SERENGETI BOYS YAZIDI KUTAMBA YAILAZA CAMEROON IKIWA NYUMBANI. - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 1 May 2017

SERENGETI BOYS YAZIDI KUTAMBA YAILAZA CAMEROON IKIWA NYUMBANI.


Timu ya taifa ya Tanzania ya  vijana wenye umri chini ya miaka 17 "Serengeti boys" usiku wa April 30 imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 goli lililofungwa na mchezaji Ally Nganzi katika mchezo uliochezwa mjini Yaoundé nchini Cameroon.
Huu unakua mchezo wa tatu wa kirafiki kwa Serengeti boys kucheza ikiwa ni maandalizi ya ya kuelekea Gabon kushiriki katika michuano mikubwa Afrika AFCON.

Akizungumza mara baada ya mchezo kumalizika kocha wa kikosi hicho Bakari Shime amesema "Vijana wametumia nguvu kubwa hasa kulinda goli tulilolipata mapema hadi kuibuka na ushindi,hata hivyo watanzania sasa wakubari timu yao inaenda kushiriki AFCON na lengo kubwa ni kua timu bora Afrika na inawezekana chamsingi waungane na kuipa nguvu TFF" .Hata hivyo Shime aliongeza kwa kusema "Watanzania tuweke tofauti zetu kando tuiwezeshe timu ya Serengeti boys kwani kwa sasa ndio timu pekee imebaki ikishiriki mechi za kimataifa hadi sasa "....