TIMU ambazo Simba inaweza kutana nazo CAF Champions League 2022/2023
Nijuze Habari inakuleta listi ya timu ambazo Klabu ya Simba SC inaweza kukutana nazo kwenye hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Barani Afrika (CAF Champions League 2022/2023)
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limeweka wazi mpangilio wa timu utakaotumika kupanga Makundi ya Michuano hiyo Mikubwa Barani Afrika Ngazi ya Vilabu.
Droo ya hatua hiyo ya Makundi inatarajiwa kufanyika mwezi November 2022, huku Klabu ya Simba SC ya hapa Tanzania ikiwa miongoni mwa timu 16 zinazosubiri kwa hamu kubwa droo hiyo.
CAF imesema kuwa kutakuwa na POTI nne ambapo kila poti itakuwa na timu nne kwa mpangilio ufuatao;
POTI NO 1:
1:Al Ahly
2:Wydad Athletic
3:Esperance
4:Raja Casablanca
POTI NO 2:
1:Mamelod Sundowns
2:Zamalek
3:Horoya AC
4:Petro Atletico
POTI NO 3:
1:Simba SC
2:Belouizdad
3:JS Kabliye
4:Al Hilal
POTI NO 4:
1:Cotton Sport
2:Al Merikh
3:Vipers
4:AS Vita/RC Kadiogo
Aidha kila kundi litakuwa na timu moja kutoka katika kila Poti ikiwa na maana pia timu zilizo kwenye poti moja hazitakutana kwenye hatua ya Makundi.
Simba itapangwa na timu kutoka POTI ya 1, 2 na 4 hivo Simba inaweza kukutana na timu kama Cotton Sport, Al Merikh, Vipers na AS Vita au RC Kadiogo.
Zingine ni Vigogo Al Ahly, Wydad Athletic, Esperance, Raja Casablanca, Mamelod Sundowns, Zamalek, Horoya AC na Petro Atletico.
Taarifa zaidi Bofya HAPA
The post TIMU ambazo Simba inaweza kutana nazo CAF Champions League 2022/2023 appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment