KWANINI WANAUME WANAPENDA TENDO NA SIYO KUOA - EDUSPORTSTZ

Latest

KWANINI WANAUME WANAPENDA TENDO NA SIYO KUOA

KWANINI WANAUME WANAPENDA TENDO NA SIYO KUOA

UNA sababu maelfu za kusoma XXLOVE. Kwa kadiri ya uwezo, tunakupa dawa kamili ya kile ambacho kinasumbua katika masuala ya mapenzi. Uhusiano wa wengi umeimarika baada ya kujiunga na safu hii. Tunaendelea kuyajadili mapenzi.  Wanawake wengi sana wanalalamika namna wanaume wa sasa walivyo kwenye uhusiano. Wanasema wanaume wengi wamepoteza moyo wa dhati wa kuwepo kwenye uhusiano (commitment). Wanaonekana kama hawana mapenzi ya dhati tena. Wao kila siku ni kuulizia tu tendo la ndoa! Na kama halipatikani, basi anaweza kuondoka muda wowote kuelekea huko anakolipata tendo hilo. Hali hii inasumbua uhusiano na uchumba wa wengi umekumbwa na wengine wamelazimika kuvunja uchumba wakiwa karibia kuingia kwenye ndoa.

Baadhi ya wanawake wanalalamika wakisema wako wapi wale wanaume wenye kiu ya ndoa? Wako wapi wale wanaume wenye kuongelea kutaka kuoa na kuanza familia na kuwapenda watoto wao? Wako wapi wale wanaume wenye kiu ya mafanikio na kudumisha maisha pamoja na wake zao. Mbona kama wamemalizika na waliobaki wana kiu ya kula bata tu na kufanya mapenzi bila kumaanisha. Yamkini na wewe unayesoma makala hii unajiuliza maswali haya pia. Wanawake wengine wamekuwa wakinieleza kuwa wanaume waliobaki siku hizi ni wavivu, hawana hamasa ya maendeleo, atakuwa na wewe kama ana uhakika wa tendo la ndoa tu!

Hapa ngoja nizungumze na wasichana na wanawake ambao nao wana mawazo na maswali kama haya. Ni kweli vilio na malalamiko yenu ni vya kweli na tunasikitika pamoja kwenye hili, lakini zipo sababu za hali hii.

Ni vyema dada zangu mkafahamu kuwa kwa kiasi kikubwa mifumo au mbinu za mchezo wa uhusiano zimebadilika sana. Nadharia za zamani nazo zinaonekana kubadilika na hii imewafanya wanaume wengi kubadili aina ya maisha yao. Fuatilia sababu zifuatazo ili kulielewa hili sawia. Kumbuka kuwa sababu hizi zimetokana na majibu ya wanaume wengi;

Mgawanyo wa majukumu baina ya wanaume na wanawake umeingia doa. Wanaume wa kawaida hupenda kufanya kazi ili kujitafutia kipato chao na familia na wakitoka kazini au kwenye majukumu yao ya kila siku wanataka kupumzika na kufanya kile wanachojisikia kufanya iwe ni kulala, kuangalia televisheni, kusikiliza redio n.k na siyo kukimbizana na vijishughuli vya nyumbani kama vile kusaidia kupika, kusafisha vitu, kukaa na watoto na kazi nyingine ambazo wao wanaona siyo zao.

Ndani yao wana kiu ya kuona wapenzi wao wanawakaribisha kwa upendo, kuwaandalia maji, kuwasaidia kuweka mazingira ya wao kupumzisha akili na mwili baada ya kula chakula, wana kiu ya kuona tabasamu, sauti nzuri na ikiwezekana kupata penzi. Kwao hali hii huwapa nguvu tayari kuwaandaa na siku nyingine ya kesho.

Tatizo linakuja pale mwanaume huyu anajikuta ameoa mwanamke mfanyakazi au mwenye majukumu mengi yamkini kumzidi hata mume, akikaa, akilala anawaza kazi, anawaza biashara, anawaza miradi na vingine vingi, akirudi nyumbani mwanamke huyu anakuja amechoka na hajiwezi kimwili na kiakili kama vilevile alivyo mume wake, mke na mume wote wamechoka sana, mke na mume wote wana msongo na wanahitaji kupepewa maana hawajiwezi kwa kuchoka. Mwanamke amechoka hana hamasa ya kufanya kazi ndogondogo za nyumbani au hata kuwashughulikia watoto.

Ulimwengu wa kazi na majukumu umeshamfanya mwanamke kuwa na misuli ya kukimbizana na maisha kama mwanaume. Hali hii inawafanya wote wawili wanarudi nyumbani wamechoka kabisa na kila mmoja ana uhitaji wa msaada wa mwenzake wakati hakuna aliye tayari wala aliye na nguvu ya kumsaidia mwenzake. Katika hali kama hizi, vijihasira na vihisia hasi huamka kwa urahisi sana na ugomvi huweza kupenye hapohapo.

Ule uwiano wa masaidiano umeshapotea na kilichoota ni hatari sana kwa uhusiano wa wawili hawa. Wachunguzi wanasema ndiyo maana zipo jamii na imani fulani ambazo mke huachwa nyumbani akimsubiri mume wake na mume kazi yake ni kuhakikisha anafanya kila jitihada kuilisha na kuitunza familia, siyo kwamba hawataki mke afanye majukumu ya baba la hasha, wanamuandaa kuweza kumhudumia mumewe vilivyo.

Najua hoja za wengi pia zina mashiko kwamba wanawake wengine wangependa kukaa na kuwasubiria waume zao ili wawaenzi, lakini wanaume wengine wameshindwa kubeba majukumu yao kama wanaume na viongozi wa familia na hiyo imewalazimu wanawake kusimama na kufunga mkanda. Pamoja na hayo hali ya usumbufu haijapungua.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz