Vifaa 7 vya kiteknolojia vilivyowahi kubuniwa na kuushangaza ulimwengu - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Monday, 1 May 2017

Vifaa 7 vya kiteknolojia vilivyowahi kubuniwa na kuushangaza ulimwengu

Kila mwanasayansi duniani hutaka kugundua teknolojia flani ili kujijengea heshima na jina katika fani yake, lakini kuna baadhi ya vifaa vya kiteknolojia ambavyo vimegunduliwa na wanasayansi mbalimbali duniani ambavyo vimeleta gumzo na kushangaza watu wengi.
Leo May 1, 2017 nimeona si vibaya nikikusogezea teknolojia saba za kushangaza na kustaajabisha zilizowahi kutengenezwa na wanasayansi mbalimbali duniani.
1: Kiatu chenye kiyoyozi
Hii ni moja ya teknolojia ambayo ilistajabisha watu wengi baada ya kampuni ya Hydro-Tech kutengeneza kiatu ambacho kina kiyoyozi kinachosaidia mvaaji wa viatu hivyo kupata ubaridi akiwa sehemu zenye joto kali.kiatu hiki kinauzwa dola 75.
2: Jacket unayoweza kufanya kama TV
Mwaka 2015 kampuni ya Lenovo ilizinduwa jacket inayojulikana kama “screen jacket” ambayo unaweza kuigeuza na kuifanya Tv ambayo unaweza  kuangalia vipindi mbambali. ,jacket hili pia limewekewa program kama Netflix ambapo mtu anaweza kuangalia movie .
3: Kifaa cha kupoozea chakula
Kifaa hiki cha kupoozea chakula cha moto kilitengezwa na kampuni Tech E kutoka Japan, Lengo la designer aliyekibuni kifaa hichi ni kusaidia kupoza chakula cha moto hasa kwa watoto.
4: Kifaa cha kuangalia movie huku unatembea
Kifaa hiki chenye muundo wa kofia kimebuniwa na kampuni ya B-tech kwa ajili ya watu wanaopenda kuangalia movie peke yao bila bughudha ,kifaa hiki kilipata umaarufu mkubwa mwaka 2015 na kiliuzwa zaidi ya pisi milioni 5 duniani kote.
5: Kifaa cha kukupa ulinzi
Mwaka 2016 kampuni ya Techstars ilizindua kifaa maalum ambacho kinaweza kutuma taarifa kwa familia na marafiki  iwapo mvaaji amepatwa na tatizo kwani itaonesha mahali alipo, Kifaa hiki kilibuniwa mahususi kwa ajili ya Wanawake wanapopata matatizo hasa ya kuvamiwa na kubakwa.
6: Kiatu kinachotumia bluetooth
Kampuni ya HSG-IMIT ilizindua kiatu kinachojulikana kama “smart shoes” kwa mara kwanza mwaka 2016 katika maonyesho ya  Consumer Electronics, kiatu hiki kinauwezo wa kuunganishwa na bluetooth ya simu yako ambapo unaweza kufunga na kufungua mikanda ya viatu kwa kutumia smart phone yako.
7: Mkanda wa kuzuia unene
Mwaka 2016 kampuni ya Samsung ilizindua mkanda maalum ambao mtu akiuvaa unamsaidia kujua ale chakula kiasi gani ili asinenepe, mtumiaji wa mkanda huu anaweza kuufunga na kufungua kwa kutumia simu yake ya mkononi.