Hofu ya kupoteza nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka sita, imeuingia uongozi wa Simba ambao sasa umepanga kuelekeza nguvu zote katika mechi 10 zilizobaki ili imalize juu katika nafasi mbili, ikiwa na maana ni lazima iishushe Azam FC.
Kitendo cha kutoshiriki mashindano hayo kitaifanya Simba isiwe na uwezekano wa kuvuna kitita cha Dola 700,000 (Shilingi 1.8 bilioni) ambacho Caf hutoa kwa kila timu inayotinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambacho kinaongezeka zaidi ikiwa timu husika inafika hatua za juu za mashindano hayo.
Kwa sasa Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 46, ikizidiwa na Yanga ina-yoongoza ikiwa na pointi 55, huku Azam FC ikishika nafasi ya pili na pointi zake 50, ikiwa ndiyo timu ina-yotishia nafasi ya Simba.
Tanzania msimu ujao itawakilishwa na timu mbili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo kwa mujibu wa kanuni ni mbili zitakazoshika nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi mwishoni mwa msimu huu, jambo lililoishtua Simba ambayo inaona inaweza kujikuta ikiangukia katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Mmoja wa vigogo wa Simba aliliambia gazeti hili kuwa katika kikao ambacho mwekezaji wa timu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’ alikutana na bodi ya wakurugenzi ya Simba chini ya Salim Abdallah ‘Try Again’ miongoni mwa mikakati iliyowekwa ni kuhakikisha Simba inapata ushindi katika mechi zote 10 ilizobaki-za ili ijiweke katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa na ikishindikana imalize katika nafasi ya pili ambayo kwa sasa inashikiliwa na Azam.
Michezo 10 ambayo Simba imebakiza kwenye Ligi Kuu ni dhidi ya Yanga, Dodoma Jiji, Mtibwa, Na-mungo, Tabora United, Azam, Kagera Sugar, Geita Gold, KMC na JKT Tanzania.
Hata hivyo, Azam inaonekana kuwa tishio kwa Simba msimu huu ikiwa imeizidi kwenye vitu vingi mu-himu kwenye msimamo wa ligi.
Timu tatu za juu kwenye msimamo, Yanga, Simba na Azam zimepoteza michezo miwili kila moja, lakini Azam imeizidi Simba kwenye mabao ya kufunga ikiwa imefunga 49 huku Simba ikifunga 40, lakini mabao ya kufungwa Azam imefungwa 16 Simba ikifungwa 19 pamoja na kwamba ina mchezo mmoja mkononi.
Kama Simba ambayo imeshacheza michezo 20 na Azam 22 haitachanga karata zake vizuri kwenye michezo kumi iliyobaki basi itashiriki Shirikisho msimu ujao.
No comments:
Post a Comment