ILE Siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa ni leo Yanga vs Simba bado unajiuliza utaiangalia vipi mechi hii live buree bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live buree kabisa
Wananchiiiiii...! Ile siku imewadia.. Wanasema usiku wa deni haukawii kucha! Ni pale uwanja wa Benjamin Mkapa mtanange wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba utapigwa
Ni Wazee Derby, Yanga ikiutumia mchezo huu kuwapa heshima Wazee ambao walitimiza vyema wajibu wao na kuhakikisha wanarithisha kizazi cha leo Yanga iliyo imara
Baada ya ushindi wa mabao 5-1 katika mchezo wa duru ya kwanza, matumaini ya mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao ikiendeleza ubabe dhidi ya watani zao
Kama Yanga itashinda leo basi itajiweka katika nafasi nzuri zaidi katika mbio za ubingwa kwani wataongeza gap la alama dhidi ya washindani wake Azam Fc na Simba
Ni derby, itakuwa mechi ngumu ambayo itahitaji wachezaji kuvuja jasho jingi kuweza kupata matokeo mazuri
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesisitiza hawaendeshwi na fikra za ushindi mnono mara ya mwisho walipokutana na Simba
Wanafahamu huu utakuwa mchezo mpya ambao hata wapinzani wao watakuja kivingine kujaribu kulipa kisasi ingawa amewatahadharisha kisasi hicho kinaweza kuwatokea puani
Yanga inaelekea katika mchezo huu ikiwa na kikosi kamili. Wachezaji wote wa Yanga wako tayari kwa mchezo huu ni jukumu la Gamondi na benchi lake la ufundi kuamua silaha 11 atakazozitumia leo
Mageti ya uwanja wa Benjamin Mkapa yanatarajiwa kuwa wazi kuanzia saa 5 asubuhi
No comments:
Post a Comment