Mwanamuziki Juma Jux Afunguka Chanzo cha Kuvurugana na Harmonize - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwanamuziki Juma Jux Afunguka Chanzo cha Kuvurugana na Harmonize

 


Hatimaye msanii Jux amefunguka ukweli wa kilichotokea kati yake na Harmonize punde baada ya kutangazwa kwake kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Afro East Carnival linaloandaliwa na msanii Harmonize bila ya kuwepo kwa makubaliano yeyote baina yao.

Jux ameweka wazi kuwa kitendo hicho amekitafsiri kama utovu wa nidhamu kwa madai ya kuwa Harmonize amemkosea heshima

“Harmonize aliwahi kunicheki ananiambia kuna ishu ya Show, akanitajia tarehe na kila kitu lakini mimi sikujibu chochote kwa sababu tulikuwa tuna chat DM. Aliniambia kwa mambo zaidi meneja wake atanipigia tuongee.

Nikamwambia mpe namba ya Ray ambaye ni meneja wangu, ukapita muda kidogo, sasa leo naamka nikatumiwa artwork na timu yangu wananiuliza kama hii show nimekubaliana nayo, Nikawaambia hapana, Na hata hata Ray alisema pia hakupigiwa simu.

Lakini pia Ray aliwapigia simu akaongea nao, wakamwambia kuna wasanii ambao Harmonize anaongea nao mwenyewe, akasema anadhani Harmonize atakuwa amekubaliana nao ndio maana artwork ikatengenezwa, nikawaomba waishushe lakini walikataa.

Nikamcheki Harmonize nikamuuliza kama aliongea na timu yangu akasema aliongea nayo, ila ngoja awacheki tena, mimi nikamwandikia hakuna makubaliano yoyote na ulitakiwa uhakikishe kama ambavyo ulinicheki mara ya kwanza, kwangu naona kama unanichukulia poa na dharau.

Hiyo message haikujibiwa na muda unazidi kwenda ndio nikaenda pale nika-comment.” alisema Jux

Jux ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano maalum aliyofanya kupitia kipindi cha Empire.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz