Muna Love "Mungu Amenitoa Kwenye Umauti" - EDUSPORTSTZ

Latest

Muna Love "Mungu Amenitoa Kwenye Umauti"ROSE Alphonce Nungu almaarufu Muna Love; ni mwigizaji wa Bongo Movies ambaye hajaonekana lokesheni kitambo ambaye anasema kuwa, kila siku anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu amemuinua na kumtoa kwenye umauti kisha kumrejesha uzimani.

Muna anasema kuwa, jambo hilo hakulitegemea kabisa katika maisha yake kama atasimama tena.

Hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji (sajari) sehemu mbalimbali za mwili wake kwa ajili ya kurekebisha maumbile yake.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA kwa njia ya WhatsApp akiwa nchi za nje, Muna anasema kuwa, alipita katika mapito magumu mno kiasi cha kukata tamaa, lakini Mungu amemsaidia na ameinuka na hivi karibuni atarejea tena.


“Mungu amenitoa kwenye umauti, nitarejea tena nikiwa na hofu ya Mungu. Niliyopitia ni funzo kubwa sana katika maisha yangu na nikitulia nitaelezea yote bila woga na hapo mtu ataamua kujifunza mwenyewe,” anasema Muna ambaye hivi sasa anaonekana kupona kabisa.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz