PRISONS, Singida zafungiwa Kusajili
KLABU za Tanzania Prisons na Singida Big Stars zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, zimekutana na rungu la TFF baada ya kufungiwa kusajili wachezaji wapya kwa kipindi cha dirisha moja la usajili.
Taarifa ya kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) iliyotoka Leo Ijumaa October 07 7, 2022 imeeleza kuwa timu hizo zimefungiwa kutokana na kufanya usajili wa wachezaji ilihali wakiwa na mikataba na klabu zao za awali.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Singida ilimsajili Metacha Mnata huku akiwa bado na mkataba na Polisi Tanzania FC hivyo hivyo kwa Tanzania Prisons iloyomsajili Mussa Mbisa huku akiwa bado na mkataba na Coastal Union.
Kwa mujibu wa kamati hiyo, uamuzi huo umezingatia kanuni ya 47 (21) ya Ligi Kuu, hata hivyo, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imezikumbusha klabu zote nchini kuwa Usajili wa wachezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni na timu ambazo zitakiuka kanuni hizo, zitachukuliwa hatua.
The post PRISONS, Singida zafungiwa Kusajili appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment