NGOMA AZIDI KUPASUA VICHWA - EDUSPORTSTZ

Latest

NGOMA AZIDI KUPASUA VICHWA



Licha ya ufafanuzi uliojitosholeza uliotolewa na uongozi wa Yanga juu ya kukosekana kwa Obrey Chirwa, bado mchezaji huyo anahitaji kuwajibika zaidi kuitumikia Yanga na sio kuweka zaidi maslahi yake mbele.

Huenda ana madai ya msingi kwa Yanga lakini ni busara kuusikiliza uongozi unapomuahidi kwani naamini yeye sio mchezaji pekee na wa kwanza kuidai Yanga.

Na hakuna namna yoyote kwa uongozi wa Yanga chini ya Katibu Mkuu mweledi Charles Mkwasa unaweza ukamdhulumu madai yake.

Katika wachezaji wa Kimataifa walio kwenye kikosi cha Yanga, sijawahi kumsikia Thabani Kamusoko au Amissi Tambwe akifanya mgomo wa aina yoyote.

Siamini kama wawili hawa hawajawahi kuwa na madai kwa uongozi lakini wamekuwa na nidhamu, wanapokuwa fiti wanajituma kwelikweli.

Lakini hali ni tofauti kwa Obrey Chirwa na Donald Ngoma. Nakumbuka mwaka jana Chirwa aligoma kusafiri kwenda Algeria kwenye mchezo wa marudio kombe la shirikisho dhidi ya MC Alger ambapo Yanga ilipoteza kwa mabao 4-0.

Yeye sambamba na Vicent Bossou waligoma kushinikiza walipwe stahiki zao.

Wachezaji wa Yanga ni lazima wafahamu kuwa hivi sasa klabu yao inapita katika kipindi kigumu tangu Mwenyekiti wake Yusuph Manji akumbwe na matatizo yaliyompelekea ajiuzulu wadhifa wake.

Hiki ni kipindi cha mpito tu hasa ikizingatiwa tayari Yanga imeanza mchakato wa kuifanya klabu ijiendeshe kwa faida.

Wakati wa Neema kwa wachezaji wa Yanga unakuja pengine jambo hilo litafanikiwa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo..

Naamini Yanga hiyo mpya itakuwa kimbilio la kila mchezaji mzuri kwani wakati huo fedha halitakuwa tatizo kabisa.

Chirwa anaweza kuwa anarubuniwa hasa ikizingatiwa mkataba wake wa kuitumikia Yanga unamalizika Juni 30, 2018 lakini namwambia tu asije akaja kujuta baadae.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz