Mwajaku Atoa Ushauri Kwa Wadada Wenye Maboifrendi Wasio na Pesa wala Kazi Nzuri - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwajaku Atoa Ushauri Kwa Wadada Wenye Maboifrendi Wasio na Pesa wala Kazi Nzuri


Boyfriend wako anaweza kuwa hana gari. Anaweza akawa hana pesa nyingi. Anaweza kuwa anaishi kwenye chumba kimoja. Anaweza kuwa anashindwa kukupa zawadi za gharama. Vilevile hana kazi kubwa ya maana.

Ila inatosha kumuona kuwa anakupenda wewe peke yako. Anazo ndoto nyingi zenye tija. Ni muaminifu. Ni mchapakazi na ni mpole na msikivu..anakufanya utabasamu mara kwa mara.

Anaongea na wewe kila siku na anatabia ya kukusikiliza. Anakujibu sms zako kwa wakati. Anakuvumilia pale unapokuwa out of mood. Familia yake inakujua. Kila siku anakusifu kuwa u mzuri..anakuona kila mara anapopata muda.

Anakujali, anakuheshimu, anakubali hata vitu vidogo unavyovifanya na anajivunia wewe kuwa mpenzi wake na anaku-treat kama malikia kwa sababu wewe ndio kila kitu kwake.

Kwanini umuombe vitu ambavyo hana uwezo navyo? Anaweza kuwa hana saa hizi..ila siku moja huko mbeleni atakuwa navyo.

Sasa hivi anaweza akawa anaishi maisha ambayo siyo ya ndoto zake ila siku moja ataishi apendavyo...

Kichwani mwake anajenga picha kutengeneza familia na wewe na anamaanisha kweli anavyosema anakupenda.

Ladies, mpende mwanaume kama huyo ambae anajitahidi kadiri ya uwezo wake awe kama vile wewe unavyopenda...muda ni rafiki mzuri..siku atakuja kuwa poa..atapata pesa, atanunua ardhi na atajenga nyumba kwa ajili yenu wote.

Hatabaki kuwa na hali hiyo miaka yote, alimradi anajitihada atatimiza kila ahadi aliyokupa kwako na uzao wako. Wewe kuwa mvumilivu tu kama kweli unampenda.

"Don't be pushed around by money and
what you wanna eat now.... I pray you don't eat up the future of your unborn children!" Cc @aliciousm @aliciousm @aliciousm

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz