki zangu hapo wananiambia namna ligi ya huko ilivyo na ushindani,” alisema Pokou.

“Nimewaomba viongozi wa klabu wasiniwekee ngumu katika kuondoka, nafahamu hii ni timu ambayo inapenda kuuza wachezaji wake Ulaya, napenda kwenda huko lakini nani anajua ni lini ofa kama hiyo itakuja?”

Wakati Pokou akiyasema hayo, kocha wake Jullie Chevalier alisema kiungo huyo uamuzi wa kuondoka kwake unategemea na uongozi wa klabu yao endapo timu inayomtaka itawafuata kwa kuwa bado amesalia na mwaka mmoja.


“Serge (Pokou) ni mchezaji mzuri, nadhani kama atataka kuondoka itategemea na ofa ambayo itakuja kwa uongozi wa klabu, kwa kuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja hapa, ingawa sijawahi kuona viongozi wanazuia mchezaji akitaka kuondoka,” alisema ChevalierDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz