Simba wanamtaka Marouf Tchakei - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba wanamtaka Marouf Tchakei

Marouf Tchakei

Ni kesho Dodoma jiji vs Simba usikose kuitazama mechi hii live bure kabisa kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live bure kabisa pia ukiwa na app hii utaweza kutazama muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili na pia ya mambo yetu yale bofya sasa kudownload

Baada ya kumkosa katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 2024, mwaka huu, Klabu ya Simba imeanza tena mchakato wa kusaka huduma ya winga na kiungo mshambuliaji wa Ihefu, raia wa Togo, Marouf Tchakei.

Simba SC imepania kwa kiasi kikubwa kufumua kikosi chake na kutengeneza timu mpya yenye ushindani kwa ajili ya msimu jao wa mashindano, inapiga hodi kwa kiungo huyo ambaye anacheza namba moja na Clatous Chama.

Habari kutoka ndani ya Simba SC zinasema huenda safari hii wanaweza nyota huyo kirahisi kutokana na kilichoelezwa pia nyota huyo yuko tayari kupata changamoto mpya lakini bado anabanwa na mkataba wake.

Chanzo kingine kutoka Ihefu kimesema bado ana mkataba, hivyo kama Simba SC inamhitaji italazimika kufanya mazungumzo.


"Tulimhitaji dirisha dogo la usajili, lakini ilishindikana, klabu yake iliweka ngumu lakini mwenyewe alikuwa radhi kujiunga na timu yetu, akatuambia tusubiri msimu uishe atakuwa huru, sisi tunasimamia pale pale, lakini kama itakuwa vinginevyo basi tutaangalia itakavyokuwa lakini ni lazima tumng'oe, tumejidhihirisha ni mchezaji mzuri na atatusaidia sana, ameshaifahamu Ligi ya Tanzania na ameizoea," amesema mtoa taarifa hizi.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz