Baada ya Simba SC kushinda dhidi ya Azam FC, Young Africans SC wanahitaji pointi (3) pekee badala ya (5) za awali kutwaa Ubingwa wa (30) wa ligi kuu Tanzania bara bila kujali matokeo ya timu zingine.
Simba akishinda mechi zote (5) zilizobaki atafikisha points (71). Azam FC akishinda mechi zake zote (4) atafikisha points (69). Yanga akishinda dhidi ya Mtibwa mechi inayofuata atafikisha pointi (71).
Kwa mujibu wa kanuni mpya timu zikilingana points wanaangalia head to head hivyo automatically Yanga anakuwa bingwa kwa sababu kamfunga Simba home and away (1-5) & (2-1) kwa Aggregate ya (7-2) hata idadi ya mabao, Yanga anatofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa ikilinganisha na Simba.
Yanga anamzidi Simba takribani mabao 20 ambayo si rahisi kuyafikia ndani ya mechi chache zilizobaki.
Msimu huu unaweza kusema ni kama Simba imeizawadia ubingwa Yanga kwa kuipa alama zote Sita na bao 7. Simba KuIfunga Azam ni njia nyingine ya kuisogezea Ubingwa Yanga. Hivyo Simba imechangia pakubwa sana kwenye kumpa ubingwa mtani wake Yanga msimu huu.
Kwa kifupi ni kwamba Yanga SC wakishinda dhidi ya Mtibwa Mei 13 wanatwaa Ubingwa wa (3) mfululizo wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa na viporo vitatu mkononi.
Mechi za kufunga msimu Ligi Kuu | Mei
Young Africans SC:
◉ 13 - Mtibwa » Ugenini.
◉ 22 - Dodoma Jiji » Ugenini.
◉ 25 - Tabora United » Nyumbani.
◉ 28 - Prisons » Nyumbani.
Azam Football Club:
◉ 12 - KMC » Ugenini
◉ 20 - JKT Tanzania.
No comments:
Post a Comment