BUSERESERE WAAMBULIA KIPIGO NA KUWAPISHA MTIBWA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 26 February 2018

BUSERESERE WAAMBULIA KIPIGO NA KUWAPISHA MTIBWA
Mtibwa Sugar imekuwa miongoni mwa timu zilizoingia hatua ya nane bora ya mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuisambaratisha Buseresere FC kwa mabao 3-0.

Katika mchezo huo uliopigwa Nyamagana Stadium, Mtibwa Sugar walijipatia mabao yao kupitia Hassan Dilunga, aliyefunga kwa njia ya penati katika dakika ya 52, na katika dakika ya 80, Haruna Chanongo aliandika bao la pili.

Haikuchukua muda mrefu, kuelekea mwishoni mwa mchezo, kiungo Ally Malani, aliiongezea Mtibwa bao la 3 kwenye dakika ya 90 na kuufanya mchezo huo umalizike kwa matokeo ya 3-0.

Sasa Mtibwa inasubiri droo ya kupangiwa icheze na nani katika hatua ya robo

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ