;
SIMBA WAANZA KUMNYATIA MZAMBIA MWINGINE KUMRITHI OMOG - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 29 December 2017

SIMBA WAANZA KUMNYATIA MZAMBIA MWINGINE KUMRITHI OMOG
Kocha wa zamani wa Simba mzambia Patrick Phiri anatajwa kuwa miongoni mwa makocha watakaochukua kibarua cha kuifundisha Simba baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Joseph Omog kuoneshwa mlango wa kutokea kufuatia kutupwa nje kwa timu yake kwenye michuano ya kombe la shirikisho Tanzania (Azam Sports Federation Cup).

Habari ambazo shaffihdauda.co.tz imezipata ni kwamba, kwa sasa kuna mchakato unaendelea ndani ya Simba kutafuta kocha ambaye atachukuwa nafasi ya Omog lakini jina la Phiri likipewa kipaumbele katika mchakato huo.

“Ni kweli kwa sasa Simba kwa sasa ipo katika harakati za kuhakikisha kocha mpya anapatikana haraka kuchukua nafasi ya Omog aliyefukuzwa, Patrick Phiri anapewa nafasi kubwa katika mchakato huo kutokana na uzoefu wake kwenye ligi ya Tanzania pamoja na uzoefu ndani ya klabu kwa hiyo anaweza akapewa nafasi” kimeeleza chanzo kutoka ndani ya uongozi wa Simba.


Phiri anakumbukwa kwa kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara bila kufungwa rekodi ambaye ilifikiwa na Joseph Omog wakati akiifundisha Azam iliposhinda ubingwa mwanga 2013.


Phiri aliwahi kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara mbili 2004/05 na 2009/10

Amewahi kuwa kocha bora wa mwaka Tanzania 2009/10
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB