BOB JUNIOR ATETA KILICHOMPOTEZA KWENYE ULIMWENGU WA SANAA - EDUSPORTSTZ

Latest

BOB JUNIOR ATETA KILICHOMPOTEZA KWENYE ULIMWENGU WA SANAA



Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’.

MSANII wa Bongo Fleva ambaye pia ni prodyuza, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ ameibuka na kueleza kilichompoteza kwenye muziki huku akijikuta akipitwa na wale wanamuziki aliowafundisha au kuwaingiza kwenye tasnia hiyo akiwemo Bonge la Nyau.

 Bob Junior alisema ni kweli amepitwa na amepotea kwenye ulimwengu wa muziki kwa sababu aliamua kuingia kwenye biashara ambapo mpaka sasa anamiliki maduka mawili Kariakoo huku akiwa anasimamia mali za wazazi wake kwa kuwa ndiye mtoto wa kwanza.

“Ninafanya biashara ya kupeleka bidhaa mbalimbali nchi tofautitofauti na pia namiliki maduka mawili Kariakoo hivyo nakuwa bize sana ndiyo maana nimepotea kwenye muziki ila wiki ijayo nitaanza kuachia ngoma mpya,”alisema Bob Junior.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz