SABABU ILIYOMFANYA MWINYI AANDIKE BARUA KUOMBA KUACHWA NA YANGA HII HAPA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 29 December 2017

SABABU ILIYOMFANYA MWINYI AANDIKE BARUA KUOMBA KUACHWA NA YANGA HII HAPA

Beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji ameiandikia barua klabu yake akitaka imuachie aende zake kutafuta maisha.


Haji ameindika barua akitaka Yanga imuachie aende kujiunga na klabu ya AFC Leopards ya Kenya ambayo tayari kumsajili.


Akizungumza na SALEHJEMBE, Haji amesema ameona hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga, hivyo angependa kwenda kujiendeleza zaidi.


"Kama sina nafasi, maana yake sina msaada na sihitajiki. Hivyo kwa makubaliano mazuri bila ya kugombana acha niende nikajiendeleze.


"Kazi yangu ni soka na ninataka kujiendeleza. Siwezi kuendelea nikiwa benchi, hivyo Yanga nimewaandikia waniachie niwahi kujiunga na AFC Leopards," alisema.


Beki huyo alionyesha kiwango cha juu na kuisaidia Zanzibar Heroes kufika fainali ya Kombe la Chalenji lililomalizika wiki moja na ushee iliyopita.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ