Kwa mujibu wa almachiuskanyasi Klabu ya Young Sports Club ilikwishaanza Mazungumzo ya kuwaongezea Kandarasi baadhi inatamatika na wanahitajika klabuni Wachezaji hao ambao Mikataba yao.
Farid Mussa - Ni kweli mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu ila mpaka muda huu hakuna mazungimumzo yoyote yaliyoanza.
Zawadi Mauya - Kweli mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu ila imefahamika kuwa Klabu ya Yanga haina Mpango wa kuendelea kuwa nae.
Denis Nkane - Mwisho wa Msimu huu atakuwa Mchezaji huru na imefahamika kuwa klab yake ya Yanga haina Mpango nae tena.
Nickson Kibabage - Yes ameshaongeza mkataba mpya wa Miaka 3 baada ya ule wa Mkopo kutamatika.
Clement Mzize - Mkataba wake na Young Africans ulikuwa unaelekea ukingoni ila tayari ameshaongeza kandarasi ya miaka 2.
Makudubela Skudu - Ameshataarifiwa kuwa klab ya Yanga hakina Mpango nae kuelekea Msimu ujao.
Kibwana Shomari - Kweli Mkataba wake na Yanga unaelekea ukingoni ila Mazungumzo ya Mkataba mpya yameanza na klab yake licha ya kuwa tayari ana ofa 3 mkononi mwake.
Bakar Mwamnyeto - Mazungumzo ya mkataba mpya yameanza na muelekeo wake mzuri, tayari alikuwa na ofa za vilabu viwili vikimuhitaji.
Joyce Lomalisa - Ni kweli Mkataba wake unaelekea tamati na hakuna mazungumzo yoyote ya kuongeza kandarasi Mpya mpaka muda huu.
Metacha Mnata - Kandarasi yake na Klabu ya Yanga inaelekea mwishoni kabisa ila bado hakuna mazungumzo ya mkataba mpya.
Pacome Zouzoua - Ni kweli amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja ila klabu yake imepanga kumuongezea miaka miwili zaidi.
Aziz Ki - Mkataba wake ukiwa ukingoni taarifa za ndani ya uongozi wa Yanga zinadai alishaongeza kandarasi na waajiri wake ambao ni Yanga.
Kuna uwezekano kuna wachezaji Wazawa wasiopungua 3 wataachwa baada ya mikataba yao kuisha na wapo wakigeni pia wasiopungua 4 ili kupisha maingizo mapya.
Imefahamika kuwa Klabu ya Yanga itasajili wachezaji wasiopungua 4 wakigeni, washambuliaji wawli, kiungo mmoja na Mlinzi wa kushoto 1 hao ndio wanawanchi kuelekea dirisha kubwa la usajili.
No comments:
Post a Comment