BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Showing posts with label Magazine. Show all posts
Showing posts with label Magazine. Show all posts

Saturday, 2 June 2018

02 June

GUMUZO MITANDAONI KUHUSU TARATIBU ZA MAZISHI NCHINI GHANA

Raia wa Ghana wanafahamika kwa ubunifu wao wa majeneza.


Wiki iliyopita kulikuwa na taarifa jinsi mazishi yanavyotekelezwa huko Ghana.

Mwili wa chifu aliyefariki miaka sita iliyopita ulikuwa kwenye hifadhi ya maiti kutokana na mzozo kwenye familia ya nani atakaye kuwa ''muombolezaji maalum.''

Lakini taarifa hiyo haishangazi kwani ni mazoea ya raia wa Ghana kuiacha miili ya wafu kwenye hifadhi ya maiti kwa muda mrefu ili kusuluhisha mizozo inayoibuka baada ya kifo chochote kinachotokea nchini humo.

Raia wa Ghana wanasifika kwa majeneza yaliyobuniwa kwa miundo tofauti kama hili lililotengenezwa maalum kwa chifu.

Utamaduni huu unaangaziwa na jamii inayotoka kusini mashariki, Ga.

Maonyesho ya majeneza yamefunguliwa rasmi ya Jack Bell Gallery huko London.

Mazishi yaliyoghali zaidi na yaliojaa mbwembwe na majeneza yaliotengenezwa kwa miundo tofauti yamehifadhiwa.
Mageneza ya kuvutia
Lakini jukumu la ''familia'' kwenye mazishi ni lipi

Raia wa Ghana akipinga ngoma wakati wa mazishi.Unaweza kudhani kwamba unatambua nani hasa ni familia yako. Lakini kifo kinapotokea ,maelezo kuhusu familia hubadilika kabisa.
Ni familia tu, yaani jamaa zako wa upande uliko zaliwa ndio hutoa uamuzi wa nani atakaye kuwa muombolezi mkuu na vyeo vyote ambavyo hutokana na kifo.

Mfano wa geneza hili litengenezwa mwaka 1951 na seremala wawili , Kane Kwei na kakake Adjetei. Walitengeneza geneza hilo kwa bibi mwenye umri wa miaka 91 ambaye hakuwahi kusafiri kwa ndege lakini aliwaambia kwamba alitamani kusafiri kwa ndege.

'Familia hiyo' na muombolezaji mkuu wanaweza kuwa hawajazungumzi kwa muda wa zaidi ya miaka 30 na marehemu, lakini wanatambulika kumfahamu zaidi aliyefariki kuliko mpenzi wake na watoto.

Baada ya hapo ndipo mikutano isiyoisha hufuata inayoongozwa na 'familia', pale maneno ya mpenzi wa marehemu na watoto yanapuziliwa mbali.

Tena wiki kadhaa hutumika kuandika tangazo la kifo kwenye gazeti na ni kazi ngumu kuandika orodha ya waombolezaji kwa hadhi zao.

Kwa hivyo siku nyengine ukikutana na tangazo kama hilo kwenye gazeti la Ghana , ni heri uthamini kazi hiyo ya uandishi wa tangazo hilo ili kuhakikisha hakuna migogoro ya aina yoyote inatokea au hata migogoro ya hapo awali kuzuka upya.

Miguu ya marehemu akiwa kwenye nyumba ya kuhifadhi maiti

Jukumu la kumchagua muombolezi mkuu ni gumu sana kwa sababu si yeye pekee ndiye anayetoa maagizo ya mazishi , yeye pia lazima awe mwanamume na si mwanamke, yeye ndio anayetoa uamuzi wa mwisho wa nani atakaye mrithi marehemu.

Kwa wakati huo wote, mwili wa marehemu huhifadhiwa kwenye jokovu iwapo kutakuwepo na migogoro ya lini na wapi marehemu atakapo zikwa.

Si jambo la kushangaza kwamba mara nyingi watu hujipata kortini kwa makosa ya kumzuia mtu kuuondoa mwili wa marehemu.

Kwa mara nyingi , ucheleweshwaji wa mazishi hautokani na mizozo.

Densi na nyimbo ni sehemu ya mazishi nchini Ghana
Sisi huchukulia maanani kumpatia marehemu mazishi ya hali ya juu.
Huwa tunaifanyia marekebisho nyumba ya marehemu alipofia au hata kumjengea nyumba mpya ili kukidhi kiwango cha mazishi.

Hilo huchua muda.

Iwapo mtu anawakata wageni mashuhuri kwenye mazishi hayo , hapo basi tarehe maalum inastahili kubuniwa kulingana na wageni hao.

Na hilo pia huchukua wakati mwingi.

Jeneza hili maalum linaaminika kutoka huko Teshi, jamii ya wavuvi iliyo nje kidogo ya mji mkuu wa Accra. Mvuvi angezikwa kwenye geneza lenye umbo la samaki.

Katika mazishi ya mfanyibiashara na mwanasiasa maarufu ,Nana Akenten Appiah-Menka.
Kitabu cha maelezo ya mazishi kilikuwa na kurasa 226 ya picha zake na risala za rambirambi kuhusiana na maisha yake aliyoishi ya miaka 84.

Pia hilo huchukua muda kukusanya hayo yote.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

Wednesday, 30 May 2018

30 May

FAIDA 10 MUHIMU KWA AFYA YAKO ZITOKANAZO NA MAFUTA YA NAZI

Mafuta ya nazi 

FAIDA KUMI MUHIMU KWA AFYA YAKO ZITOKANAZO NA MAFUTA YA NAZI

1. Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo:

Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.

2. Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula:

Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.

3. Mafuta ya nazi hung’arisha ngozi:

Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji.

4. Huongeza nguvu mwilini:

Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ‘medium chain triglycerides – MCT’ ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa ‘ketones’ ambacho ni chakula cha ubongo. Kwahiyo ikiwa unatafuta lift ya kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.

5. Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya:

Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya. Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!

6. Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama:

Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula. Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki kuwa magumu hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.

7. Huzuia maradhi mengi hatari mwilini:

Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric acid. Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini. Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mine na utaona maajabu.

8. Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu:

Hii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

9. Hutumika kulainisha uke mkavu:

Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.

10. Husaidia katika ugonjwa wa mzio/aleji:

Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza, moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.

MHIMU: Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani ile ya asili. Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Tuesday, 1 May 2018

01 May

WAFAHAMU WATU 12 WALIOWAHI KUFIKA KWENYE MWEZI
Mtu wa mwisho kutembea kwenye Mwezi, Gene Cernan, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

Alikuwa kamanda wa chombo cha safari za anga za juu cha Apollo 17 mwaka 1972 na miongoni mwa watu watatu waliofika mwezini mara mbili.

Lakini kuna watu wengine 11 waliomtangulia kufika na kuukanyaga Mwezi. Ni nani hao?


Neil Armstrong (1930 - 2012) na Edwin 'Buzz' Aldrin (alizaliwa 1930)


Armstrong ni maarufu sana kwa maneno yake baada ya kuwa mtu wa kwanza kuukanyaga Mwezi: "Hatua moja ndogo kwa mwanamume mmoja, hatua moja kubwa kwa binadamu."

Buzz Aldrin alimfuata.


Wakiwa kwenye Mwezi, Neil na Buzz waliweka bendera ya Marekani na kuacha bango lililokuwa na ujumbe, "Hapa, wanaume kutoka sayari ya Dunia walikanyaga Mwezi kwa mara ya kwanza Julai 1969, AD (Baada ya Kuzaliwa kwa Yesu). Tulifika sote hapa kwa amani kwa niaba ya binadamu wote."

Charles 'Pete' Conrad (1930 - 1999)


Apollo 12 ilipaa angani kukiwa na tufani na radi, hali iliyosababisha nguvu za umeme kuzimika muda mfupi baada yao kuruka angani.

Conrad mwishowe alipoukanyaga Mwezi, alisema kwa sauti: "Whoopee! Bwana, hiyo huenda ilikuwa hatua ndogo kwa Neil, lakini kwangu imekuwa kubwa sana."

Alan L Bean (alizaliwa 1932)


Bean ni msanii pekee ambaye amewahi kusafiri nje ya sayari ya dunia.

Michoro na picha zake kwa hivyo zina uhalisia fulani kuhusu hali ilivyo kwenye Mwezi.

Alan Shepard (1923 - 1998)


Shepard anakumbukwa kwa kupiga mipira kadha ya gofu kwenye Mwezi akitumia kipande kidogo cha chuma.

Kutokana na kiwango cha chini cha nguvu mvutano (graviti), mipira hiyo ilikwenda mbali sana kuliko inavyowezekana kwenye Dunia.

Edgar D Mitchell (1930 - 2016)


Mitchell alikuwa binadamu wa kwanza kupeperusha picha za runinga za rangi kutoka kwenye Mwezi. Alibeba pia jiwe la uzani wa kilo 43.5 kutoka mwezini pamoja na mchanga na akarejea navyo duniani.

David Scott (alizaliwa 1932)


Scott ni maarufu sana kutokana na stempu zake.

Bila idhini ya Nasa, alisafiri na stempu za posta hadi mwezini akiwa na mpango wa kuziuza baada ya kurejea nazo duniani. Hakusafiri anga za juu tena.

James B Irwin (1930 - 1991)


Irwin alipokuwa safarini, maafisa ardhini waligundua alikuwa akikabiliwa na matatizo ya moyo.

Lakini kwa sababu alikuwa akipumua oksijeni asilimia 100 na nguvu mvuto huko kwenye Mwezi zilikuwa chini, waliamua hakuwa hatarini.

Mpigo wa moyo wake ulirejea kawaida aliporudi duniani.

Hata hivyo, alifariki kutokana na mshtuko wa moyo miezi kadha baadaye.


John Young (alizaliwa 1930)


John Young ndiye mwana anga aliyehudumu muda mrefu zaidi katika historia ya Nasa, kufikia sasa.

Wakati mmoja, aliingia na kipande cha mkate kilichotiwa mboga kwenye chombo cha anga za juu safarini.

Wakuu wa Nasa hawakufurahishwa na hilo. Lakini Young aliendelea na kazi na alisafiri anga za juu mara sita.

Charles M Duke Jr (alizaliwa 1935)


Duke aliweka historia alipougua surua wakati wa mafunzo ya wahudumu wa ziada wa Apollo 13.

Aliwaweka hatarini wahudumu na kulazimisha mmoja wa wana anga kubadilishwa.

Harrison 'Jack' Schmitt (alizaliwa 1935)


Schmitt alikuwa mwanasayansi wa kwanza kwenda anga za juu.

Alikuwa kwenye Apollo 17 na alikaa siku tatu kwenye Mwezi akiwa na Gene Cernan.

Alirusha nyundo pekee waliyobeba mbali na pia aliacha vifaa vyake vya kupimia kwenye Mwezi.

Thursday, 26 April 2018

26 April

ORODHA YA WANAWAKE WAZURI 10 DUNIANI NA NCHI ZENYE WAREMBO WAKALI ZAIDI


Tunaona quotes nyingi zikisema kuwa uzuri uko ndani ya mtu, ni katika macho ya mtu kuangalia uzuri. ni kweli katika nafsi na kadhalika. Hata hivyo tunasisitiza kuwa nzuri ni mambo ambayo yanaonekana na yanayovutia macho. .
Hapa kuna orodha ya nchi kumi za juu na wanawake waliovutia sana. Nchi hizi zinasemekana kuwa na wanawake wazuri, wenye kuvutia na wenye kupendeza duniani. Hebu tuangalie:


Hii hapa orodha ya warembo 10 na nchi kumi zenye wanawake wanaovutia zaidi.

Liza Soberano - Ufilipino Uzuri .

10. Philippines

Watu wa Filipino wanajulikana kwa mtazamo wao mzuri na uzuri lakini kuna upande mwingine wa nchi hii. Ina mafanikio zaidi katika "Vipindi vya Urembo Bora Vya Kimataifa vya Kimataifa". 

Helen Flanagan - Mwanamke mzuri sana wa Uingereza.


9. Uingereza


Wanawake wa Uingereza wa leo ni mchanganyiko wa tamaduni tofauti ambazo ni kwa nini huja katika tani mbalimbali za ngozi na inaonekana. Wao ni wenye elimu, wenye busara na juu ya yote - nzuri. 

Eugenie Bouchard - Mchezaji Bora zaidi wa tenisi wa Canada .

8. Marekani / Canada


Wanawake wa Amerika ni furaha , huru na wanajua jinsi ya kujitunza wenyewe. Nje ya barabara ya Miami, NY na Los Angeles utaona wanawake wengi mzuri ambao wanajua kujitunza wenyewe kwa sababu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. Tutachukua wanawake wa Canada na Amerika kwa kiwango sawa. Angalia wanawake kumi wenye moto zaidi zaidi nchini Canada .


Doutzen Kroes - Mwanamke Mzuri zaidi wa Kiholanzi .
7. Uholanzi (Wanawake wa Kiholanzi)Kwa urefu wa urefu wa 5'7 "na nywele za blonde, mwanamke Kiholanzi anastahili kuwa katika nafasi ya 7 katika orodha ya nchi zilizo na wanawake waliovutia zaidi ulimwenguni. Angalia orodha ya Maeneo Ya Juu 10 na Wasichana Wenye Nzuri .

Mfano Mzuri Mzuri wa Kiitaliano Cristina Chiabotto.

6. Italia

Unaposema juu ya uzuri wa classy, ​​unazungumzia wanawake wa Italia walio sasa kwa mtindo, mtindo na babies. 

Norelys Rodriguez - Uzuri wa Venezuela.

Venezuela


Wanawake kutoka nchi hii wana taji nyingi kutoka mashindano ya uzuri wa kimataifa na miili yao midogo, ndogo hufanya hivyo kwa wapiganaji wa juu kila mwaka.

4. Uturuki

Meryem Uzerli - Mwanamke wa Kituruki wa Sexiest.


Uturuki hufanya juu ya orodha yetu juu ya wanawake nzuri na kwa nini haipaswi hivyo? Wao ni photogenic na takwimu nzuri na kujifanya karibu na ukuu ambao unaweza tu kuhusishwa na wafalme na vichwa vya historia ya Kituruki. Ikiwa una shaka, fuata sabuni na vipindi vya Kituruki kwenye TV!

Mfano wa Kirusi Mzuri zaidi Irina Shayk

3. Urusi

.

Je, umeona Mwanasheria Mkuu wa Urusi ? Hiyo inapaswa kukupa wazo la uzuri nchini. Wanawake wa Kirusi wana mchanganyiko wa sifa za magharibi na mashariki kwa namna ya cheekbones ya juu, miili pana na mirefu yenye nywele.  

Mwanamke mzuri Kiukreni Ani Lorak.
2. Ukraine


Wakati Ukraine na Urusi ni sawa, tunaona kuwa wanawake wa Ukraine wanajishughulisha zaidi kuliko wale wa Urusi. (Kura yetu kubwa bado ni kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ingawa!) 

Adriana Lima - Wanawake Wazuri zaidi wa Brazili.

1. Brazil


Wanawake wa Brazil wanajulikana kwa maslahi yao katika kijamii na mila. Wanajua jinsi ya kujitegemea, wanafanya jukumu kubwa katika sherehe ambazo huingia nchini kila mwaka. Nchi ina wanawake bora zaidi duniani.
Hizi ndio nchi kumi za juu na wanawake waliovutia zaidi
Brazil
Ukrain
Urusi
Uturuki
Venezuela
Italia
Uholanzi
USA / Canada
Uingereza
Philippines


like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika

For Booking>>>
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI

Saturday, 31 March 2018

31 March

JITIBU MWENYEWE; ORODHA YA VYAKULA ASILIA VYENYE KUONGEZA NGUVU ZA KIUMEMwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.


Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.


Sababu za kukosa nguvu za kiume
Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.


1. Blueberry


Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume.


Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.
2. Mtini (Figs)

Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.


3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)

Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.


Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.


4. Karanga

Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.


5. Vitunguu saumu

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.


6. Ndizi

Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).
7. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.
Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.


Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.


Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.


Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.

NINI MAONI YAKO? ACHA UJUMBE WAKO HAPA CHINI!!!

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno