Diamond Platnumz Ndio Mrithi wa RUGE Mutahaba, Hilo Halina Ubishi - EDUSPORTSTZ

Latest

Diamond Platnumz Ndio Mrithi wa RUGE Mutahaba, Hilo Halina Ubishi


Ruge alikuwa MasterMind, Diamond Platnumz pia ni MasterMind, Ruge alikuwa MasterMind kwasababu alitumia akili kubwa katika kuongoza na kubuni Project mbalimbali ndani ya Media, Jamii, Tasnia ya Burudani n.k


Tangu kifo cha Ruge kitokee Tulikosa mtu ambaye anaweza kuvaa viatu vya Ruge ila kwasasa naamimi Diamond Platnumz ndio Mrithi kamili wa Ruge.

Diamond platnumz anaakili kubwa anajua uongozi na ni mbunifu pia, hii inatosha kabisa kumpa jina la MasterMind.

Diamond platnumz ni Mrithi wa Ruge kwasababu hivi sasa anafanya maajabu ambayo kwa muda mrefu hatujaona na hata kama yalikuwepo basi yalifanywa na Ruge.

UANDAAJI WA EVENTS.

Ruge alikuwa Mtaalam sana wa kuandaa event na ikafanikiwa sana, mfano Fiesta, enzi za uhai wake ilikuwa show kubwa Tanzania na Afrika nzima. Hivi sasa Diamond ndio anaweza kuandaa Event na Tanzania ikashituka, Tunaona Namna ambavyo alifanya vizuri kwenye Wasafi Festival, Event ya kumkaribisha Zuchu, Uzinduzi E.P ya Zuchu, Mahaba Ndindindi, yani ni Event kubwa sana ambazo zimeacha Historia.

PROMOTION.

Clouds chini ya uongozi wa Ruge ilikuwa vizuri sana kwenye promotion, yani wakiandaa event basi Tanzania nzima itajua, wakiamua kumpandisha msanii ni sekunde moja yani atajulikana Bongo nzima, ila kwasasa Diamond ndio anauwezo huo, Event za Wasafi zinapata Promo kubwa mno, wasanii wa Wasafi wanapata promo ya kutosha, ukisainiwa wasafi, wiki moja unajulikana Tanzania nzima.

MUZIKI.

Ruge alitoa wasanii wengi sana, mwanzo walikuwa hawajulikani lakini kwa mkono wake na clouds kwa ujumla karibia kila msanii wa bongo fleva ameshine. Kwasasa Diamond Platnumz ndio Mfalme, kupitia lebo yake ametoa wasanii kibao ambao baadhi wametoka kwenye lebo yake na wakatoa wasanii wengine.

MEDIA.
Uwezo wa Ruge katika media ulikuwa mkubwa sana, alifanya watanzania wapende burudani kuliko chochote kile, alifanya clouds kuwa media bora Tanzania. Ila kwasasa, Diamond Platnumz ndio ameishikilia Tasnia ya Habari hasa katika nyanja ya Burudani, Wasafi inasikilizwa sana, kwenye Digital platforms inafatiliwa sana kuliko media yoyote ile Tanzania na Afrika Mashariki.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz