Milionea wa Urusi akiri kumuua kwa kumpiga risasi mwanaume ‘aliyedhani kuwa ni dubu - EDUSPORTSTZ

Latest

Milionea wa Urusi akiri kumuua kwa kumpiga risasi mwanaume ‘aliyedhani kuwa ni dubuMwanasiasa milionea katika Mashariki ya Mbali ya Urusi amekiri kumuua mtu ambaye anasema alidhani ni dubu.Igor Redkin, 55, amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari vya Urusi kwamba alikuwa amesikia kulikuwa na dubu kwenye jalala la takataka katika kijiji cha Ozernovsky huko Kamchatka.

Alitaka kumtisha mnyama huyo na alifyatua risasi, lakini baadaye “aligundua kuwa mkazi wa eneo hilo alijeruhiwa katika eneo lililo karibu wakati huo huo,” alisema.

Mwanaume huyo wa miaka 30 ambaye alipigwa risasi baadaye alikufa hospitalini.

Kesi ya jinai ilifunguliwa dhidi ya milionea huyo wiki iliyopita.

Bwana Redkin ndiye mmiliki mwenza wa biashara kadhaa kubwa katika peninsula ya Kamchatka na ameelezewa kama mmoja wa maafisa tajiri wa umma wa Urusi.

Alisema “alikuwa ameshafanya uamuzi na alikuwa tayari kukubali adhabu ambayo mhakama itaamua”.

Tangu wakati alipoondoka chama cha Rais Vladimir Putin cha United Russia.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi, mwanasiasa huyo atatumikia miezi miwili chini ya kifungo cha nyumbani wakati wa uchunguzi.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz