Mwanamuziki Otile Brown afanyiwa upasuaji - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwanamuziki Otile Brown afanyiwa upasuaji

Mwanamuziki mashuhuri Jacob Obunga almaarufu kama Otile Brown anaendelea kupata afueni baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali moja jijini Nairobi.

Bingwa huyo wa muziki wa kisasa alifahamisha wafuasi wake kuhusu upasuaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Brown alipakia video iliyoonyesha akiwa anasukumwa kutoka kwa chumba cha upasuaji huku  akiwa amelazwa kwa kitanda cha wagonjwa.


"Ilienda vizuri" Brown aliandika chini ya video iliyoonyesha akiwa ameporea katika wadi huku akionekana mchangamfu.


Otile Brown hata hivyo hakueleza sehemu ya mwili wake ambayo ilifanyiwa upasuaji wala kilichokuwa kimemwathiri.

Mamia ya mashabiki wa msanii huyo walimiminika mitandaoni kumwandikia jumbe nzuri na kumtakia afueni ya haraka.


 
"Shukran kwa jumbe zenu nzuri. Nazithamini" Brown aliwajibu walioonyesha upendo.

Sote tunamtakia mwanamuziki huyo mahiri afueni ya haraka.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz